MTVBASE east kimetumia lisaa 1 kupiga ngoma za diamond

Hziyech22

JF-Expert Member
Joined
Jun 8, 2019
Posts
15,351
Reaction score
21,362
Kituo kikubwa Cha entertainment Cha MTVBASEeast kimetumia saa 1 kupiga ngoma za diamond pekee Kama sehemu ya kumwish happy birthday msanii wa kimataifa Diamond Platnumz kutoka Tanzania ambaye amefikisha umri wa miaka 30 siku ya leo.
 
Hao mtv base wangepata mashairi ya nash mc au dizasta wangejuta kupoteza muda wao kupiga mumble music
mziki si mashairi....kumbuka enz zile zakina awilo wanatamba ...tulikua hatuelewi lugha but mziki ulienda....akaja Cabo snoop na Windeck na prakata Dumba yake watu walizielewa...so jifunze zaidi nini maana ya mziki na nini maana ya poems au mashairi au tenzi
 
Dizasta vina au Nash ni wasanii wanaofanya muziki mgumu kutoka kwa lugha isiyofahamika na wengi.
Mkuu lugha isiyoeleweka unaipimaje? unaweza kuniambia maana ya kwangwaru?? Mziki wa nash ni moja ya mziki makini usio kua na shaka katika usahihi wa lugha
.
Tanzania haina msingi mzuri wa Hip hop, Rosa ree huyu hapa anafanya kwa kizungu na Kiswahili kapepea sasa ni international Singer, anawashirikisha wasanii wa aina tofauti tofauti hata usipomuelewa utapenda melody
Nash alisema Kwa isani ya promo mnarudi utumwani haujui siri yeyote unaandika kwa hisani ya kusikika hewani...kaandika kuhusu matumizi ya kiswahili kwenye fani ya ushahiri, chanini kingereza? Jiulize tumia akili maana fikra sahihi huja kwa lugha asili.

Kwa mfano kuna jamaa fulani anaitwa carbo snoop alitamba miaka fulani hapa bongo kwa nyimbo yake ya parakata tumba lakini bado alikiki sio kwamba lugha yake ilikua ni rahisi au inayofahamika sana, mi mpaka leo sijajua ile ni lugha gani

Ili uweze kua International huitaji kutumia kingereza ili watu wajue unachokiwasilisha luis fons kaimba despacito saizi ina views bilion 6. Sasa jiulize je katika hao bilion 6 wote wanajua lugha ya kispanish?? je hiyo inamaana kua luis ni international sana kuzidi drake au chris brown ambao hawana hizo views katika hit song zao???
.
Kuna mtu anaitwa Phyno na Sarkodie hawa wote wanaimba kwa lugha za makabila yao ila wamepenyaa kwa sababu waliwashirikisha wasanii wakubwa, video wanafanya kali, melodies kali.

Hapa ndio tatizo linapokuja kua wasanii wengi wanafanya hivyo kwa hisani ya kusikika tu hewani no matter anaimba nini na ndio sababu wanajumuishwa kwenye list ya mumble rappers and singer



Dizasta alipata meneja lakini katika vitu ambavyo hakua tayari kuvifanya ni kuharibu utaratibu wake aliojiwekea wa kuto vunja miko ya hip hop. Halafu meneja anampanga kua kitu flani ufanye na kitu flani usifanye kitu ambacho hakua tayari kukifanya na kubidi mkataba uvunjike
 

Hahaha umenikumbusha kuna mdau nimetoka kumjibu hivyo hivyo kuhusu huyu carbo snop aiseee umenifanya nicheke tena baada kuiona hii coment yako

Mzee mashairi yana nafasi yake katika tungo. Hivi bila mashairi mazuri yenye mafunzo unafikiri profesa jay na feruzi wangepata ile tuzo waliyopewa na mkapa?? Bila mashairi yenye funzo twent percent angepewa tuzo??

Mashairi yana nafasi yake mkuu
 
Unafanya dhambi kubwa sana kumfananisha msanii namba moja Africa na hao masela mavi.
Nyegezi, kwangwaru, kanyaga, ichomekee kwa ndani, paka mate ni teleze and others mumble verses ni zaidi ya mavi
 
Lugha inayoeleweka na wengi mfano Kiingereza na Kifaransa.
Lugha katika sanaa wala haina mashiko we ushawahi kujiuliza chali champlin alivyo hit katika movie zake ambazo hazina sauti wala lugha?


Kwangwaru sijui maana yake.
Ila content ya nyimbo naijua
kwani kwangwaru sio sehemu ya content??


sawa tuko pamoja



Hadhira anayoilenga Nash MC kwenye hiyo ngoma ni waswahili waliokwenda shule hata kidogo yule ambaye hajasoma hawezi muelewa Nash.
Hapana mashairi yake yamekaa kimtaani sana na wala hayahitaji elimu kuyaelewa maana ndiyo culture ya hip hop ilipoanzia. Rejea kina pac kina biggie mashairi yao yamekaa ki gangsta yanayolenga changamoto zinazoikumba jamii.

Yaani Bora ungesema mashairi ya mrisho mpoto ndiyo ningekuelewa

Kaimba Kireno hakuna aliyeelewa maudhui ya ile ngoma TZ ila ilipendwa kwa sababu ya style yake ya uimbaji, dancing style na melody ya maana.
Kwaiyo umekubali kua ugumu wa lugha sio kigezo cha kukubalika international industry??

Unafikiri watu wote wanaomsikiza koffie olomide wanajua maana ya ekotite?? Lakini mbona watu wanaskiza ngoma zake japokua lugha ni ngumu kwao?


Original version haina viewers B6 bali remix aliyomshirikisha Justin Bieber.
Alafu ile ngoma hata ingeimbwa kisukuma ina melody kali.
Ngoma gani ya Nash ina melody ya maana?
Hapa mzee umeyumba inaonekana unabisha bila kua na hata reference, nilikuacha nikajua utafanya edit hapa ujikoseo mwenyewe lakini nilichokijua hukuandika kwa bahati mbaya.

Despacito original ina views bilion 6.4

Beats za Duke zile kavuuu hazina hata mixing ya maana.
hapa nazungumzia mashairi mzee sio mixing na blah blah zakibana pua, mziki ukishindwa kuufanya uwe mzuri kwa mashairi bila kutegemea mixing hustaili kuitwa msanii hapo sifa inaenda kwa prodyuza.

Wengi wenu hua mnafata biti na ndio maana hata mkiimbiwa kwangwaru kwwnye beat linalokita utaipenda tu

Ukitaka beats na mixing nenda kasikize trap
Nchi ambayo mamaneja ni ma-demager
Eti trap beats ndo kipenzi cha mateenager



Tumependa melody aina ya uimbaji uliotumika ukimjumlisha na Justin ndo balaa jingine.
hapa hoja yako imekosa nguvu kwasababu imesimama katika msingi potofu kudhani kwamba despacito ya remix ndiyo ina views billion 6
.
Ile ngoma ina remix na cover za kutosha kwa malugha tofauti tofauti, ngoma gani ya Nash utaitengenezea cover kwa beats zake?
Ukishasema malugha tofauti tofauti hapo unajikosoa mwenyewe kua mziki sio lugha, hivyo hata nash kwa lugha ya kiswahili anauwezo wakutusua na watu wakafanyia cover na remix

Enrique Iglesias anaimba lugha zaidi ya nne ila hata akiimba hicho kispanish lazima utapenda tu maana anaimba vizuri ma anatumia beats kali.
we umesema lugha ngumu inafanya mziki usitambulike halafu tena unasema enriquei akiimba kispanish lazima nipende. Nikueleweje mbona undefined sana kama sigara kali??
.
Kendrick Lamar anaimba Hip Hop ila hatumii beats za ajabu ni rahisi kusikilizika na hata asiyependa huo muziki
ma teenager ndio wanaofat beats ila ma legends hufata mashairi, na ndio maana utaona legend wa hip hop anahesabika kama tupac japokua beats zake ni mbovu kulinganisha na huyo lamar


Ngoma ya Nash unaweza kuilinganisha angalau na Ngoma ya Fid Q Mwanza?
kimashairi au kimdundo??

Hivi unaelewa kua fid Q saizi kapunguza fleva ya hip hop amekua sio fid Q yule wa zamani?

Madee aliimba Hip Hop hailipi wala haiuzi.
Yeye nani bwana kama kina Joh walikuwa wagumu Fid lakini now wame switch kuja kwa commercial Hip Hop.

hip hop haiuzi au wewe ndio huuzi??

Wanakuambia zoea msoto ili ushinde komaa na msoto maana msoto ndio utaokufua na katika gemu sio wote watamaliza dakika tisini. Rejea ule usemi ule unaosema kua baada ya sungura kushindwa kuzichuma ndizi akasemaje??? Alisema sizitaki mbichi hizi, na hivyi ndivyo alivyofanya madii


Yes lazima meneja akupangie si anataka arudishe pesa yake.

Amenikuta nafanya mziki gani mpaka akashawishika kuni dhamini?? Na kwanini anipange kunilazimisha nifanye

Kama anataka arudishe pesa zake awekeze kwenye madini au miradi mingine sio uwekeze halafu uue talent ya mtu na siku zote mtu anayeweka maslahi mbele kuliko kujali interest ya mtu huyo ni snitch. Sasa hip hop na usnitch wapi na wapi??

anachokitaka ambacho sio interest yake
Meek Mill alikuwa akiimba Gang rap yani ile ngumu akawa hana mbele wa nyuma kazi ikawa kuwachania polisi tu akikamatwa sasa hivi unaiona Hip Hop anayofanya?
yaliyo nyuma ya pazia katika ishu ya meek mill hadi kupelekea kufungwa jela ni swala la ugomvi kati yake na police aliyetaka kuwa manager wake lakini yeye hakutaka na ndio maana hizo diss track kwa mapolis zilikua hazikauiki

.
Melody kali yani daaah! Sikiliza ngoma za kikorea au kwetu Japan melody tamuuu

Mbona unanichanganya tena? kikorea na kijapani ni lugha ngumu na wewe umesema lugha ngumu haifanyi mziki ukubalike international halafu unaniambia nisikilize ngoma za kikorea nikueleweje??

 
Mzee hizi ni dharau na roho mbaya + chuki za kishamba.
naongea ukweli sidharau na tukianza ku confess nani aliyedharau utagundua ni yule jamaa aliyewaita hip hop artists masela mavi.

Ungekua kweli we ni muingwana usiependa dharau yeyote haijalishi nani anadharauliwa basi ungepaza sauti kumkemea huyo jamaa. Ila kwakua kadharau watu ambao unawadharau hivyo inakuwia vigumu kukemea.

Kiukweli leo umeonesha usimba na uyanga
.
Young Lunya anaimba Real gang hip hop alitaka kufanya remix ya Kanyaga we unaita ma.vi seriously?

na ndio maana alitaka ila hakufanya


Kuna utofauti kati ya kutaka na kufanya, pengine alitaka kufanya ila baada ya kuichunguza akagundua ni nyimbo mbovu na itamshushia hadhi endapo ataitolea remix na ndio maana aka skip


naweza kukwambia jay z alitaka kufanya collabo na nikki mbishi lakini haimaanishi kua alifanya collabo
Beats za hizo ngoma unazisikia sikia vipi yani?
Beats sio kitu hata singeli wanazo, huyo jamaa yako ana beats hadi ya taarabu. Kama una interest na beats basi sikiliza dubsteps au msikize marshmallow na allan walker ila ukitaka mashairi huko huyakuti

Mshauri Nash akagonge beats kwa producers wanaoeleweka afuate mfano wa Baba Shaka Zulu Gosby

kipaji ni kipaji tu mzee, unataka kuniambia diamond anabebwa na beats sio??

Mafatilie joyner lucas au tech9ine utajifunza vingi na utajuta kupoteza muda wako kusikiliza huo upupu wa dzain ya kwangwaru
 

Hacha mbalil kote huko mkuuu siku hizi yupo Dogo anaitwa Fally na InnosB...hatuelewinkitu ila tunakata mauno kama kawa.
 
Hiii population ni ya duniani tu au na mbinguni na kwingineko?,6.4B....daahhhh!!!!
 
S
Mbona Sky Sports walitumia wiki nzima kuonesha game za Ali Kiba ila hatukusema.

Ali Kiba hapendi show off.
Sasa wewe ulishindwaje kuja hapa nakutumbia haya acha wivu wa kike
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…