Mtwara: Jinsi Askari Polisi akiwemo Mkuu wa Kituo na Upelelezi walivyoshiriki Mauaji ya Mfanyabiashara wa Madini

Mtwara: Jinsi Askari Polisi akiwemo Mkuu wa Kituo na Upelelezi walivyoshiriki Mauaji ya Mfanyabiashara wa Madini

Siku zote nasemaga wabongo ni makatili sana,huyo anayesemaga
Kuna amani ni muongo
Narudia kusena,kama unavipesa
Hakikisha hawa jamaa wasijuwe
Maana kuna kundi maalum wao kazi yao kuwatisha watu na kuwatemesha pesa...

Ova
Harafu hilo kundi linataka hela nyingi balaa sio chenji na ndio maana wanaoshindana nao lazima wakutwe mtaroni...
 
Huyu Tajiri Mussa Hamisi Hamisi atakuw amtu mzito na mtu wa chama.

Sio rahisi kesi yake kusimama hivi. Kama tulivyozoea.

Vinginevyo tunawapongeza Jeshi la Polisi na Serikaki kusimamia haki.
Hapa ndipo sasa tatizo linapoanzia. Unawapongeza wanaosababisha matatizo. Mpaka siku tukijua mzizi wa tatizo ni nini, ndiyo haya mauaji yatapungua.
 
Siku zote nasemaga wabongo ni makatili sana,huyo anayesemaga
Kuna amani ni muongo
Narudia kusena,kama unavipesa
Hakikisha hawa jamaa wasijuwe
Maana kuna kundi maalum wao kazi yao kuwatisha watu na kuwatemesha pesa...

Ova
Huyo dr wa polisi Msuya anajaribu kujitoa kwenye kundi la mauaji kiaina baada ya kuona limevunda. Inakuwaje umchome mtu sindano ya usingizi ili eti akiamka ndiyo aseme kila kitu. Alijua kabisa marehemu atafanywa nini baada ya kuchomwa sindano.
 
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kipolisi Ilala, Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP), Yustino John Mgonja ameieleza Mahakama Kuu Kanda ya Mtwara namna mfanyabiashara wa madini, Mussa Hamis Hamis, alivyouawa.

Pia, amewataja washtakiwa waliokuwepo eneo la tukio na yule anayedaiwa kutekeleza mauaji hayo ya mfanyabiashara huyo aliyekuwa mkazi wa Nachingwea mkoani Lindi.

ACP Mgonja alitoa maelezo hayo jana wakati akitoa ushahidi katika kesi hiyo ya mauaji inayowakabili maofisa saba wa Jeshi la Polisi mkoani Mtwara. Yeye ni shahidi wa tatu wa upande wa mashtaka kati ya mashahidi 72 wanaotarajiwa kuitwa na upande wa mashtaka katika kesi hiyo.

Washtakiwa katika kesi hiyo ya jinai namba 15 ya mwaka 2023 ni pamoja na aliyekuwa Mkuu wa Upelelezi wa Wilaya ya Mtwara, Gilbert Sostenes Kalanje na Mkuu wa Kituo cha Polisi Mtwara, Charles Onyango.

Wengine ni aliyekuwa Ofisa Intelijensia ya Jinai Mkoa wa Mtwara, Nicholaus Kisinza, Marco Mbuta, Mkaguzi wa Polisi, John Msuya, aliyekuwa mganga mkuu wa Zahanati ya Polisi Mtwara, Shirazi Mkupa na Koplo Salim Mbalu.

Maofisa hao wa Polisi wanakabiliwa na shtaka moja la mauaji wakidaiwa kumuua kwa makusudi Mussa waliyemchoma sindano ya sumu katika kituo cha Polisi Mitengo Wilaya ya Mtwara, Mkoa wa Mtwara, Januari 5, 2022.

Hata hivyo, wakati polisi hao wakiwa mahabusu kabla ya kupandishwa kizimbani, mtuhumiwa mwenzao, Grayson Mahembe alidaiwa kujinyonga hadi kufa Januari 22, 2022 akiwa mahabusu.

Kesi hiyo inasikilizwa na Jaji Edwin Kakolaki kutoka Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam.

Katika ushahidi wake akiongozwa na mwendesha mashtaka, Wakili wa Serikali Mkuu, Pascal Marungu aliieleza mahakama kuwa Mussa aliuawa na SP Kalanje Kwa kumziba kwa tambala mdomoni na puani, muda mfupi baada ya Dk Msuya (mshtakiwa wa Tano) kumdunga sindano ya usingizi.

Shahidi huyo aliieleza Mahakama kuwa alipata taarifa za tukio hilo baada ya kuwahoji baadhi ya askari waliokuwa zamu katika kituo cha Polisi Mitengo, pamoja na Dk Msuya mwenyewe na ofisa wa polisi, Grayson (marehemu kwa sasa) ambao walisimulia tukio hilo.

Kwa mujibu wa shahidi huyo, siku ya tukio Januari 5, 2022, mshtakiwa wa kwanza, SP Kalanje alimpigia simu Dk Msuya akamtaka waonane na Dk Msuya ambaye al8ikaribisha ofisini kwake katika zahanati ya Polisi na wakazungumza.

Alidai kuwa SP Kalanje alimueleza Dk Msuya kuwa wana mtuhumiwa wao wa wizi wa pikipiki ambaye amekuwa akifanya matukio ya wizi huo maeneo mbali katika mikoa ya Mtwara, Lindi na Dar es Salaam na amekuwa akiwasumbua hivyo wanataka wammalize.

Hivyo alidai kuwa SP Kalanje alimuuliza Dk Msuya kama anaweza kufanya namna ya kupata sindao ya sumu ili wamdunge, lakini Dk Msuya alimjibu kuwa tangu aajiriwe na kuapa kuwa daktari hajawahi kumdunga mtu sindano ya sumu.

Shahidi huyo amedai kuwa badala yake. Dk Msuya alimshauri SP Kalanje wamdunge sindano ya usingi , akizinduka ataanza kueleza matukio yote ya wizi aliyoyafanya, ushauri ambao Kalanje alikubaliana nao.

Kwa mujibu wa shahidi huyo, licha ya SP Kalanje kutaka waende kutekeleza mpango huo wakati huohuo, lakini Dk Msuya alimueleza kuwa wakati huo bado alikuwa na wagonjwa wengine akiwahudumua na akashauri wafanye baadaye.

Saa 8:30 mchana, Kalanje alifika ofisini kwa Dk Msuya kwa ajili ya kutekeleza mpango huo kama walivyokuwa wamekubaliana, hivyo alimuuliza kama alikuwa tayari akamjibu kuwa alikuwa tayari.

Lakini Dk Msuya alimuuliza SP Kalanje mahali alikokuwa huyo mtuhumiwa wao, akamjibu kuwa alikuwa katika kituo cha Polisi Mitengo.

Kwa mujibu wa shahidi huyo, Dk Msuya alisema yeye anaelewa kituo cha Mitengo kina wahalifu sugu hivyo akajua na huyo amehifadhiwa kwa wahalifu sugu, akakubali akaingia kwenye gari na akakaa kiti cha mbele huku gari likiendeshwa na SP Kalanje.

Wakati gari inaondoka pale zahanati, Dk Msuya alihisi kama viti vya nyuma vina watu.

Hivyo aligeuka kutazama akawatambua watu wawili, ambao ni ASP Onyango na A/Insp Grayson waliokuwa wamekaa viti vya pembeni kulia na kushoto na katikati kulikuwa na mtu mwingine ambaye hakuweza kumtambua.

Waliendelea na safari hadi kituo cha Polisi Mitengo na SP Kalanje alishuka akaenda kuzungumza na mkuu wa kituo hicho, Paulo Kiula.

Dk Msuya na askari wale wawili pamoja na yule mtu ambaye hakumtambua nao walishuka wakamfuata SP Kalanje na mkuu wa kituo walipokuwa wanaelekea ndani ya jengo la kituo hicho.

Dk Msuya alimuomba OCS Kiula amuonyeshe Kalanje ofisi moja ambayo aliingia Kalanje, Onyango, Grayson na yule kijana na yeye akabaki nje.

Lakini baada ya dakika tatu hivi, naye alingia ndani ya hiyo ofisi na alimkuta yule kijana amevuliwa shati yuko kifua wazi na mikono yake ikiwa imefungwa kwa kamba kwa nyuma akiwa amelala kwenye sakafu huku akilia.

SP Kalanje alimwambia Dk Msuya amdunge sindano ya usingizi mkono wa kulia yule kijana.

Na baadaye kidogo, Dk Msuya anasema alimsikia Kalanje akisema huyo anawachelewesha, akachukua tambala akamziba yule kijana pua na mdomo.

Anasema baada ya Dk Msuya kuona vile aliamua kutoka nje akawaacha Karanje na wale wenzake na yule kijana akiwa amelala chini.

Lakini baada ya muda mfupi, Kalanje alimuita Dk Msuya akamuuliza, "tayari?" huku akimuonyesha yule kijana pale chini.

Dk Msuya alimuangalia kama hapumui lakini hakumpima ila alielewa lile swali la SP Kalanje kwamba lilikuwa linamaanisha kama amekufa na yeye alijibu kuwa tayari.

Hivyo wote walitoka mle chumbani na kumuacha yule kijana akiwa amelala pale chini.

SP Kalanje alikwenda kwa OCS akachukua kufuli likiwa na funguo akafunga mlango kisha wakaondoka wote akiwa na huo ufunguo, wakapanda gari na kuondoka.

Kamanda huyo wa polisi ambaye ni shahidi, aliieleza Mahakama kuwa baada ya maelezo hayo ya mdomo kutoka kwa Dk Msuya, alielekeza yaandikwe maelezo kama alivyosimulia na maelezo yake yawekwe kwenye jalada la uchunguzi.

“Wakati huo tulimchukulia Dk Msuya kama mtoa taarifa,” alidai Kamanda Mgonja.

Alidai wakati yote hayo yakifanyika, alijiuliza hayo mauaji ni ya huyo kijana Mussa ambaye ndugu zake walikuwa wanamtafuta au kuna mwingine?

"Hivyo nikaagiza atafutwe mjomba wa Mussa Hamis anayeitwa Salum Mombo aje ofini kwangu, alikuja nikamtaka anitafutie picha za Mussa kusudi ili niangalie yule mtu ambaye askari wanasema walimuona akiingia pale Mitengo ndiyo huyu kijana Mussa Hamis au ni mwingine,” alieleza.

Shahidi huyo alieleza kuwa mjomba huyo akiwa ofini kwake alipiga simu Nachingwea kwa baba wa kufikia wa Mussa akamtaka atafute picha zake azitume kwenye gari.

"Kesho yake Januari 22, 2022 zililetwa picha nikazitazama nikamkabidhi ASP Esau ili waendelee na utaratibu wa upelelezi,” alieleza ACP Mgonja.

Alidai kulikuwa na mauaji Januari 21,2022 niliagiza apatikane Grayson ambaye alikuwa mahabusu Tandahimba, kwanza kati ya watu wote waliotajwa yeye alikuwa ametajwa maeneo mengi.

Alieleza kuwa baada ya Grayson kuletwa aliongeza timu ya wapelelezi akiwajumuisha askari watano wa timu ya Task Force waliokuwa wanashughulikia magaidi wakingozwa na SP Simba, hivyo ikawa timu ya wapelelezi 10 akiwemo yeye mwenyewe.

"Tulifikiri kwa pamoja tukakubaliana tumlete Dk Msuya ili asimulie mbele ya Grayson nini kiliendelea pale Mitengo kama alivyonisimulia mimi.”

"Kwa kuwa Msuya alishuhudia kila kitu kilichofanyika pale Mitengo na Grayson akiwepo, kwa hiyo sisi kama makachero tuliona Grayson akisikia, basi mahojiano yetu naye yatakuwa rahisi."

Shahidi huyo alihitimisha Kwa kueleza kuwa katika mahojiano ya mdomo waliyoyafanya na Dk Msuya mbele ya Grayson, alisimulia kama alivyokuwa amemsimulia yeye na walipomuuliza Grayson, alikubali kuwa alivyosimulia Dk Msuya ndivyo walivyofanya.

“Hivyo mimi kama RCO picha iliyoniijia kichwani ni kwamba, haya sasa ni mauaji na kama ni mauaji hakuna mauaji ambayo hayana mwili au mtu aliyeuawa, hivyo nikamtaka Grayson atuonyeshe huyo ambaye wamemuua yuko wapi."

Hata hivyo wakati shahidi huyo anataka kueleza kile Grayson alichosema, kiongozi wa jopo la mawakili wa utetezi, Majura Magafu aliweka pingamizi akisema kwa kuwa Grayson si mshtakiwa wala shahidi, hawezi kutoa maelezo yake kwa sababu hawatapata fursa ya kumhoji kuhusu ukweli wake.

Pingamizi hilo liliibua mvutano wa hoja na upande wa mashtaka na Jaji Kakolaki baada ya kusikiliza hoja za pande zote aliahirisha kesi hiyo Kwa ajili ya kuandika uamuzi wake.
Hatari sana Polisi wetu
 
Yaani nimesoma hiyo habari yaani nimesikitika sana aisee yaani watu wanatafuta chumba kwa ajili ya kumuua mtu harafu daktari anaambiwa angalia kama kafa au laa na daktari anathibitisha kuwa kafa daaah Nchi hii ina watu wakatili sana sijapata kuona sio wa kukaa na binadamu hao wanyama..
Ndugu yangu ni hivi: haya ni baadhi ya matukio machache sana yanayojulikana. Mengi yanaishia chini kwa chini. Tulitakiwa tuwe na tume huru ya kupokea na kuchunguza malalamiko kutoka kwa wananchi.
 
Hii kesi ngumu sana na Kuna watu wanaenda kula nyundo za kutosha mana ingekuwa ameuliwa mtu ambae Hana connection yoyote ingekuwa kesi ishazimwa na wangesema mtuhumiwa bwana hamis kajinyonga mwenyewe.!

Lakin hata kosa alilofanya mpaka wakamuuwa hawalisemi kafanya Nini.

Polisi wakitaka kukutia hatiani kwanza wanakupa jina baya kama hawakuita unatumiwa na magaidi basi watakupa hata kesi za bangi na unga !

Huyu mchizi alikuwa na Hela na alikuwa na ushamba flani hivi mana kapata Hela ukubwani alafu za haraka haraka sasa akawa anaruka majoka sana .Nasikia alikuwa anatoka na kibegi Cha Hela kwenda kula Bata ndio wale wajomba wakatonywa kuwa Kuna mchizi anatamba huko viwanja na kibegi Cha Hela

Tatizo likaanzia hapo.

Polisi wengi Huwa hawana roho za kibinadamu kabisa .wao wanaishi kama wanyama

Wanahisi wakishakutoa roho ni kama ndio wamemaliza maisha yako. Wasichokijua ni kuwa kufa sio mwisho WA maisha.!
 
Majura Magafu licha ya utaalamu wake lakini kama Ushahidi umenyooka huwa anagonga mwamba,nadhani alikuwepo kwenye kuwatetea wale waliomuua Bilionea Msuya na wote walihukumiwa KUNYONGWA japo kwenye Rufaa akachomoka mmoja huku Master mwenyewe aliyefadhili Pesa ili mpango ukamilike akibaki ndani mpaka leo kusubiria Hukumu licha ya utajili wake wote. Kwa hiyo kwa kifupi Kesi hii ni ngumu kwa ndugu yangu Gilbert Kalanje. Inafanana na ile Kesi ya Zombe lakini hii ni ngumu maana Mtekelezaji wa Mauaji ndie mshtakiwa wa kwanza(Gilbert Kalanje). Ile Kesi ya Zombe Mtekelezaji wa Mauaji ya wale Wafanyabiashara na Dreva Tax (Koplo Saad)hakuwahi kukamatwa mpaka leo ndio maana Jaji aliwaachia huru kina Zombe na akawaambia Upande wa Mashtaka wamlete Muuaji Mahakamani yaani Koplo Saad
Unaikumbuka kesi ya kuuawa kwa wafanyabishara wa madini ya 2006 ya ACP Abdallah Zombe na wenzake kumi na moja?

Ni kweli kwamba Ephraim Sabinus Chigumbi, Sabinus Chigumbi, Juma Ndugu (dereva tax) na Mathias Lunkombe waliuawa wakiwa mikononi mwa polisi.

Magafu alikuwa ndiyo aliyesimama pale kati. Na unajua nini kilitokea baada CPL Saad Alawi kutoweka kabla ya kukamatwa?

Unajua kilichotokea baada ya DC Rashid Lema kuugua ghafla akiwa mahabusu, siku moja kabla ya kutoa ushahidi wake mahakamani, na baadaye kufariki?

Nikukumbushe, Zombe na wenzake waliachiwa huru. Baadaye Bageni pekee alinaswa kwenye rufaa.

Na huko Mtwara tayari mtuhumiwa moja ameshafariki kwa kujinyonga. Ukiona Magafu yuko kwenye kesi anazoziweza zaidi, usibet.

Ova
 
Ndugu yangu ni hivi: haya ni baadhi ya matukio machache sana yanayojulikana. Mengi yanaishia chini kwa chini. Tulitakiwa tuwe na tume huru ya kupokea na kuchunguza malalamiko kutoka kwa wananchi.
Upo sahihi na hiyo Tume huru iwepo kila mkoa maana unaona kabisa pana wahuni wapo busy kuua Raia kwa kutumia Kodi za Wananchi inaumiza sana ujue watu wanapambana kupata pesa wakipata harafu wanakuja wahuni kuua ili watoke na hizo hela huku Wabunge wakiwa kimya kuangalia maslahi yao tu huko Bungeni...
 
Ile taarifa ya mauaji ya yule kijana iliniumiza sana mtu unapambana hustle zako zinajibu shimo linatema wanakuja watu na njaa zao wanakubambikizia kesi wachukue pesa zako wanaona haitoshi wanaamua kufanya ukatili wa mauaji..
Inaumiza sana
 
Hapana.

Kutoa hoja kwamba 'Jeshi la Polisi' lifumuliwe halafu liundwe 'Jeshi' jipya siyo suluhu, kwa sababu, ninadhani tatizo linaanza kwenye jina "Jeshi".

Kimsingi ukishaita taasisi "Jeshi" maana yake ni taasisi ya mapambano ya kivita.

Sasa swali ni je, hii taasisi yenye jina la kijeshi linapambana na wananchi au linatoa huduma kwa wananchi?

Jibu ni kwamba tunahitaji Huduma za Kipolisi (Police Services) na siyo Jeshi la Polisi (Police Army).

Tatizo lilianzia kwa mkoloni ambaye aliunda Jeshi la Polisi kwa lengo la kuwanyamazisha wazalendo waliokuwa kinyume na wakoloni, na Jeshi hilo likarithiwa na Serikali, na hatimaye kazi zake zikabadilika kidogo na kuwa Jeshi la kupambana na raia badala ya kutoa huduma kwa raia ambalo ndilo lengo la Serikali.
Jina siyo tatizo per se. Tatizo ni CCM. CCM inawatumia polisi kukandamiza wananchi ili iendelee kutawala. In turn lazima iwaachie wafanye watakavyo ili isiwaudhi. Polisi inayotumiwa na serikali kufanya maovu ni lazima nayo ifanye uhuni kwani inajua kabisa watawale ni wahuni.
 
Taasisi nyingi za serikali wanakwambia ‘system’ haifanyi kazi mtandao uko chini unadhani police watashindwa kuzima hizo camera ili wafanye yao? Na hawashindwi kukata umeme kabisa ili watimize yao.
Ninafanya kazi ya kukusanya mapato kwa kutumia mashine za serikali.

Hili suala la system kutokufanya kazi ni la kweli na huwa linatokea.

Sitetei wala kukataa kwamba kuna wanaodanganya, ila binafsi huwa linanitokea katika majukumu yangu ya kazi.
 
Back
Top Bottom