Mtwara: Jinsi Askari Polisi akiwemo Mkuu wa Kituo na Upelelezi walivyoshiriki Mauaji ya Mfanyabiashara wa Madini

Hakuna binaadam mwenye akili timamu anayesubiri kukatazwa kuua ndipo aone kama ni jambo baya.

By the way wapo wenzako wameielewa dini kukuzidi wanaua sababu ya dini hiyo hiyo na mafundisho yake,unazungumzaje kuhusu hilo!!!
Wewe unaongelea binadamu kama mtu mzima kukatazwa wakati mimi naongelea mtoto mdogo mpaka nimekupa na mfano wa samaki mkunje ...
Mkuu mimi sio mbishani na sipo hapa kubishana bali nachangia mada tu
Hao unaosema wanaelewa dini kunizidi na wanauwa kwa ajili ya dini sio kweli kwa sababu mimi sijaona mahali naambiwa muuwe mwenzio hata siku moja
Naomba niishie hapa na tuendelee kuchangia mada kama wengine please
Asante kwa maelezo yako
 
Msingi wa kesi upo kwenye Kifo cha Grayson,Lakini anatakiwa ahojiwe Kalanje na Onyango waseme nao ilikuwaje na Hamisi yuko wapi maana kama kupotea amepotea mikononi mwao.

Lakini kesi Iko chini ya PM hii hawawezi kuchomoka kirahisi hapo
 
Dk kwenye mipango akikwepo na ndo akiyetoa mbinu ya kuua,kumbuka hata sindano ya kumwua alitoa yeye
Yeye alikataa kumchoma sindano ya Sumu badala yale alishauri achomwe sindano ya usingizi baadae akiamka ataeleza yote. Lkn kwa bahati mbaya wale askari walimua kwa kumziba na tambala puani na mdomoni. Kwa maelezo hayo huyo Dr ndio sasa anakuwa mtu muhimu sana na yy ndio alitoa maelezo namna gani yule kijana aliuawa, wakati yule askari marehemu yy ndio alienda kuonesha wapi walipoutupa mwili wa Kijana yule. Nasubiri kujua Rafiki yangu Salimu amehusikaje ili nijue kama atasalimika au atatoka.
 
WATU WAKIJUWA UNA MPUNGA especially baadhi ya police lazima
Watakuja kufanya mpango wa kukunyanganya,kukupora utabambikiwa hata kesi

Ova
 
Mawasiliano ya Tume huru nayapataje? Au mpaka waziri aiunde ndiyo ifanye kazi.
 
Hiyo kesi hawatoboi, kama ingekuwa aliyeua ndio ndio aliyefariki basi ingekuwa rahisi kwao kutoboa. Lkn aliyeua ndio mtuhumiwa namba 1 sasa wanatokaje? Afu haki sio kushinda kesi, bali waliofanyiwa tukio wapate haki yao.
Kama ningekuwa Rais ningebalisha sheria mbalimbali sana.
 
Wewe hujaelewa soma tena, wapi walisema ameuawa kwa kuchomwa sindano ya sumu? Wamesema walishauri achomwe sindano ya sumu Dr akakataa akashauri achomwe ya Usingizi ili akiamka ahojiwe vyema, ndio walipoamua kumzima na tambala. Hizo habari umesoma wapi?
 
Nadhani ulianza kufuatilia suala hili baada ya kuanza kesi, pengine huna story ya moja kwa moja kabla ya kesi kwenda mahakamani.

Nasema hivi kutokana na story yako kwa DC Lema. Kwamba alionewa kukamatwa, wakati yeye alijisalimisha mwenyewe.

Ni kwamba, Lema ndiye aliyeendesha gari iliyopeleka miili ya waliuawa kwenye chumba cha kuhofadhia maiti, Muhimbili.

Lema ndiye aliyetoa ushahidi mzito uliofanya ACP Zombe aingizwe kwenye kesi na kuwa mshitakiwa namba moja.

Ilikuwa hivi,
Tukio lilitokea wakati Zombe akikaimu nafasi Kanda Maalum, wakati ambao Tibaigana alikuwa likizo. Yakatokea ya kutokea.

Zombe akaibuka na press akisema marehemu walikuwa majambazi. Na kwa wakati huo CPL Saad Alawi na DC Rashid Lema walishatoroka.

Saad aliwafyatulia risasi na Lema alipeleka miili Muhimbili. Baada ya kelele nyingi, Rais Jakaya Kikwete akaunda tume.

Tume iliongozwa na Jaji Ramadhan Kipenka, na ikatangaza kwa umma mwenye ushahidi aende nao. Hadi wakati huo Zombe yuko uraiani.

Lema alienda kwao Arusha, na huko akasimulia wazazi wake. Kutokana na uchamungu wa wazazi wakagoma kumwelewa.

Wakamshinikiza akatoe ushahidi kwa tume ya Kipenka. Ndipo hapo kila kitu kwenye kesi kikabadilika, alinyoosha kama huyo daktari wa Mtwara.

Na msingi wa kesi uliundwa zaidi kwa ushahidi wa Lema, kama ya Mtwara ilivyoundwa kwa ushahidi wa daktari.

Hadi suala la Msitu wa Pande ni Lema alileta. Ndiyo maana Lema alikuwa shahidi muhimu katika ile kesi na kifo chake kilitoa ahueni ya kesi.

Saad na Lema ndiyo waliokwenda kufyatua risasi hewani kwenye misitu ya Bunju ili kuunda ushahidi hewa wa kuwa wajibizana kwa risasi na marehemu.

Tume ya Kipenka ilipokea ushahidi hadi wa wezi halisi waliofanya tukio la ujambazi ambalo Zombe alisema kwenye press kuwa lilifanywa na marehemu.

Kwa hiyo;
Haya maelezo yaliyotolewa na daktari yanabaki kama msingi wa kesi huku daktari akiwa ndiye shahidi muhimu kama Lema.

Sasa tuifuatilie hii kesi hadi mwisho, na tuwe na kalamu na karatasi ya kunakili maswali ya Magafu kwa hao mashahidi ili tusichanganyikiwe na hukumu.

Ila naendelea kushauri, Magafu yuko hapo. Tusibet.

Ova
 
Ukisoma vizuri maelezo ya Dr, hakuwa anajua kuwa mtuhumiwa ni nani, na askari wana mpango gani nae, wameingia ndani yeye alichokuwa anajua ni kwenda kumchoma sindano ya usingizi na sio kuua, iyo inamuondoa hatiani
Ndo umtibu mgonjwa kwnye gari?? Kwann asipelekwe hospitali akamchome hiyo sindano??

Sent from my Infinix X683 using JamiiForums mobile app
 
Zombe alichomoka
Zombe alikuwa mshz tu

Ova
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…