Mtwara: Askari Polisi mmoja kati watuhumiwa wa mauaji ya mfanyabiashara alikutwa mahabusu akiwa amejinyonga tarehe 22 Jan 2022

Mtwara: Askari Polisi mmoja kati watuhumiwa wa mauaji ya mfanyabiashara alikutwa mahabusu akiwa amejinyonga tarehe 22 Jan 2022

Askari mmoja Kati ya wale 7 waliokuwa wakituhumiwa kufanya mauaji ya mfanyabiashara kijana ajinyonga

--
Afisa wa Jeshi la Polisi Mkoani Mtwara, Mrakibu Msaidizi wa Polisi, Greyson Mahembe ambaye ni miongoni mwa maafisa saba wa jeshi hilo waliofunguliwa mashtaka ya mauaji ya mfanyabiashara amejinyonga kwa tambala la kudekia akiwa mahabusu ya kituo cha polisi wilaya ya Mtwara.

Jeshi la Polisi Mkoani Mtwara liliwakamata na kuwafikisha mahakamani Maafisa wa Polisi saba kwa tuhuma za mauaji ya Mussa Hamisi Hamisi (25) mkazi wa Kijiji cha Ruponda wilayani Nachingwea Mkoani Lindi aliyekuwa akiwadai askari hao zaidi ya Sh milioni 33.7.

Kulingana na taarifa iliyotolewa na Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Mtwara, ACP Marck Njera ilisema mauaji hayo yalifanyika Januari 5, 2022 na mwili wa marehemu ulitupwa kitongoji cha Majengo kijiji cha Hiari Wilayani Mtwara.

Habari Leo

Kuhusu mauaji ya mfanyabiashara
, soma Mtwara: Maafisa Saba(7) wa Polisi wafikishwa Mahakamani kwa tuhuma za mauaji ya Kijana aliyekuwa akiwadai zaidi ya Tsh milioni 33.7 (Januari 25, 2022)

View attachment 2095972
Yaani Maabusu 7, wamefungiwa chumba Kimoja then mmoja akutwe amejinyonga, lipo jambo hapa, kwa ufahamu wangu mdogo ni kwamba mahabusu inakuwa na vyumba viwili yaani cha wanaume na wanawake ikiwa expanded zaidi kuna kuwa na mahabusu ya watoto wa kiume na watoto mahabusu wa kike, hakuna uwezekano wa mahabusu mmoja kukaa chumba chake peke yake, hii ina maana kuwa mahabusu inayedhaniwa amejinyonga hakuwa amehifadhiwa peke yake kwenye chumba, Maswali yangu;

i/ wakati anajinyonga hao wengine 6 walikuwa wapi?
ii/ Polisi wa zamu alikuwa wapi?
iii/ Tambala la deki ndani ya chumba cha mahabusu lilikuwa linafanya nini?

Kuna hatihati kukawa na kesi 2 za mauaji hapa, aliyefariki huenda ni mtu mwenye taarifa muhimu sana kwenye hili tukio la mauaji ya huyu Kijana mfanyabiashara wa madini!!!
 
Ebu tuambie unaona nini?kwamba tambala la deki haliwezi kuua?
Ebu tafuta tambala la deki ujaribu uje utupe mrejesho
Hivi tambaza la deki kweli tambaa la deki hebu fikiria tena tambaa la nini la deki

Sasa ukirudi kwenye kesi ya Zombe na wenzake kuna askari mmoja naye alijinyonga hivyo hivyo

Kuna kitu hapo kuna kitu huenda huyo jamaa ndio anajua siri zote

Bila ya kuwekwa tume huru ya uchunguzi kama ile ya Zombe kuna mtu ataangushiwa Zigo la dhambi hapo
 
Hivi tambaza la deki kweli tambaa la deki hebu fikiria tena tambaa la nini la deki

Sasa ukirudi kwenye kesi ya Zombe na wenzake kuna askari mmoja naye alijinyonga hivyo hivyo

Kuna kitu hapo kuna kitu huenda huyo jamaa ndio anajua siri zote

Bila ya kuwekwa tume huru ya uchunguzi kama ile ya Zombe kuna mtu ataangushiwa Zigo la dhambi hapo
Hizi tume ni kamba tu za kulia kwa urefu wake.
 
Alijinyongà vipi wakati wanawekwa selo moja? Au wao wanawekwa private? Mtu akiwa humo si vitu hatarishi vinatolewa? Semeni wamemnyonga wenzie, ili msituumize kichwa.
 
Wakuu: Sote tukiulizwa maelezo yetu ni hayo kama nilivyoaambia.
Wenzake: Ndio mkuu.
Yeye: Siwezi sema uongo mimi...
Wakuu: Unasemaa...? Staki kumuona huyu.
Wenzake: Ndio mkuu
 
Back
Top Bottom