Ule mjadala mpana wa kisayansi unaoendelea jf kuhusu aya ndani ya kitabu kitukufu cha Quran,aya inayotaja JUA KUZAMA KATIKA TOPE JEUSI...Maelezo ya kina na ya kueleweka yamefafanuliwa vizuri katika video hii na Sheikh Suleyman Abbas,Mungu ampe kila jema Sheikh huyu.
Sheikh ameelezea kwa mapana sana jinsi Quran inavyotumia baadhi ya maneno ili kumpa nafasi binadamu apate kufanya tafiti zaidi,lakini pia iwe chachu kwa binadamu kuamini kwamba Quran ni maneno halisi ya Mungu mwenyewe muumbaji na kwamba si maneno ya Muhammad.
Kwa wale ndugu zangu tuliokuwa tunaikebehi Quran kwamba imekosea sasa hebu itazame video hii kwa nia ya kujifunza...utagundua kuwa Quran ni kitabu cha ajabu sana na kwamba hakuna neno wala jambo lililokosewa katika kitabu kile.
Hii ndiyo Quran tukufu,kitabu kisicho na shaka,kitabu kilichopokelewa na Mtume Muhammad s.a.w,mtume asiyejua kusoma wala kuandika.
Aya ilianza hivi:
83-Na wanakuuliza khabari za Dhul- Qarnaini. Waambie: Nitakusimulieni baadhi ya hadithi yake.84 -Sisi tulimtilia nguvu katika ardhi na tukampa njia za kila kitu.85 - Basi akaifuata njia. 86 - Hata alipo fika machwea-jua aliliona linatua katika chemchem yenye matope meusi. Na hapo akawakuta watu. Tukasema: Ewe Dhul-Qarnaini! Ama uwaadhibu au watwae kwa wema.”
Na sheikh Abbas anafafanua hivi: