Bi zandile
JF-Expert Member
- Sep 12, 2024
- 459
- 1,155
Unaelewa maana ya neno "wazushi "?Weka hoja za hao wanaodai kwamba kuna mistari inaonyesha Paulo alioa
Kama kuna dini ya Ukweli Paulo ndio atakuwa mtume wake mkuu kwa sababu hana makandokando mengi.Kuna mambo mawili hapa ya kuthibitisha kuwa mtume hakuwahi kuwa katika mahusiano:
#1. Paulo alisema wazi kabisa kuwa alikuwa mseja (1Kor. 7:7-8).
Aliandika mafundisho mengi kuhusu ndoa mara nyingi sana - lakini kamwe hakuwahi kuandika kuhusu yeye mwenyewe kuwa katika ndoa.
Katika maandishi yake, alitofautisha kati ya waseja, wajane, na waliotalikiana. Alijitambulisha wazi kuwa yeye ni mtu pekee yaani aliyeamua kuishi kiseja.
#2. Biblia haisemi kuhusu mke au mtoto yeyote wa mtume paulo. Inataja wake za Petro na mitume wengine (1 Kor. 9:5) lakini kamwe haitaji mke wa Paulo.
Paulo aliwataja watu wengi kwa majina lakini hakutaja hata mara moja kuhusu mke wake au watoto wake, hakufanya hivyo kwa sababu hakuwahi kuwa katika mahusiano ya ndoa.
Ukimya wa Maandiko unazungumza kwa sauti kubwa - Paulo alitumikia katika utumishi bila kuoa , na alitumika vyema kabisa(1 Kor. 7:32-35).
Kuna wazushi fulani huzusha kwamba mtume Paulo alikuwa na mke ila walitengana - and ikiwa wewe ni miongoni mwao basi leta hapa uthibitisho wa ndoa ya mtume Paulo ukiambatanisha na maandiko.
Unajitekenya na kucheka mwenyewe 🚮Unaelewa maana ya neno "wazushi "?
Nimetumia neno hilo ili kukusaidia uelewe kile ambacho Biblia inasema kuhusu maisha binafsi ya mtume Paulo kama alioa ama hakuoa.
Hoja za madai ya "wazushi" zimejumuishwa ndani ya neno "wazushi" so sina haja ya kukuwekea hapa hizo hoja ila ikitokea ukakutana na hoja zao popote pale basi rejea kwa hili bandiko ili uujue ukweli.
Kivipi?Unajitekenya na kucheka mwenyewe 🚮
Na hakuwahi kutumia vibaya michango yote ya hela (sadaka)..Kama kuna dini ya Ukweli Paulo ndio atakuwa mtume wake mkuu kwa sababu hana makandokando mengi.
Kwa mujibu wa maandiko ya Biblia, Paulo hakuwahi kuoa. Alichagua maisha ya uhuru ili kumtumikia Mungu kikamilifu.
Biblia haijaandikwa na mtu mmoja, ni mkusanyiko wa maandiko ya watu zaidi ya 40.Wazushi pia wanasema "PAULO MTUME WA MUNGU ALIKUFA" wakati Biblia haijaandika..
Upo sahihi mkuu.Kwa mujibu wa maandiko ya Biblia, Paulo hakuwahi kuoa. Alichagua maisha ya uhuru ili kumtumikia Mungu kikamilifu.
Nini tatizo?Mpk sijawowa na sina mahusiano
Ndo maana hawajaandika ndoa au kifo cha Paulo?Biblia haijaandikwa na mtu mmoja, ni mkusanyiko wa maandiko ya watu zaidi ya 40.
Tunataka maandiko wapi Yesu alisema msioweKwa mujibu wa maandiko ya Biblia, Paulo hakuwahi kuoa. Alichagua maisha ya uhuru ili kumtumikia Mungu kikamilifu.
Huwa unasoma Biblia?Ndo maana hawajaandika ndoa au kifo cha Paulo?
Kwani wapi tumesema Yesu anasema tusioe ?Tunataka maandiko wapi Yesu alisema msiowe
Wewe unachanganya na mafundisho au mapokeo ya waroman mapadri wao kutooa ,hayo ni mapokeo Yao sio maandikoTunataka maandiko wapi Yesu alisema msiowe