green rajab
JF-Expert Member
- Oct 16, 2015
- 12,387
- 39,119
Ma polisi ma mbwa sana ndio maana magu kayakomoa na kikokoto
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Ma polisi ma mbwa sana ndio maana magu kayakomoa na kikokoto
Wewe unaongelea binadamu kama mtu mzima kukatazwa wakati mimi naongelea mtoto mdogo mpaka nimekupa na mfano wa samaki mkunje ...Hakuna binaadam mwenye akili timamu anayesubiri kukatazwa kuua ndipo aone kama ni jambo baya.
By the way wapo wenzako wameielewa dini kukuzidi wanaua sababu ya dini hiyo hiyo na mafundisho yake,unazungumzaje kuhusu hilo!!!
Harafu huyo greyson alikufaje?
Pesa ilikuwa Mil 70 mkuu sio ndogo hiyo.Watu wengi pesa ndogo
Yeye alikataa kumchoma sindano ya Sumu badala yale alishauri achomwe sindano ya usingizi baadae akiamka ataeleza yote. Lkn kwa bahati mbaya wale askari walimua kwa kumziba na tambala puani na mdomoni. Kwa maelezo hayo huyo Dr ndio sasa anakuwa mtu muhimu sana na yy ndio alitoa maelezo namna gani yule kijana aliuawa, wakati yule askari marehemu yy ndio alienda kuonesha wapi walipoutupa mwili wa Kijana yule. Nasubiri kujua Rafiki yangu Salimu amehusikaje ili nijue kama atasalimika au atatoka.Dk kwenye mipango akikwepo na ndo akiyetoa mbinu ya kuua,kumbuka hata sindano ya kumwua alitoa yeye
Mawasiliano ya Tume huru nayapataje? Au mpaka waziri aiunde ndiyo ifanye kazi.Upo sahihi na hiyo Tume huru iwepo kila mkoa maana unaona kabisa pana wahuni wapo busy kuua Raia kwa kutumia Kodi za Wananchi inaumiza sana ujue watu wanapambana kupata pesa wakipata harafu wanakuja wahuni kuua ili watoke na hizo hela huku Wabunge wakiwa kimya kuangalia maslahi yao tu huko Bungeni...
Hiyo kesi hawatoboi, kama ingekuwa aliyeua ndio ndio aliyefariki basi ingekuwa rahisi kwao kutoboa. Lkn aliyeua ndio mtuhumiwa namba 1 sasa wanatokaje? Afu haki sio kushinda kesi, bali waliofanyiwa tukio wapate haki yao.Unaikumbuka kesi ya kuuawa kwa wafanyabishara wa madini ya 2006 ya ACP Abdallah Zombe na wenzake kumi na moja?
Ni kweli kwamba Ephraim Sabinus Chigumbi, Sabinus Chigumbi, Juma Ndugu (dereva tax) na Mathias Lunkombe waliuawa wakiwa mikononi mwa polisi.
Magafu alikuwa ndiyo aliyesimama pale kati. Na unajua nini kilitokea baada CPL Saad Alawi kutoweka kabla ya kukamatwa?
Unajua kilichotokea baada ya DC Rashid Lema kuugua ghafla akiwa mahabusu, siku moja kabla ya kutoa ushahidi wake mahakamani, na baadaye kufariki?
Nikukumbushe, Zombe na wenzake waliachiwa huru. Baadaye Bageni pekee alinaswa kwenye rufaa.
Na huko Mtwara tayari mtuhumiwa moja ameshafariki kwa kujinyonga. Ukiona Magafu yuko kwenye kesi anazoziweza zaidi, usibet.
Ova
Wewe hujaelewa soma tena, wapi walisema ameuawa kwa kuchomwa sindano ya sumu? Wamesema walishauri achomwe sindano ya sumu Dr akakataa akashauri achomwe ya Usingizi ili akiamka ahojiwe vyema, ndio walipoamua kumzima na tambala. Hizo habari umesoma wapi?Changamoto ni kwamba, kisheria, hao watuhumiwa kwa sasa ni sawa na wewe uliye uraiani yaani hawana hatia kwa sasa.
Zaidi sana sheria za jinai hutafsiriwa katika kumlinda mtuhumiwa dhidi ya uonevu wa Serikali, yaani serikali inatakiwa ithibitishe pasina shaka kwamba waliua kweli.
Mfano, ukirudia kuisoma hii habari kuna maelezo kwamba marehemu alichomwa "sindano ya sumu" mengine marehemu "alichomwa "sindano ya usingizi na pia marehemu "alifungwa na kuzibwa pua na mdomo" .
Sasa kama ndivyo ilivyo kisheria, na kwa kuwa shahidi wa kwanza ndiye kayasema haya mahakamani, na kwa kuwa shaidi namba moja ndiye mbeba kesi, na ikiwa Jaji atazingatia haya maelezo, basi tayari chanzo cha kifo cha marehemu kina utata na hapo huenda watuhumiwa wakakutwa na kosa dogo ama wakaachiwa huru.
Nadhani ulianza kufuatilia suala hili baada ya kuanza kesi, pengine huna story ya moja kwa moja kabla ya kesi kwenda mahakamani.Sijajua kama ulikuwa unaniuliza unataka nikujibu au unatoa ufafanuzi [emoji1745]
Wafanyabiashara wa Madini na yule Dreva Tax wote waliuawa kwa kupigwa Risasi tena za SMG,Askari wote 11 waliokuwepo kwenye tukio lile ilionekana siku ya tukio ni Silaha moja tu SMG ya Koplo Saad Ally ndio ilitumika(actually namfahamu sana maana tulikuwa nae pale Oysterbay).
Maana unapoingia kazini kama unabeba SMG maana yake unapewa na Risasi zake 30 kwenye Magazine,na kama unabeba Bastola(Chinese Pistol)maana yake unahesabiwa na Risasi zake 8. Wale Askari walipomaliza zamu na kurudisha Silaha na Risasi,Askari wote walirudisha Silaha na Risasi zikiwa sawa isipokuwa Koplo Saad tu ndie ambaye alirudisha Risasi pungufu hivyo aliandika maelekezo kwa nini amerudisha Risasi pungufu na pia kwenye Armoury Register(Kitabu cha Makabidhiano ya Silaha na Risasi)taarifa hiyo iliandikwa(Mahakamani Kitabu kile kilikuwa sehemu ya vielelezo upande wa Mashtaka). Ndio maana Jaji aliwaachia Huru watuhumiwa wote na akawaambia upande wa Mashtaka wamlete Koplo Saad maana hakuwahi kukamatwa mpaka leo na ndie ambaye Silaha yake ilitumika.
Upande wa Mashtaka ulipokuja kukata Rufaa ndio Mkuu wa Upelelezi wa Wilaya(OC CID Christopher Bageni)akaangukiwa na jumba bovu akahukumiwa Kunyongwa. Na hata alipokata Rufaa bado Majaji wakatupilia mbali Rufaa yake hivyo yupo Jela mpaka leo.
Sababu ya Bageni kukutwa na Hatia na Majaji wa Mahakama ya Rufaa ni kwa kwamba yeye ndie alikuwa Incharge wa Upelelezi Wilaya hivyo mtiririko mzima wa tukio hilo alikuwa anaujua hivyo alikuwa na uwezo wa kuzuia Mauaji yale lakini hakufanya hivyo maana mpaka Mabwepande alienda na kile Kikosi kukamilisha Mauaji. Zombe kama Mkuu wa Upelelezi wa Mkoa alikuwa anapewa taarifa tu na Bageni na hakuwepo eneo la Mauaji.
Hivyo kitendo cha Mhusika Mkuu aliyefyatua trigger kuua wale jamaa wanne kutokuwepo Mahakamani ndio ikawa pona ya wengine.
Kuhusu kifo cha Rashid Lema akiwa Mahabusu ni kwamba yeye aliona kama kukamatwa alionewa maana hakuhusika,hivyo kwenye ile Tume iliyoundwa alinyoosha Maelezo A to Z kama alivyonyoosha huyu Daktari na yule A/Inspekta aliyefia Mahabusu. Hivyo kwa vyovyote mnavyokuwa na tatizo watu watano kwa mfano,ni lazima mkae mpangane nini cha kuongea,lakini inapotokea mwenzenu anakuwa tofauti na nyie maana yake anataka kuwachoma,hivyo mwisho wa siku lazima nae mumpoteze tu.
Ninategemea kwenye Kesi hii huyo Daktari atanyoosha maelezo A to Z maana haya ushahidi wa huyo ACP Mgonja umeegemea kwenye maelezo waliyoyapata kutoka kwa huyo Daktari na yule Askari aliyefia Mahabusu.
Kesi hii labda hao Watuhumiwa wote wakane kuhusika akiwemo huyo Daktari akane maelezo ambayo huyo Shahidi ACP Mgonja anadai aliambiwa na Daktari. Kisha wote wamuangushie jumba bovu Marehemu Askari aliyefia Mahabusu kwamba ndie aliyeua. Lakini hapohapo huyu Gilbert ndie alikuwa na Cheo kikubwa kuliko wote,swali ni kwa nini alishindwa kuzuia Mauaji hayo kama Incharge??
Anyway,Kesi ni nzuri,tusubiri tuone
Ndo umtibu mgonjwa kwnye gari?? Kwann asipelekwe hospitali akamchome hiyo sindano??Ukisoma vizuri maelezo ya Dr, hakuwa anajua kuwa mtuhumiwa ni nani, na askari wana mpango gani nae, wameingia ndani yeye alichokuwa anajua ni kwenda kumchoma sindano ya usingizi na sio kuua, iyo inamuondoa hatiani
Zombe alichomokaNadhani ulianza kufuatilia suala hili baada ya kuanza kesi, pengine huna story ya moja kwa moja kabla ya kesi kwenda mahakamani.
Nasema hivi kutokana na story yako kwa DC Lema. Kwamba alionewa kukamatwa, wakati yeye alijisalimisha mwenyewe.
Ni kwamba, Lema ndiye aliyeendesha gari iliyopeleka miili ya waliuawa kwenye chumba cha kuhofadhia maiti, Muhimbili.
Lema ndiye aliyetoa ushahidi mzito uliofanya ACP Zombe aingizwe kwenye kesi na kuwa mshitakiwa namba moja.
Ilikuwa hivi,
Tukio lilitokea wakati Zombe akikaimu nafasi Kanda Maalum, wakati ambao Tibaigana alikuwa likizo. Yakatokea ya kutokea.
Zombe akaibuka na press akisema marehemu walikuwa majambazi. Na kwa wakati huo CPL Saad Alawi na DC Rashid Lema walishatoroka.
Saad aliwafyatulia risasi na Lema alipeleka miili Muhimbili. Baada ya kelele nyingi, Rais Jakaya Kikwete akaunda tume.
Tume iliongozwa na Jaji Ramadhan Kipenka, na ikatangaza kwa umma mwenye ushahidi aende nao. Hadi wakati huo Zombe yuko uraiani.
Lema alienda kwao Arusha, na huko akasimulia wazazi wake. Kutokana na uchamungu wa wazazi wakagoma kumwelewa.
Wakamshinikiza akatoe ushahidi kwa tume ya Kipenka. Ndipo hapo kila kitu kwenye kesi kikabadilika, alinyoosha kama huyo daktari wa Mtwara.
Na msingi wa kesi uliundwa zaidi kwa ushahidi wa Lema, kama ya Mtwara ilivyoundwa kwa ushahidi wa daktari.
Hadi suala la Msitu wa Pande ni Lema alileta. Ndiyo maana Lema alikuwa shahidi muhimu katika ile kesi na kifo chake kilitoa ahueni ya kesi.
Saad na Lema ndiyo waliokwenda kufyatua risasi hewani kwenye misitu ya Bunju ili kuunda ushahidi hewa wa kuwa wajibizana kwa risasi na marehemu.
Tume ya Kipenka ilipokea ushahidi hadi wa wezi halisi waliofanya tukio la ujambazi ambalo Zombe alisema kwenye press kuwa lilifanywa na marehemu.
Kwa hiyo;
Haya maelezo yaliyotolewa na daktari yanabaki kama msingi wa kesi huku daktari akiwa ndiye shahidi muhimu kama Lema.
Sasa tuifuatilie hii kesi hadi mwisho, na tuwe na kalamu na karatasi ya kunakili maswali ya Magafu kwa hao mashahidi ili tusichanganyikiwe na hukumu.
Ila naendelea kushauri, Magafu yuko hapo. Tusibet.
Ova
Unaua kwa ngapi?Sasa milioni 60 ni hela ya kufanya ue watu kweli?
Nadhani mpaka ipitishwe Bungeni sasa hivi walipita kuchukua maoni tuu na kazi walimaliza wakakabidhi taarifa kwa Mh Rais...Mawasiliano ya Tume huru nayapataje? Au mpaka waziri aiunde ndiyo ifanye kazi.
Killer cops.Hatari sana