Mtwara: Askari Polisi mmoja kati watuhumiwa wa mauaji ya mfanyabiashara alikutwa mahabusu akiwa amejinyonga tarehe 22 Jan 2022

Mtwara: Askari Polisi mmoja kati watuhumiwa wa mauaji ya mfanyabiashara alikutwa mahabusu akiwa amejinyonga tarehe 22 Jan 2022

Mimi nilikaa MAHABUSU pale madale.ndani Kuna choo mnawekewa na maji .
Pia tambala lipo kwa ajili ya kufutia maji
Uenda hiyo MAHABUSU Ina choo Cha ndani.
Ila Mimi ninachojua polisi kafa.
Tambala la kudekia lina nguvu gani ya kumbeba mtu mzima akajinyonga atleast wangesema ametumia suruali inaleta sense
 
Kwani Mshahara wa Mrakibu ni kiasi gani?Mbona tamaa zinawaua hawa?

Btw;Dead men tell no tales!
 
Askari mmoja Kati ya wale 7 waliokuwa wakituhumiwa kufanya mauaji ya mfanyabiashara kijana ajinyonga

--
Afisa wa Jeshi la Polisi Mkoani Mtwara, Mrakibu Msaidizi wa Polisi, Greyson Mahembe ambaye ni miongoni mwa maafisa saba wa jeshi hilo waliofunguliwa mashtaka ya mauaji ya mfanyabiashara amejinyonga kwa tambala la kudekia akiwa mahabusu ya kituo cha polisi wilaya ya Mtwara.

Jeshi la Polisi Mkoani Mtwara liliwakamata na kuwafikisha mahakamani Maafisa wa Polisi saba kwa tuhuma za mauaji ya Mussa Hamisi Hamisi (25) mkazi wa Kijiji cha Ruponda wilayani Nachingwea Mkoani Lindi aliyekuwa akiwadai askari hao zaidi ya Sh milioni 33.7.

Kulingana na taarifa iliyotolewa na Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Mtwara, ACP Marck Njera ilisema mauaji hayo yalifanyika Januari 5, 2022 na mwili wa marehemu ulitupwa kitongoji cha Majengo kijiji cha Hiari Wilayani Mtwara.

Habari Leo

Kuhusu mauaji ya mfanyabiashara
, soma Mtwara: Maafisa Saba(7) wa Polisi wafikishwa Mahakamani kwa tuhuma za mauaji ya Kijana aliyekuwa akiwadai zaidi ya Tsh milioni 33.7 (Januari 25, 2022)


View attachment 2095972
Kesi ya kina zombe ilikuwa hivi hivi aliyepiga risasi alitoroka na askari mmojawapo aliyekuwa shahidi muhimu nae akifariki.yetu macho na masikio.
 
Mimi nilikaa MAHABUSU pale madale.ndani Kuna choo mnawekewa na maji .
Pia tambala lipo kwa ajili ya kufutia maji
Uenda hiyo MAHABUSU Ina choo Cha ndani.
Ila Mimi ninachojua polisi kafa.
Ulikuwa peke yako au mlikuwa wengi
 
Nadhani ni vyema wizara ya mambo ya ndani kuangalia maslahi ya polisi..ikiwemi mishara na marupu rupu mengine ili wasishawishike kudhulumu wananchi hela zao
Njaa nayo ni mbaya wandugu
 
Hicho kifo kichunguzwe. Usikute alitaka kumwaga siri za wakubwa kwenye hiyo kesi wakaona wamuwahi. Hilo tambala la deki kalitoa wapi?
 
Duh jeshi la polisi kama jeshi la polisi. Wanaweza kukuletea ushahidi wa kesi na kuupoteza wenyewe
 
Back
Top Bottom