Mtwara: Maafisa Saba(7) wa Polisi wafikishwa Mahakamani kwa tuhuma za mauaji ya Kijana aliyekuwa akiwadai zaidi ya Tsh milioni 33.7

Unachotetea wewe NI nini mpaka unapanic?
Una matatizo ya AKILI?
Au unalipwa?
Sasa litachunguzwa majibu upewe wewe kiazi mviringo!!!

Endelea kumwona shujaa wako maana kwa uvivu wa akili ulio nao hata mgonjwa wa akili anawezakuwa masihi kwako.
 
ukiona kamanda wao (
Ukiona kamanda wao (ZIRO) ametinga mtwara basi ujue kuna jambo linaenda kutengenezwa. lengo ni kupoteza tusijue kitachojiri... ukichanganya kujinyonga /kunyongwa wanakosema... siwezi amini hili linawezekanaje kirahisi hivi ndani ya selo. ZIRO kahojiwa kiduchu tu kachomoa anamlengesha BOSS wake ndio atajibu mambo ya polisi wake .
TUENDELEE KUTEGA SIKIO HUENDA AKAUMBUKA NTU FULANI BAH!
 
Unachotetea wewe NI nini mpaka unapanic?
Una matatizo ya AKILI?
Au unalipwa?
Hakuna ninachotetea soma vizuri, naweka sawa bichwa lako.

Wewe polisi 7 wako matatani kwa kuua mtu mmoja, ulivyo mbuzi unasema ndio maana hamza shujaa wako kisa aliua polisi barabarabi pale!!!

Akili umebadiri na mkate ama!!!!
 
Said Mwema ndo alikua IGP makini.
Siro na Mahita ndo ma IGP wa hovyo sana.
Said mwema kipind chake polisi walikuwa Wana uwa watu ujambazi wa ma benki ulishamil kweli ukitoka benk Una porwa pesa na uhalifu wa pikipik ulikuwa kawaida
 
unajua walichomfanya Hamza?
Unajua maumivu aliyoyapata Hamza?
Si Bora wao wapo MAHABUSU vipi Yule waliyemuua na kimtupa!
Yaani damu ya MTU wewe unaona haina maana Ila hao polisi kukaa rumande ndo inakuuma?
Hamza angekuwa gaidi angechagua watu wa kuuaa?
Sirro alishindwa vipi kufanya uchunguzi kujua chanzo Cha Hamza ni nini mpaka akaamua kuua polisi?
Walifumbia macho tukioa Hamza Leo wanaumbuka.KARMA KARMA KARMA,
kiufupi polisi waache DHULMA
Hakuna ninachotetea soma vizuri, naweka sawa bichwa lako.

Wewe polisi 7 wako matatani kwa kuua mtu mmoja, ulivyo mbuzi unasema ndio maana hamza shujaa wako kisa aliua polisi barabarabi pale!!!

Akili umebadiri na mkate ama!!!!
 

Acha ujinga hata kama ni fani yako, anatia watu hasara.
Nimekuuliza ripoti ya hamza ulitaka upewe wewe!!!wewe unajua hamza alifanya nini!!
Hujui magaidi huwa wanachagua wa kuua!!unawajua magaidi!!!

Hakuna sehemu nimesema nimesema naona sawa mtu kuuawawa na polisi labda unipe ushahidi, nakushangaa wewe toka post yako niliyoinukuu ukimsifu shujaa wako hamza, yaani wewe, hamza na hao polisi 7 watuhumumiwa mna tofauti gani ya kimsingi kama sio nafasi tu!!!

Unalaumu unyama wa polisi 7 halafu unamsifu hamza!!!ni nani yako hamza!!!
 
Na huyo wa mtwara alikuwa gaidi?
 
Hamza NI shujaa aliyepinga DHULMA.
 
hapo umeshindwa kutambua kwamba matokeo ya magumu yao tunayalipa sisi maraia Kama ilivyotokea kwa huyo jamaa wa Mtwara. Mambo yakiwa tight kwao wanatupress zaid raia ili kuziba Hilo gap. Leta hoja nyingine
 
too little too late
 
#ZILIZOTUFIKIA Jeshi la Polisi Mkoani Mtwara limewakamata na kuwafikisha mahakamani Maafisa wa Polisi saba kwa tuhuma za kufanya mauaji ya Mussa Hamisi Hamisi (25) mkazi wa Kijiji cha Ruponda wilaya ya Nachingwea Mkoani Lindi.

Mauaji hayo yamefanyika baada ya marehemu Mussa Hamisi kudai fedha zake Sh milioni 33,748,980 ambazo maafisa hao wanadaiwa kuzichukua kutoka kwa kijana huyo baada ya kumfanyia upekuzi.

Kulingana na taarifa iliyotolewa na Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Mtwara, ACP Marck Njera imesema mauaji hayo yalifanyika Januari 5, 2022 na mwili wa marehemu ulitupwa kitongoji cha Majengo kijiji cha Hiari Wilayani Mtwara.

Maafisa wanaoshikiriwa ni Mrakibu wa Polisi Gilbert Kalanje -Mkuu wa Upelelezi wa wilaya ya Mtwara, Mrakibu Msaidizi wa Polisi Charles Onyango -Mkuu wa Kituo cha Polisi Mtwara, Mrakibu wa Polisi Msaidizi Nicholaus Kisinza -Mkuu wa Kikosi cha Intelejensia ya Jinai mkoa wa Mtwara, Mkaguzi wa Polisi John Msuya Mganga- Mkuu wa Zahanati ya Polisi Mtwara, Mkaguzi wa Polisi Msaidizi Marco Mbuta, Mkaguzi wa Polisi Shirazi Mkupa na Koplo Salimu Juma Mbalu.

Uchunguzi wa tukio hilo bado unaendelea.

Imeandaliwa na Anne Robi

#HabarileoUPDATES
#Mauaji
#Polisi
#tanzania[emoji1241]
 
Polisi nao wameanza kuunda magenge ya uhalifu.
Kila mbuzi atakula urefu wa kamba yake
 
Mwl Nyerere aliwahi kulivunja Jeshi la King African Rifles baada ya Maasi
Why don't be to this PT
Hili jeshi livunjwe maana hawajui majukumu yao wamekazana na philosophy yao ya kuajiri waliofeli form four wengi hadi mipaka ya nchi wengine hawajui hili jeshi limekuwa fedheha sana inapaswa kuvunjwa na kusukwa upya na katiba ongozi ya polisi ibadilishwe na chombo kiundwe cha kusimamia nidhamu za Askari na uwajibikaji ....
 
Jeshi wanaajiri waliofeli wanaajiri watu wasio na utu kwa jamii ..jeshi hili livunjwe raia washapoteza matumaini na hili jeshi la foolish
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…