A
Anonymous
Guest
Watumishi wanaohama kutoka Halmashauri moja kwenda nyingine wanakabiliwa na changamoto ya mfumo wa PEPMIS, ambapo wanapohamishwa, asilimia zao za utendaji kazi zinaonekana kuanza upya kutoka sifuri, hata kama mtumishi alikuwa amefikisha, kwa mfano, asilimia 60 katika Halmashauri aliyotoka.
Hali hii ni changamoto kubwa kwa sababu muda wa tathmini huwa umeendelea, hivyo mtumishi anapohamia Halmashauri nyingine anakuwa na muda mfupi wa kufikisha asilimia zinazotakiwa. Matokeo yake, baadhi yao hukwama kupanda madaraja na kupata stahiki zao, licha ya kuwa walikuwa wakifanya kazi vizuri katika vituo vyao vya awali.
Pia, wakati mwingine uhamisho wa mishahara huchukua muda mrefu. Mtumishi anapofuatilia kwa Maafisa Utumishi, badala ya kupata suluhisho, huambiwa tu kuwa hajafikisha asilimia zinazohitajika kwenye PEPMIS.
Tunaomba TAMISEMI ifanyie kazi changamoto hii. Ikiwa mtumishi anahamishwa, kwa nini taarifa na alama zake za utendaji kazi zisihamishwe pamoja naye? Mfumo wa PEPMIS unapaswa kuwa na uwezo wa kusomana kati ya Halmashauri moja na nyingine ili mtumishi asiadhibiwe kwa sababu ya uhamisho.
Haiwezekani mtumishi akafanya kazi kwa bidii, akatimiza majukumu yake na kufikia viwango vinavyotakiwa, lakini mwisho wa siku akose stahiki zake kwa sababu ya changamoto ya mfumo.
Mfano, kuna mtumishi mwenzetu aliyehama kutoka Halmashauri moja ndani ya Mkoa wa Mbeya kwenda nyingine, na changamoto hii imesababisha kukwama kupanda daraja.
TAMISEMI, tunaomba suluhisho la kudumu. Uhamisho wa mtumishi usiwe sababu ya kupoteza historia yake ya utendaji kazi wala kunyimwa stahiki anazostahili.