Mtungie shairi lenye ubeti mmoja au zaidi mwanadada umpendaye hapa JF

Mtungie shairi lenye ubeti mmoja au zaidi mwanadada umpendaye hapa JF

Upendo wako kwangu ni zaidi ya maisha yangu
Sijakupenda leo tangia mwanzo wa life langu
Tupendane milele tuwashinde mpaka mwewe
Sweetlee we ni zaidi ya sweetheart kwangu.
[emoji7]
Waoooooh [emoji7][emoji7][emoji7][emoji7]
My everything [emoji131][emoji177]

Sent from my SM-N910T using JamiiForums mobile app
 
halihitaji hirizi,wala usijisumbuwe

watakupiga fitizi,wataka wakuganguwe

hao wote ni walozi,nimekupenda mwenyewe

pendo langu mimi nawe halihitaji hirizi


halihitaji hirizi,nimekupenda mwenyewe

sitaki masimulizi,,juu yako niambiwe

kwa hila za kibazazi,kwangu zitangonga jiwe

pendo langu mimi nawe halihitaji hirizi


halihitaji hirizi,tulia kwangu utuwe

tuama nita kuenzi,kama baba na mwanawe

moyo umekufa ganzi,stamani penginewe

pendo langu mimi nawe halihitaji hirizi


halihitaji hirizi,nikoseapo upowe

nijapo itaka razi,msamaha usikawe

niaminini laazizi,furaha yangu ni wewe

pendo langu mimi nawe halihitaji hirizi


halihitaji hirizi,kikubwa ni thaminiwe

kwako niwe mwenye hazi,mfano wangu pasiwe

kwenye wako usingizi,sura yangu ndio iwe

pendo langu mimi nawe halihitaji hirizi.


Kwako nimekufa nimeoza usinitese tafadhali Mshana Jr
 
Demiss usiamini anacho kiandika, lengo lake ni kupata tunda.
Mfungie vioo kabisa, kwanza ni mtu hatari huko kitunda.
Usifanye makosa tena, huyo anachojua ni kudunda,
Karibu kwangu kwenye raha,Kwa huyo utaishia ofisini kwa Makonda.
Aiseeeeh umeua
 
Back
Top Bottom