Mtwara: Jinsi Askari Polisi akiwemo Mkuu wa Kituo na Upelelezi walivyoshiriki Mauaji ya Mfanyabiashara wa Madini

Mtwara: Jinsi Askari Polisi akiwemo Mkuu wa Kituo na Upelelezi walivyoshiriki Mauaji ya Mfanyabiashara wa Madini

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kipolisi Ilala, Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP), Yustino John Mgonja ameieleza Mahakama Kuu Kanda ya Mtwara namna mfanyabiashara wa madini, Mussa Hamis Hamis, alivyouawa.

Pia, amewataja washtakiwa waliokuwepo eneo la tukio na yule anayedaiwa kutekeleza mauaji hayo ya mfanyabiashara huyo aliyekuwa mkazi wa Nachingwea mkoani Lindi.

ACP Mgonja alitoa maelezo hayo jana wakati akitoa ushahidi katika kesi hiyo ya mauaji inayowakabili maofisa saba wa Jeshi la Polisi mkoani Mtwara. Yeye ni shahidi wa tatu wa upande wa mashtaka kati ya mashahidi 72 wanaotarajiwa kuitwa na upande wa mashtaka katika kesi hiyo.

Washtakiwa katika kesi hiyo ya jinai namba 15 ya mwaka 2023 ni pamoja na aliyekuwa Mkuu wa Upelelezi wa Wilaya ya Mtwara, Gilbert Sostenes Kalanje na Mkuu wa Kituo cha Polisi Mtwara, Charles Onyango.

Wengine ni aliyekuwa Ofisa Intelijensia ya Jinai Mkoa wa Mtwara, Nicholaus Kisinza, Marco Mbuta, Mkaguzi wa Polisi, John Msuya, aliyekuwa mganga mkuu wa Zahanati ya Polisi Mtwara, Shirazi Mkupa na Koplo Salim Mbalu.

Maofisa hao wa Polisi wanakabiliwa na shtaka moja la mauaji wakidaiwa kumuua kwa makusudi Mussa waliyemchoma sindano ya sumu katika kituo cha Polisi Mitengo Wilaya ya Mtwara, Mkoa wa Mtwara, Januari 5, 2022.

Hata hivyo, wakati polisi hao wakiwa mahabusu kabla ya kupandishwa kizimbani, mtuhumiwa mwenzao, Grayson Mahembe alidaiwa kujinyonga hadi kufa Januari 22, 2022 akiwa mahabusu.

Kesi hiyo inasikilizwa na Jaji Edwin Kakolaki kutoka Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam.

Katika ushahidi wake akiongozwa na mwendesha mashtaka, Wakili wa Serikali Mkuu, Pascal Marungu aliieleza mahakama kuwa Mussa aliuawa na SP Kalanje Kwa kumziba kwa tambala mdomoni na puani, muda mfupi baada ya Dk Msuya (mshtakiwa wa Tano) kumdunga sindano ya usingizi.

Shahidi huyo aliieleza Mahakama kuwa alipata taarifa za tukio hilo baada ya kuwahoji baadhi ya askari waliokuwa zamu katika kituo cha Polisi Mitengo, pamoja na Dk Msuya mwenyewe na ofisa wa polisi, Grayson (marehemu kwa sasa) ambao walisimulia tukio hilo.

Kwa mujibu wa shahidi huyo, siku ya tukio Januari 5, 2022, mshtakiwa wa kwanza, SP Kalanje alimpigia simu Dk Msuya akamtaka waonane na Dk Msuya ambaye al8ikaribisha ofisini kwake katika zahanati ya Polisi na wakazungumza.

Alidai kuwa SP Kalanje alimueleza Dk Msuya kuwa wana mtuhumiwa wao wa wizi wa pikipiki ambaye amekuwa akifanya matukio ya wizi huo maeneo mbali katika mikoa ya Mtwara, Lindi na Dar es Salaam na amekuwa akiwasumbua hivyo wanataka wammalize.

Hivyo alidai kuwa SP Kalanje alimuuliza Dk Msuya kama anaweza kufanya namna ya kupata sindao ya sumu ili wamdunge, lakini Dk Msuya alimjibu kuwa tangu aajiriwe na kuapa kuwa daktari hajawahi kumdunga mtu sindano ya sumu.

Shahidi huyo amedai kuwa badala yake. Dk Msuya alimshauri SP Kalanje wamdunge sindano ya usingi , akizinduka ataanza kueleza matukio yote ya wizi aliyoyafanya, ushauri ambao Kalanje alikubaliana nao.

Kwa mujibu wa shahidi huyo, licha ya SP Kalanje kutaka waende kutekeleza mpango huo wakati huohuo, lakini Dk Msuya alimueleza kuwa wakati huo bado alikuwa na wagonjwa wengine akiwahudumua na akashauri wafanye baadaye.

Saa 8:30 mchana, Kalanje alifika ofisini kwa Dk Msuya kwa ajili ya kutekeleza mpango huo kama walivyokuwa wamekubaliana, hivyo alimuuliza kama alikuwa tayari akamjibu kuwa alikuwa tayari.

Lakini Dk Msuya alimuuliza SP Kalanje mahali alikokuwa huyo mtuhumiwa wao, akamjibu kuwa alikuwa katika kituo cha Polisi Mitengo.

Kwa mujibu wa shahidi huyo, Dk Msuya alisema yeye anaelewa kituo cha Mitengo kina wahalifu sugu hivyo akajua na huyo amehifadhiwa kwa wahalifu sugu, akakubali akaingia kwenye gari na akakaa kiti cha mbele huku gari likiendeshwa na SP Kalanje.

Wakati gari inaondoka pale zahanati, Dk Msuya alihisi kama viti vya nyuma vina watu.

Hivyo aligeuka kutazama akawatambua watu wawili, ambao ni ASP Onyango na A/Insp Grayson waliokuwa wamekaa viti vya pembeni kulia na kushoto na katikati kulikuwa na mtu mwingine ambaye hakuweza kumtambua.

Waliendelea na safari hadi kituo cha Polisi Mitengo na SP Kalanje alishuka akaenda kuzungumza na mkuu wa kituo hicho, Paulo Kiula.

Dk Msuya na askari wale wawili pamoja na yule mtu ambaye hakumtambua nao walishuka wakamfuata SP Kalanje na mkuu wa kituo walipokuwa wanaelekea ndani ya jengo la kituo hicho.

Dk Msuya alimuomba OCS Kiula amuonyeshe Kalanje ofisi moja ambayo aliingia Kalanje, Onyango, Grayson na yule kijana na yeye akabaki nje.

Lakini baada ya dakika tatu hivi, naye alingia ndani ya hiyo ofisi na alimkuta yule kijana amevuliwa shati yuko kifua wazi na mikono yake ikiwa imefungwa kwa kamba kwa nyuma akiwa amelala kwenye sakafu huku akilia.

SP Kalanje alimwambia Dk Msuya amdunge sindano ya usingizi mkono wa kulia yule kijana.

Na baadaye kidogo, Dk Msuya anasema alimsikia Kalanje akisema huyo anawachelewesha, akachukua tambala akamziba yule kijana pua na mdomo.

Anasema baada ya Dk Msuya kuona vile aliamua kutoka nje akawaacha Karanje na wale wenzake na yule kijana akiwa amelala chini.

Lakini baada ya muda mfupi, Kalanje alimuita Dk Msuya akamuuliza, "tayari?" huku akimuonyesha yule kijana pale chini.

Dk Msuya alimuangalia kama hapumui lakini hakumpima ila alielewa lile swali la SP Kalanje kwamba lilikuwa linamaanisha kama amekufa na yeye alijibu kuwa tayari.

Hivyo wote walitoka mle chumbani na kumuacha yule kijana akiwa amelala pale chini.

SP Kalanje alikwenda kwa OCS akachukua kufuli likiwa na funguo akafunga mlango kisha wakaondoka wote akiwa na huo ufunguo, wakapanda gari na kuondoka.

Kamanda huyo wa polisi ambaye ni shahidi, aliieleza Mahakama kuwa baada ya maelezo hayo ya mdomo kutoka kwa Dk Msuya, alielekeza yaandikwe maelezo kama alivyosimulia na maelezo yake yawekwe kwenye jalada la uchunguzi.

“Wakati huo tulimchukulia Dk Msuya kama mtoa taarifa,” alidai Kamanda Mgonja.

Alidai wakati yote hayo yakifanyika, alijiuliza hayo mauaji ni ya huyo kijana Mussa ambaye ndugu zake walikuwa wanamtafuta au kuna mwingine?

"Hivyo nikaagiza atafutwe mjomba wa Mussa Hamis anayeitwa Salum Mombo aje ofini kwangu, alikuja nikamtaka anitafutie picha za Mussa kusudi ili niangalie yule mtu ambaye askari wanasema walimuona akiingia pale Mitengo ndiyo huyu kijana Mussa Hamis au ni mwingine,” alieleza.

Shahidi huyo alieleza kuwa mjomba huyo akiwa ofini kwake alipiga simu Nachingwea kwa baba wa kufikia wa Mussa akamtaka atafute picha zake azitume kwenye gari.

"Kesho yake Januari 22, 2022 zililetwa picha nikazitazama nikamkabidhi ASP Esau ili waendelee na utaratibu wa upelelezi,” alieleza ACP Mgonja.

Alidai kulikuwa na mauaji Januari 21,2022 niliagiza apatikane Grayson ambaye alikuwa mahabusu Tandahimba, kwanza kati ya watu wote waliotajwa yeye alikuwa ametajwa maeneo mengi.

Alieleza kuwa baada ya Grayson kuletwa aliongeza timu ya wapelelezi akiwajumuisha askari watano wa timu ya Task Force waliokuwa wanashughulikia magaidi wakingozwa na SP Simba, hivyo ikawa timu ya wapelelezi 10 akiwemo yeye mwenyewe.

"Tulifikiri kwa pamoja tukakubaliana tumlete Dk Msuya ili asimulie mbele ya Grayson nini kiliendelea pale Mitengo kama alivyonisimulia mimi.”

"Kwa kuwa Msuya alishuhudia kila kitu kilichofanyika pale Mitengo na Grayson akiwepo, kwa hiyo sisi kama makachero tuliona Grayson akisikia, basi mahojiano yetu naye yatakuwa rahisi."

Shahidi huyo alihitimisha Kwa kueleza kuwa katika mahojiano ya mdomo waliyoyafanya na Dk Msuya mbele ya Grayson, alisimulia kama alivyokuwa amemsimulia yeye na walipomuuliza Grayson, alikubali kuwa alivyosimulia Dk Msuya ndivyo walivyofanya.

“Hivyo mimi kama RCO picha iliyoniijia kichwani ni kwamba, haya sasa ni mauaji na kama ni mauaji hakuna mauaji ambayo hayana mwili au mtu aliyeuawa, hivyo nikamtaka Grayson atuonyeshe huyo ambaye wamemuua yuko wapi."

Hata hivyo wakati shahidi huyo anataka kueleza kile Grayson alichosema, kiongozi wa jopo la mawakili wa utetezi, Majura Magafu aliweka pingamizi akisema kwa kuwa Grayson si mshtakiwa wala shahidi, hawezi kutoa maelezo yake kwa sababu hawatapata fursa ya kumhoji kuhusu ukweli wake.

Pingamizi hilo liliibua mvutano wa hoja na upande wa mashtaka na Jaji Kakolaki baada ya kusikiliza hoja za pande zote aliahirisha kesi hiyo Kwa ajili ya kuandika uamuzi wake.
[emoji24][emoji24]
 
Moja kati ya kesi ambayo nilikuwa natamani sana kujua mwendelezo wake, naomba tu haki itendeke.
Changamoto ni kwamba, kisheria, hao watuhumiwa kwa sasa ni sawa na wewe uliye uraiani yaani hawana hatia kwa sasa.

Zaidi sana sheria za jinai hutafsiriwa katika kumlinda mtuhumiwa dhidi ya uonevu wa Serikali, yaani serikali inatakiwa ithibitishe pasina shaka kwamba waliua kweli.

Mfano, ukirudia kuisoma hii habari kuna maelezo kwamba marehemu alichomwa "sindano ya sumu" mengine marehemu "alichomwa "sindano ya usingizi na pia marehemu "alifungwa na kuzibwa pua na mdomo" .

Sasa kama ndivyo ilivyo kisheria, na kwa kuwa shahidi wa kwanza ndiye kayasema haya mahakamani, na kwa kuwa shaidi namba moja ndiye mbeba kesi, na ikiwa Jaji atazingatia haya maelezo, basi tayari chanzo cha kifo cha marehemu kina utata na hapo huenda watuhumiwa wakakutwa na kosa dogo ama wakaachiwa huru.
 
Hii kesi ngumu sana na Kuna watu wanaenda kula nyundo za kutosha mana ingekuwa ameuliwa mtu ambae Hana connection yoyote ingekuwa kesi ishazimwa na wangesema mtuhumiwa bwana hamis kajinyonga mwenyewe.!

Lakin hata kosa alilofanya mpaka wakamuuwa hawalisemi kafanya Nini.

Polisi wakitaka kukutia hatiani kwanza wanakupa jina baya kama hawakuita unatumiwa na magaidi basi watakupa hata kesi za bangi na unga !

Huyu mchizi alikuwa na Hela na alikuwa na ushamba flani hivi mana kapata Hela ukubwani alafu za haraka haraka sasa akawa anaruka majoka sana .Nasikia alikuwa anatoka na kibegi Cha Hela kwenda kula Bata ndio wale wajomba wakatonywa kuwa Kuna mchizi anatamba huko viwanja na kibegi Cha Hela

Tatizo likaanzia hapo.

Polisi wengi Huwa hawana roho za kibinadamu kabisa .wao wanaishi kama wanyama

Wanahisi wakishakutoa roho ni kama ndio wamemaliza maisha yako. Wasichokijua ni kuwa kufa sio mwisho WA maisha.!
Mkuu,naomba nikumbushe kisa cha huyu kijana hadi kufikia kuuawa na polisi.

Sent from my SM-A037F using JamiiForums mobile app
 
Ninamfahamu sana huyo Mkuu wa Upelelezi SP Gilbert Kalanje ambaye Shahidi anasema ndie aliyemziba na tambala Marehemu,actually nilikuwa Askari Polisi na huyo Gilbert tuliingia nae Depo moja CCP mwezi Juni 1998 na tukamaliza Februari 1999 na wote tukapangwa kazi Kituo cha Polisi Oysterbay japo mimi baadaye nilikuja kuacha kazi kwa hiari. Maisha haya Mungu tu ndie anayejua,niishie hapa NB:kwenye picha Gilbert Kalanje ni yule mwishoni kulia, alifanya sana kazi Kituo cha Polisi Oysterbay na Kituo cha Polisi Kawe
Jamaa yako amekaa kiuhuruma kwenye picha..hii kazi bora umeacha ni kazi ya laana.
 
Ninamfahamu sana huyo Mkuu wa Upelelezi SP Gilbert Kalanje ambaye Shahidi anasema ndie aliyemziba na tambala Marehemu,actually nilikuwa Askari Polisi na huyo Gilbert tuliingia nae Depo moja CCP mwezi Juni 1998 na tukamaliza Februari 1999 na wote tukapangwa kazi Kituo cha Polisi Oysterbay japo mimi baadaye nilikuja kuacha kazi kwa hiari. Maisha haya Mungu tu ndie anayejua,niishie hapa NB:kwenye picha Gilbert Kalanje ni yule mwishoni kulia, alifanya sana kazi Kituo cha Polisi Oysterbay na Kituo cha Polisi Kawe
Kumbe ana koneksheni mjini ndio maana anajidai sana
 
Kila siku Huwa nasema polisi wa Tz ni viumbe hatari Sana wakijua una pesa watu hunibishia hakika hii ni Zaid ya aibu askari kuua Kwa akili ya 70m!?
 
Greyson wakat kesi inaanza yeye ndo alikuwa wa kwanza kukamatwa,hvyo wakubwa wakamuua akiwa mahabusu ili kuficha ushahidi
Wakasingizia eti kajiua kwa kujinyonga na tambara la dekio
BaBA greyson wakat anapokea mwili wa mwanae alisema haamin kabisa kama mwanae alijiua na alisema kuna kitu na waliomuua na wao litawakuta jambo
Mzee mzito
 
In short kuwa askari kwa nchi kama Tanzania ni sawa na mtu aliyelaaniwa.

Babu yangu mzaa mama wakati watoto wake wanachagua kazi za kufanya aliwaonya asithubutu hata mmoja kujisemea anataka kuwa askari,yeye aliutafsiri uaskari kama kazi ya dhulma na ukiangalia matukio wanayofanya hawa mabwana huwezi kuwatenganisha hata nukta na laana.

Ukute huyu babu alikuwa mwanachama wa ccm,halafu anazungumza kuhusu dhurma.
 
Hao ndio askari wetu, uhakisia wao.
Mie hata ndugu au jamaa yangu akiwa askari najiweka nae mbali, moyo unaweza ukamuamini lakin akili inaniambia ndio wale wale.

Kula pini kabisa,na siku wenzie wakikutight kwenye 18 ndio utajua hata povu linaloelea huwa ni tumaini kwa anayezama maji[emoji23][emoji23][emoji23].

Hutakiwi kumwamini mtu yoyote,weka nafasi ya mashaka kwake.
 
Bora sisi tunafundishwa zaidi maisha na kufanya mema na kukataa mabaya
Ila hawa sijui huwa wanafundishwa nini huku, kuiba na kuuwa na chuki
Kwa kweli siwezi kuwaza hata siku moja kukopa kwa riba, au kuuwa, kudanganya, kuroga na mengi kwa sababu ndio mwalimu na wazazi walikuwa wanatufundisha kila siku hata uzinzi
Hivi huwa wanafundishwa nini kama EPA na ESCROW waligawiwa mpaka waalimu wao?
Tegemea mengi sana na hii ni tip of the iceberg

Kwahiyo mujahdeen akifanya hayo kafundishwa pia!!!!
 
Kwahiyo mujahdeen akifanya hayo kafundishwa pia!!!!
Tumekatazwa kuuwa period
Anaeuwa anapata dhambi kubwa sana
Mimi sikubaliani na wizi, mauwaji na mabaya yote
Hapa tunaongelea mafundisho mema
Kama hutamkunja samaki akiwa mbichi haya ndio matokeo yake
Kupata watu wa hovyo
 
Ukisoma vizuri maelezo ya Dr, hakuwa anajua kuwa mtuhumiwa ni nani, na askari wana mpango gani nae, wameingia ndani yeye alichokuwa anajua ni kwenda kumchoma sindano ya usingizi na sio kuua, iyo inamuondoa hatiani
Hao wote ni co accused
Vicariously wako liable ila anaweza angukia kwenye manslaughter
 
Mussa Hamisi hakuwa tajiri hata kidogo. Ni kizazi masikini na alikua anachimba madini shimo likatema akadhulumiwa na hao polisi wakaona itakuwa msalama wakaamua wamzime kama taa.
Sema hii kesi ina mkono wa Katelephone waziri mkubwa. Yeye ndo alifosi mpaka tume iundwe ya kufanya uchunguzi kupitia Mkuu wa Mkoa wa Mtwara ambaye alikua Kanali wa Jeshi kama sikosei.
Otherwise wangeizima kimya kimya. Polisi sio watu.
Ndugu wa huyu dogo na ukaribu na PM ndio maana ngoma mbichi vinginevyo ilikuwa kwishnei
 
Tumekatazwa kuuwa period
Anaeuwa anapata dhambi kubwa sana
Mimi sikubaliani na wizi, mauwaji na mabaya yote
Hapa tunaongelea mafundisho mema
Kama hutamkunja samaki akiwa mbichi haya ndio matokeo yake
Kupata watu wa hovyo

Hakuna binaadam mwenye akili timamu anayesubiri kukatazwa kuua ndipo aone kama ni jambo baya.

By the way wapo wenzako wameielewa dini kukuzidi wanaua sababu ya dini hiyo hiyo na mafundisho yake,unazungumzaje kuhusu hilo!!!
 
Back
Top Bottom