Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 5,352
- 15,876
TAARIFA KWA UMMA
Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Mtwara (MTUWASA) inapenda kutoa ufafanuzi juu ya taarifa iliyochapishwa kupitia ukurasa wa JamiiForums tarehe 01/06/2026 kuhusu maunganisho ya huduma ya maji Mbae Mashariki.
Hoja ya Mdau ~ Wakazi wa Mbae (Mtwara Majini) tumeomba kuunganishiwa maji tangu 2022, MTUWASA hawatujibu wala hawaji 'site'
Eneo la Mbae Mashariki ambalo lipo katika Kata ya Ufukoni awali lilikuwa na shida ya upatikanaji wa maji kwa wakati. Katika kulishughulikia hilo Mwaka 2022 Serikali kupitia Wizara ya maji ilileta mradi kwa ajili ya kutatua changamoto hiyo ambapo hadi sasa tayari eneo la Mbae Mashariki ikijumuisha maeneo ya Mbae Chundi, Mbae Kiholo, Mbae Kawe, Mbae Kalifoni na Libya yameshafikiwa na huduma ya maji, maeneo ya pembezoni yaliyosalia ambayo wananchi wameomba kusogezewa huduma ya maji tayari Mkandarasi yupo site kwa ajili ya kuongeza mtandao wa maji ili kuwafikia wananchi hao. Aidha kazi hii inatarajia kukamilika ndani ya miezi mitatu ijayo.
MTUWASA inawahakikishia wananchi wa Mtwara Mjini wanaofaidika na huduma ya Majisafi na Salama, kuwa inaendelea na utekelezaji wa miradi mbalimbali ili kuhakikisha hali ya upatikanaji wa majisafi na salama inaimarika, pia Mamlaka imejizatiti katika usimamizi wa Miradi hiyo ili ikamilike na kunufaisha jamii kama ilivyokusudiwa.