Mtwara: Askari Polisi mmoja kati watuhumiwa wa mauaji ya mfanyabiashara alikutwa mahabusu akiwa amejinyonga tarehe 22 Jan 2022

Yaani Maabusu 7, wamefungiwa chumba Kimoja then mmoja akutwe amejinyonga, lipo jambo hapa, kwa ufahamu wangu mdogo ni kwamba mahabusu inakuwa na vyumba viwili yaani cha wanaume na wanawake ikiwa expanded zaidi kuna kuwa na mahabusu ya watoto wa kiume na watoto mahabusu wa kike, hakuna uwezekano wa mahabusu mmoja kukaa chumba chake peke yake, hii ina maana kuwa mahabusu inayedhaniwa amejinyonga hakuwa amehifadhiwa peke yake kwenye chumba, Maswali yangu;

i/ wakati anajinyonga hao wengine 6 walikuwa wapi?
ii/ Polisi wa zamu alikuwa wapi?
iii/ Tambala la deki ndani ya chumba cha mahabusu lilikuwa linafanya nini?

Kuna hatihati kukawa na kesi 2 za mauaji hapa, aliyefariki huenda ni mtu mwenye taarifa muhimu sana kwenye hili tukio la mauaji ya huyu Kijana mfanyabiashara wa madini!!!
 
Ebu tuambie unaona nini?kwamba tambala la deki haliwezi kuua?
Ebu tafuta tambala la deki ujaribu uje utupe mrejesho
 
Hizi tume ni kamba tu za kulia kwa urefu wake.
 
Alijinyongà vipi wakati wanawekwa selo moja? Au wao wanawekwa private? Mtu akiwa humo si vitu hatarishi vinatolewa? Semeni wamemnyonga wenzie, ili msituumize kichwa.
 
Wakuu: Sote tukiulizwa maelezo yetu ni hayo kama nilivyoaambia.
Wenzake: Ndio mkuu.
Yeye: Siwezi sema uongo mimi...
Wakuu: Unasemaa...? Staki kumuona huyu.
Wenzake: Ndio mkuu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…