MTVBASE east kimetumia lisaa 1 kupiga ngoma za diamond

MTVBASE east kimetumia lisaa 1 kupiga ngoma za diamond

Mkuu lugha isiyoeleweka unaipimaje? unaweza kuniambia maana ya kwangwaru?? Mziki wa nash ni moja ya mziki makini usio kua na shaka katika usahihi wa lugha
.

Nash alisema Kwa isani ya promo mnarudi utumwani haujui siri yeyote unaandika kwa hisani ya kusikika hewani...kaandika kuhusu matumizi ya kiswahili kwenye fani ya ushahiri, chanini kingereza? Jiulize tumia akili maana fikra sahihi huja kwa lugha asili.

Kwa mfano kuna jamaa fulani anaitwa carbo snoop alitamba miaka fulani hapa bongo kwa nyimbo yake ya parakata tumba lakini bado alikiki sio kwamba lugha yake ilikua ni rahisi au inayofahamika sana, mi mpaka leo sijajua ile ni lugha gani

Ili uweze kua International huitaji kutumia kingereza ili watu wajue unachokiwasilisha luis fons kaimba despacito saizi ina views bilion 6. Sasa jiulize je katika hao bilion 6 wote wanajua lugha ya kispanish?? je hiyo inamaana kua luis ni international sana kuzidi drake au chris brown ambao hawana hizo views katika hit song zao???
.


Hapa ndio tatizo linapokuja kua wasanii wengi wanafanya hivyo kwa hisani ya kusikika tu hewani no matter anaimba nini na ndio sababu wanajumuishwa kwenye list ya mumble rappers and singer




Dizasta alipata meneja lakini katika vitu ambavyo hakua tayari kuvifanya ni kuharibu utaratibu wake aliojiwekea wa kuto vunja miko ya hip hop. Halafu meneja anampanga kua kitu flani ufanye na kitu flani usifanye kitu ambacho hakua tayari kukifanya na kubidi mkataba uvunjike
bila shaka wewe ndo Nas Mc mwenyewe
 
Dizasta vina au Nash ni wasanii wanaofanya muziki mgumu kutoka kwa lugha isiyofahamika na wengi.
.
Tanzania haina msingi mzuri wa Hip hop, Rosa ree huyu hapa anafanya kwa kizungu na Kiswahili kapepea sasa ni international Singer, anawashirikisha wasanii wa aina tofauti tofauti hata usipomuelewa utapenda melody.
.
Kuna mtu anaitwa Phyno na Sarkodie hawa wote wanaimba kwa lugha za makabila yao ila wamepenyaa kwa sababu waliwashirikisha wasanii wakubwa, video wanafanya kali, melodies kali.
.
Nash Mc atamshirikisha Songa, Songa atamshirikisha Gifted son, Gifted son atamshirikisha Kimbunga, Kimbunga atamshirikisha Kalapina, Kalapina atamshirikisha Rais wa magwangala, Rais atamshirikisha One the incredible, One atamshirikisha Nik mbishi, Nik atamshirikisha Gheto ambassador, Geto anamcheki mansulii alafu wataaanza kujirudia hivyo hivyo
Hahaha you made my day
 
Mkuu mimi ndio maana nimebakiza nyimbo za zamani tu
Kuna upuuzi mwingine kutoka WCB unaitwa "chuchumaa" wa rayvanny. Yaani hii bongo fleva siku hizi ni upuuzi mtupu full Matusi halafu watu wanasema mziki wetu unakuwa.

Hongera sana kwa kuskiliza ngoma za zamani na hizo ndio ngoma za kuskiliza.
 
Kiukweli ukweli ndio huo japo watu hawapendi kuusikia

Diamond kipindi anaforce kutoka alikua anaimba fact sana, mfano ile ngoma ya nitarejea ina madini ambayo yaliendana na jina lake.

Ila alivyotoka tu amekua akitumia jina lake no matter ataimba nini anajua watu watapenda tu
Kwangu mimi ukiniuliza ngoma kali ya muda wote kutoka kwa bwana Alimasi ni hiyo Nitarejea. Kwanzia audio mpaka video kila kitu kimetulia, kwanzia maudhui mpaka melody vyote vimepangika na anaimba huku ametulia kabisa.

Nitarejea ni moja wapo ya ngoma ambazo sijawahi kabisa kuchoka kuziskilza, tofauti na hizi ambazo anazikanyaga kanyaga tu siku hzi zinazodumu maskioni mwa watu kwa miezi kadhaa.
 
Mtu anakuambia kiswahili ni lugha ambayo haivutii kutangaza kazi zako ki international, halafu tunamuona hadi beyonce kaweka maneno ya kiswahili katika nyimbo yake.

Pia american got talent kuna wazungu waliimba nyimbo ya dini kwa kiswahili hadi mimi nisiyeamini mambo ya dini niliikubali ile nyimbo kama hiyo haitoshi kuna malengends kama michael jackson wanaojulikana kidunia na wenye record kubwa kuzidi pimbi yeyote unayemjua ana ngoma yake ya Liberian girl aliyoweka vionjo vya kiswahili ndani yake halafu leo anakuja mpogoro anasema kiswahili sio lugha makini katika international

Juzi hapo joyner lucas katoa wimbo na tory lanez katika verse zake kapachika maneno ya kiswahili "hakuna matata" na hili neno limekua trend sana huko ughaibuni kuliko hata sisi wenye lugha yetu
Daah.. Nimefurahishwa sana na Joyner Lucas kutumia maneno ya kiswahili kwenye track yake, lakini pia nimeumizwa na maneno yenyewe aliyotumia"hakuna matata" hili neno linatumika sana Kenya na hapo ni kama amewapa shavu wakenya na hii itazidi kuiaminisha dunia kuwa kiswahili ni cha wakenya.
 
naongea ukweli sidharau na tukianza ku confess nani aliyedharau utagundua ni yule jamaa aliyewaita hip hop artists masela mavi.

Ungekua kweli we ni muingwana usiependa dharau yeyote haijalishi nani anadharauliwa basi ungepaza sauti kumkemea huyo jamaa. Ila kwakua kadharau watu ambao unawadharau hivyo inakuwia vigumu kukemea.

Kiukweli leo umeonesha usimba na uyanga
.


na ndio maana alitaka ila hakufanya


Kuna utofauti kati ya kutaka na kufanya, pengine alitaka kufanya ila baada ya kuichunguza akagundua ni nyimbo mbovu na itamshushia hadhi endapo ataitolea remix na ndio maana aka skip


naweza kukwambia jay z alitaka kufanya collabo na nikki mbishi lakini haimaanishi kua alifanya collabo

Beats sio kitu hata singeli wanazo, huyo jamaa yako ana beats hadi ya taarabu. Kama una interest na beats basi sikiliza dubsteps au msikize marshmallow na allan walker ila ukitaka mashairi huko huyakuti



kipaji ni kipaji tu mzee, unataka kuniambia diamond anabebwa na beats sio??

Mafatilie joyner lucas au tech9ine utajifunza vingi na utajuta kupoteza muda wako kusikiliza huo upupu wa dzain ya kwangwaru
Mtu kama Joyner Lucas hata ngoma yake isipokuwa na beat bado utairudia rudia kuiskiliza, kwa watu wasiomfuatilia wala kumjua huyu mshikaji wanakosa vitu adimu sana kwenye hip hop.
 
Back
Top Bottom