Bi zandile
JF-Expert Member
- Sep 12, 2024
- 459
- 1,155
Kuna mambo mawili hapa ya kuthibitisha kuwa mtume hakuwahi kuwa katika mahusiano:
#1. Paulo alisema wazi kabisa kuwa alikuwa mseja (1Kor. 7:7-8).
Aliandika mafundisho mengi kuhusu ndoa mara nyingi sana - lakini kamwe hakuwahi kuandika kuhusu yeye mwenyewe kuwa katika ndoa.
Katika maandishi yake, alitofautisha kati ya waseja, wajane, na waliotalikiana. Alijitambulisha wazi kuwa yeye ni mtu pekee yaani aliyeamua kuishi kiseja.
#2. Biblia haisemi kuhusu mke au mtoto yeyote wa mtume paulo. Inataja wake za Petro na mitume wengine (1 Kor. 9:5) lakini kamwe haitaji mke wa Paulo.
Paulo aliwataja watu wengi kwa majina lakini hakutaja hata mara moja kuhusu mke wake au watoto wake, hakufanya hivyo kwa sababu hakuwahi kuwa katika mahusiano ya ndoa.
Ukimya wa Maandiko unazungumza kwa sauti kubwa - Paulo alitumikia katika utumishi bila kuoa , na alitumika vyema kabisa(1 Kor. 7:32-35).
Kuna wazushi fulani huzusha kwamba mtume Paulo alikuwa na mke ila walitengana - and ikiwa wewe ni miongoni mwao basi leta hapa uthibitisho wa ndoa ya mtume Paulo ukiambatanisha na maandiko.