MTV Music Awards June 6th, 2014

MTV Music Awards June 6th, 2014

Naam tulikuwa tunasubiri hiki kimbunga cha diamond kiishe na sasa ally kiba is coming to take over!!!


Aje tuone, mpaka afikie alipo mwenzie alinacha atakuwa kagutuka ndotoni, by the way be strong diamond z a splendid way 2 ure flying over, u'll done viva viva viva..
 
Wanaija muziki wao wa kawaida sana trust me bro,promotion ndio kila kitu jamaa wanapromoti sana mzk wao alfu kwenye tuzo za kupigiana kura kama hizi huwezi kuwaangusha coz population yao pia ni kubwa...

Diamond amejitahidi kiasi chake na anastahili pongezi lakini siafiki kwamba wingi wa wanigeria ni kigezo cha kuwapa ushindi! Unamfahamu Keinan Abdi Warsame ( K'naan) wa Ethiopia? Amekuwa akishinda tuzo despite kupambanishwa na wasanii toka nchi zenye population kubwa kuliko yake!! Kipaji na muziki mzuri kama vipo vitaonekana tu akaze buti..
 
ndomo ni mtz mwenzangu, ananiwakilisha kimataifa na wala hanifahamu maskini ya mungu na nilikuwa nataman achukue ila nilikuwa na hofu akichukua itakuaje? ingekuwa shida sana hapa mjini kwa upande flani bora alivyokosa!



Sugua goti kumwombea apate BET kihoro cha kushindwa si mchezo but kwa competition ile ndomo anasubiri sana
 
Hii kauli kuna wadau huku mtaani kwetu nimewaambia ila hawanielewi. wao wanasoma magazeti ya shigongo wakimaliza wanasikiliza clouds wakimaliza wanalala, sasa wanadhani diamond ni msanii mkubwa kuliko mafikizolo na davido.

dawa yenu tatizo moja la watanzania wengi akili zetu zimeharibiwa na maisha magumu hata 1+1= utambiwa 11!!!
 
Tumelamba tuzo ya gani?mtanzania mzungu huyu alichukua gamba la tanzania ili apate fursa kumiliki ardhi
Hivi kweli wabongo hawamjui huyu mhindi{ Ashish Thakkar}, huyu ndiye amenunua kituo cha oysterbay police anataka kujenga mall pale
 
Diamond amejitahidi kiasi chake na anastahili pongezi lakini siafiki kwamba wingi wa wanigeria ni kigezo cha kuwapa ushindi! Unamfahamu Keinan Abdi Warsame ( K'naan) wa Ethiopia? Amekuwa akishinda tuzo despite kupambanishwa na wasanii toka nchi zenye population kubwa kuliko yake!! Kipaji na muziki mzuri kama vipo vitaonekana tu akaze buti..

dah! mkuu you are GREAT THIKER heshima kwako wingi wa wanaigeria sio kigezo cha sisi kukosa mtv awards I SALUTE YOU!!!!!
 
Kwa tuliozoea discriminations hilo halitupi shida wanaostahili hawastahili na wasiostahili wanastahili...

That is life cha kushukuru maisha yanaendelea....

Ila mshauri h.o.d abadili aina ya publicity inamfanya domo aonekane ni mtu wa ligi za mchangani kwa maneno yake ya shombo

Dai atafute watu wenye weledi uliotukuka na wanaojua kufanya publicity, asilete urafiki kazini

HOD huwa akileta ishu ya Dai najikuta hata huyo Dai nachukia kazi zake ila kiukweli Dai anajua, jamaa amebadilisha aina ya muziki wa Tanzania

Arudi ajipange hasa, beefs na skendo zinaharibu sana kwenye kugawa mashabiki.
 
msomeni Edo hapa.....

By Edo Kumwembe (Facebook page)

read this piece...nimeandika leo
Mwanaspoti


Kuanzia Okocha, Ramsey, sasa Davido
na edo kumwembe
KATIKA dimba la uwanja wa taifa wa Ufaransa,
maarufu kama Stade de France, Juni 28,
1998, Watanzania walikuwa wameganda
katika luninga zao wakishindwa kuamini kuwa
timu ya Afrika waliyokuwa wanaishabikia
katika kombe la dunia ilikuwa imekufa
mabao 4-1 kutoka kwa Denmark.
Ndio, kama ilivyo kwa Waafrika wengine,
Watanzania walikuwa wamejipa ushabiki wa
timu ya taifa ya Nigeria. Lakini Peter Moller
akaipatia Denmark bao la kwanza. Brian
Laudrup akaipatia bao la pili, Ebbe Sand
akaipatia la tatu, Thomas Helveg akaipatia la
nne. Dakika mbili baadaye, Tijani Babangida
akaipatia Nigeria bao la kufutia machozi.
Kwanini Watanzania tulikuwa mashabiki wa
Nigeria? Kwanza kabisa walikuwa
wametukosha katika fainali za kombe la
dunia mwaka 1994 nchini Marekani. Pili
wakatukosha kwa kutwaa medali ya dhahabu
ya Olimpiki pale Atlanta Georgia Marekani.
Hata baada ya kupigwa na Denmark
Watanzania wakaendelea kuwa mashabiki wa
Nigeria. Mpaka leo bado wapo mashabiki wa
Nigeria nchini. Mashabiki wa damu. Lakini
unadhani wanigeria wana tofauti kubwa
kisoka na sisi? Hapana.
Wanigeria wanajituma katika kuhaha kutafuta
maisha. Taifa lao lina watu zaidi ya milioni
170 kwa sasa. Kila Mnigeria anajituma kadri
anavyoweza. Huyu anatapeli, yule anacheza
soka, huyu anaimba, mwingine anaanzisha
dhehebu feki la dini. Ili mradi mkono uende
mdomoni.
Na ni kwa njia hii ndio Wanigeria
wametugeuza kuwa mashabiki wao. Vipaji vya
wachezaji wao ni hivi hivi vya wachezaji wetu.
Tofauti ni katika kutafuta maisha. Yakubu
Aiyegbeni ndiye Edward Chumilla.
Waliomuona Sunday Manara
hawamtofautishi sana na Jay Jay Okocha.
Peter Rufai alikuwa kipa wa kawaida asiyefikia
uwezo wa Mohamed Mwameja wala Riffat
Said. Hata mabao manne waliyofungwa na
Denmark alichangia kiasi kikubwa kufungisha.
Baada ya soka lao, Watanzania tulihamia
katika filamu zao. Mama zetu, dada zetu, na
watoto zetu wakahamia katika kupenda
filamu za Kinigeria. Ukweli ni kwamba
hawakuwa na jipya sana ambalo sisi
hatukuwa nalo.
Mastaa wao Nouah Ramsey, Desmond Elliot,
John Okafor, Ini Edo na wengineo wana
vipaji ambavyo Tanzania vilionekana tangu
zama za akina Bishanga na wengineo. Tatizo
ni uwezo wa Wanigeria kubuni vitu viwili
vitatu kama vile kuingiza mambo mengi ya
kishirikina ambayo tulikuja kuyaiga.
Hata hivyo maudhui yao ni yale yale ya
kawaida ambayo wacheza filamu wetu
wameyazoea. Mara nyingi unakuta mtoto wa
tajiri amempenda maskini. Hakuna jipya
sana. hakuna sehemu ambayo wanaweza
kuangusha ndege kama Hollywood
wanavyofanya na filamu zao za kusisimua.
Tatizo hapa wacheza Filamu wetu hawajitumi.
Wengi hawana vipaji wala elimu. Wanacheza
filamu kwa sababu walikuwa Mamiss,
wanamitindo au wamerudi kutoka katika
shindano la Big Brother. Vinginevyo
hatuangalii vipaji. Tunaangalia wauza sura.
Matokeo yake tumejikuta tumerudi kuwa
mashabiki wa Filamu za Kinigeria bila ya
sababu za msingi. Hakuna unachoweza
kufanya zaidi ya kucheka. Mcheza filamu yuko
bize na matajiri kuliko kujikita katika kazi
yake apate pesa za kuwa tajiri.
Lakini kama vile haitoshi, baada ya Wanigeria
kutuchukua kutoka katika soka na Filamu,
sasa wametuteka katika muziki. Nenda katika
baa maarufu popote Tanzania, au nenda
katika ukumbi maarufu wa Disko ukasikie
jinsi nyimbo za mwanamuziki Davido wa
Nigeria zinavyotuteka.
Wimbo wake wa Aye kwa sasa ni kama
nyimbo ya taifa ya Muziki. Kabla ya hapo
wimbo wake wa Skelewu ulikuwa gumzo
lililopitiliza. Lakini ukichunguza sana katika
nyimbo zake, hakuna cha ajabu ambacho
Watanzania hawawezi kufanya.
Wimbo wa Aye unamuonyesha akiwa
shambani. Lakini kama Diamond Platinumz
akipiga nyimbo inayomuonyesha akiwa
mashambani watu watapuuza. Hata yeye
mwenyewe hataki. Aliwahi kufanya wimbo
mmoja akiwa kijijini, lakini haukuvuma.
Na ndio maana sasa anafanya video za
kifahari Afrika Kusini ambapo anaonekana
akirekodiwa kutoka angani na vifaa vya
kisasa. Kwanini Davido anatuteka zaidi ya
Diamond? Kwanza ni kwa sababu ya kupenda
Unigeria ambao umetuingia.
Lakini pili wenzetu wamefanikiwa kujitangaza
kimataifa. Vipaji ni vile vile tu, lakini kama P
Square wanafanya wimbo na Ricky Ross huku
wewe unamtafuta Jackline Wooper na
kujaribu kumfanya kuwa mwanamuziki ili auze
sura katika wimbo wako wakati hana kipaji
chochote cha muziki.
Muziki wanaoufanya Wanigeria tunaweza
kuufanya. Mimi ni mmoja kati ya watu
wanaoamini hilo. Tatizo ni wanamuziki wetu
kukosa ubunifu, au Watanzania wenyewe
kuwa wepesi katika mapokeo....​


 
dah! edo kaongea ukweli kaka wanaigeria ni watu wanaojivunia cha kwao sio wabongo kiukweli hata huyo diamond anaiga style za nigeria halafu anataka kushindana na davido inashangaza sana!!!!!
 
Bendera ya tz kimataifa itapeperushwa na injili kutoka tz wala sio muziki, au mpira au chochote kile tofauti na injili
Note hcho

Na wewe acha bange, nani kakwambia injili inatoka TZ?
 
Hivi Wa Ethiopia wako wangapi vile???

Tukirudi kwenye mada Diamond kaza buti; wewe bado ni hero na ni number one Tz! usione kina P Square wapo hapo walipo walikuwa wanapewa maneno ya kashfa haya usomayo humu cha mtoto....lakini leo hii hao hao wanaigeria waliokuwa wanawadharau wanawapigia salute....Kawaida yetu waafrika kukubalika home ni kazi kweli kweli...

Chukulia negative comments kama changamoto...ili utakapokuwa another level usome tena hizi comments uanze kuwacheka...


Diamond amejitahidi kiasi chake na anastahili pongezi lakini siafiki kwamba wingi wa wanigeria ni kigezo cha kuwapa ushindi! Unamfahamu Keinan Abdi Warsame ( K'naan) wa Ethiopia? Amekuwa akishinda tuzo despite kupambanishwa na wasanii toka nchi zenye population kubwa kuliko yake!! Kipaji na muziki mzuri kama vipo vitaonekana tu akaze buti..
 
ila tuongee ukweli jamani hivi kweli tuzo ataacha kupewa mafikizolo ambaye kule nyumbani kwake apewe mtu mwingine??Sikutegemea sana hiki kitu, also Davido ypo mbali sanaa kuliko Diamond.
 
dah mazee imenipain sana kuona kijana wetu hajapata hata moja , ila am proud bado labda b.e.t atapata
 
Ivi huyo Dimond mnaesikitika kakosa anaimba nini cha ajabu... ukiangalia Mafikizoro utagundua ni typical south Africna music Ukimwangali Davido typical Nigerian music sasa Huwa napata shida kutambua huyu kijana wetu anaimba nini halafu kuna watu mnatoa pofu eti Davido wa kawaida sana show alizofanya Davido kwa Africa peke yake Diomond hata robo hafiki kumbuka kila anakoenda kufanya show anapata Mashabiki so ikitokea kupiga kula kama hivi ni lazima ashinde.... halafu jamani pia lugha nayo katika music inaplay big role. Kijana kajitahidi lakini safari yake kama ataendelea kubebwa na Mawingu Studio the only tuzo atakayobeba ni kili Awards Clouds ni washenzi sana wanamtumia dogo kujinufaosha badala ya kumtangaza kijana Africa nzima
 
mnafatilia vipindi vya mtv lakini? vinatoa sapot sana kwa naija na south a.
kuna top ten special kwa ajil ya naija.. special interviews kwa ajili ya naija.. hata kwenye spankin new kidogo kulikua na utata ila now ndo wana2pia macho kotekote..afu ukifatilia mtv inaonekana africa nzima.. angalieni schedule ya vipindi vyao then mlete mrejesho hapa..davido ataendelea kuchukua chake hadi bas!! mi ile naiita MTV NAIJA na sio Africa,maana hata east africa wametusahau dah!!

hapa matumain yapo bet.
 
Yaan kumshindanisha diamond na davido ni sawa na kushindanisha shule ya kata na Marian girls
 
Back
Top Bottom