Mtwara: Maafisa Saba(7) wa Polisi wafikishwa Mahakamani kwa tuhuma za mauaji ya Kijana aliyekuwa akiwadai zaidi ya Tsh milioni 33.7

Hapo inapaswa, kukamatwa mkuu wahicho kituo na hao askari wote kuwekwa ndani, RPC Lindi afutwe kazi mara moja, RC Lindi afutwe kazi mara moja... Waziri mambo ya ndani na Naibu wake wajiuzuru mara moja kama walikuwepo ofisini wakati tukio linatokea.... kama sio wao basi waliokuwa mawaziri kama wako kwenye nyadhifa nyingine watolewe mara moja.. IGP atolewe kazini mara moja..

Jeshi la Polisi linahitaji reform ya nguvu pamoja na kubadili mitaala kule CCP na mfumo mzima wa kurecruit....

Serikali inabidi ianzishe mtaala mashuleni kuanzia msingi mpaka sekondari unaoweza kuelimisha Watanzania juu ya uthamani wa maisha ya binadamu, utu, utaifa na jamii kupendana ...
 
Uko sahihi kabisa ila wakati wapinzani wakiuliwa mbona tulikaa kimyaaaaa? Mbona tulishangilia? Hakuna aliyesema kuwa Polisi wasifanye au wasiingilie mambo ya siasa? Haya sasa ndio mavuno yake. Wala sijashangilia nazungumzia facts

Nakubaliana na wewe, hakuna yeyoye aliyestaarabika anayependa Polisi kuingilia Siasa....ila nimetoa tahadhari dhidi ya wanasiasa kutumia hiyo loophole ya nguvu yetu wananchi wao kuichokoza dola kwa makusudi kupitia vyombo vyake ili wapate huruma yetu kutwaa madaraka...
 
Wajameni maswali mengi majibu hakuna,Hawa viumbe Wana roho mbaya sana,
Bora uingie genge la simba kuliko Police tz utajuta Aisee!
 
Kila siku mauaji ya raia yanayofanywa na polisi yanaongezeka . Na imekuwa too much maana hatuoni IGP akichukua hatua.

Tetesi zinasema nikwakuwa alie uwawa anatoka anakotoka PM ndio maana hayo yamegundulika. Hata sim iliotoa maagizo ni yakule... Je wangapi wanapotea kwa staily kama hii... Inatisha sana
 
Wayanyonge. Kabla ya kuyanyonga wayapeleke jela wakakutane na waliowabambikia kesi wakawalawiti kwanza kufidia uchungu waliowasababishia.
Polisi hata kama ni ndugu yako chunga sana asikujuejue. Ni mijahilia hii mijaa laana.
Duh uchungu eee?;!!!!
 
Naam. Nakubaliana na wewe pia ila kwa hili hapana, ni mbegu ambayo tuliipanda, tukaipalilia! Ikawa Ili uitwe Mzalendo basi ushangilie maumivu ya mpinzani dhidi ya Dola, ila HATUJACHELEWA KUANZA UPYA!

LEO hii Watu wameanza kupotea Tena, ukienda Polisi hakuna maelezo ya maana, tunaowapoteza ni ndugu zetu, ni watoto na kaka/dada zetu.
 
[emoji24][emoji24][emoji24][emoji24][emoji24][emoji24]
 
Moja ya matatizo yaliopo Nchii hii Ni pamoja na jeshi la polisi.
 
Nimesikitika mno na nimetoa machozi
 
Kwa kiasi cha pesa walizochukuwa kabla ya kumuuwa, lazima kuna mkubwa alishiriki. Na kwa hivyo lazima huyo askari mmoja atakuwa kanyongwa huyo kuharibu ushahidi.
 
Nilikuwa mtwara toka ijumaa ndio stori imezagaa mjini , kwa kweli hawa polisi wamefanya tendo la kikatili sana akiongozwa na mkuu wa kituo

Sent from my JKM-LX1 using JamiiForums mobile app
Inasemekana walitumia sindano ya sumu kumuuwa na kisha wakamtupa baharini.

Njia waliyoitumia kumuuwa inaonekana wazi kabisa kuwa ni wazoefu kwenye mauwaji. Ina maana kuna uwezekano wa vifo vingi vyenye utata ambavyo polisi wamehusika.
 
Hii kazi taabu tupu laana inawafate waliotenda
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…