Mtungie shairi lenye ubeti mmoja au zaidi mwanadada umpendaye hapa JF

Mtungie shairi lenye ubeti mmoja au zaidi mwanadada umpendaye hapa JF

I prefer nisitungiwe shairi kuliko utungiwe ubeti very tasteless afu unalazimika kusema asante kuua soo.

Daadeqi.

Sikubali nakushushua weeeee ujiongeze.

Watasema maneno ya mkosaji but poa tu😛😛
[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23]
 
Huyi bwana nitaanza kumfatilia

mbalizi1 anaonekana hajambo.

KWA AJILI YAKO HII..

*Maumivu yasiyokwisha, daima chozi lanidondoka,
*Hata upendo ukiusitisha, kwako katu sitoondoka,
*Yaani hata ukinitisha, siwezi kuogopa,
*Japo napandwa na presha, ninapohisi umenichoka,

*We ndio yangu safina, mwokozi kwenye gharika,
*Bandari salama, NATIA nanga bila shaka,
*Panapo dhahama, mwili wako unanifunika,
*Penzi likienda mrama, naahidi nitawajibika,
 
Hahaaa. Aisee.

Na usiogope mwaya nakupa 'A' yako safi
 
*Moyoni sina amani, kama nchi za kiarabu,
*Kifikra nipo utumwani, nafsi inapata adhabu,
*Penzi lako kwa hisani, kupata bahati nasibu,
*Nakesha madhabahuni, labda utakuja kutubu,

*Roho yangu rehani, pumzi nazihesabu,
* sweetlee niondoe taabuni, upate dhawabu,
*Huu mwezi Ramadhani, ukikataa ni ajabu,
*Nikuhifadhi ndani, karibu usione aibu........
@sweetlee mkubalie mwenzio basi
 
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
HADITHI INAYOKUJA, NI YA SUNGURA SIKIA

Hadithi inayokuja, ni ya Sungura sikia,

Hadithi uliyongoja, leo ninakuletea,

Alitoka siku moja, njaa aliposikia,

Njaa aliposikia, Sungura nakuambia

Siku ile akaenda, Porini kutembelea,

Akayaona matunda, mtini yameenea,

Sungura akayapenda, mtini akasogea,

Mtini akasogea, Sungura nakuambia.

Sungura karukaruka, lakini hakufikia,

Matunda hakuyashika, mikononi hakutia,

Hakika alisumbuka, nguvuze zikapungua,

Nguvuze zikapungua Sungura nakuambia.

Mtazame hapo juu Sungura amelegea,

Mtazame na miguu, matunda anarukia,

Atafanya sikukuu, matunda akifikia,

Matunda akifikia, Sungura nakuambia.

Karuka tena karuka, matunda akarukia,

Mwisho wake akachoka, kachoka hata mkia,

Penye mti akatoka, pembeni akasogea,

Pembeni akasogea, Sungura nakuambia.

“Sizitaki mbichi hizi” Sungura akagumia,

“Naona nafanya kazi, bila faida kujua”,

Yakamtoka machozi matunda akalilia,

Matunda akalilia, Sungura nakuambia.

Sio kama hakutaka, sasa nakupasulia,

Matunda aliyataka, ndiyo kisa akalia

Tunajua hakufika, alichoka kurukia,

Alichoka kurukia, Sungura nakuambia.

Hadithi nimemaliza, nimekwisha simulia,

Jambo moja sikiliza, rafiki yangu sikta,

Usikose kujikaza, mazuri kukazania,

Utamshinda Sungura, utapata mbivu hizi.

Hili shahiri liendee wanaume wa jf wenye tabia za sungura huyu.
Yaan umeambiwa umtungie umpendaye ukamtungia sungura [emoji23][emoji23][emoji23]
 
Back
Top Bottom