Mtwara: Maafisa Saba(7) wa Polisi wafikishwa Mahakamani kwa tuhuma za mauaji ya Kijana aliyekuwa akiwadai zaidi ya Tsh milioni 33.7

Mtwara: Maafisa Saba(7) wa Polisi wafikishwa Mahakamani kwa tuhuma za mauaji ya Kijana aliyekuwa akiwadai zaidi ya Tsh milioni 33.7

FB_IMG_1644039316577.jpg
 
Ndo maana braza Hamza akaamua kufanya yake.
Wakampa na cheo Cha ugaidi.
Nadhani sasa wabadili jina lingine la kesi ya kubambikia, hilo la ugaidi limewashinda. Kesi ya Mbowe pia wameumbuka kwa kubambikia kesi yenye jina hilo.
 
Laiti police wangemdhibiti aliyemtolea nape bastola, mfanyabiashara wa madini asingeuwawa.
 
Jeshi la Polisi lifumuliwe lote kuanzia IGP mpaka mfumo wake wote. Ni wazi, kuna uozo (saratani) usiopona.

Tatizo husababishwa na wakuu wa mikoa na wakuu wa wilaya (kamati za ulinzi) hata Rais au mawaziri wenye dhamana kubwa kubwa wanapolitumia jeshi la polisi kama nyenzo yao binafsi ya kufanyia watu "extortion".

Hata uwe mkuu vipi, ukishampa na kumuachia polisi akufanyie na au akufichie dhambi zko, inakuwa umeshampa yeye mpini na wewe umeshayashika makali. Umeshamfanya kuwa jambazi wewe mwenyewe, kwa dhambi zako tu.

Tuwaiteni Waingereza waje kuliunda na kulinoa upya jeshi la polisi, walipoondoka nnaamini hawakutuachia uozo huu.
 
Mawazo yako mazuri lakini bila kuwatenganisha police na wanasiasa, police wataendelea kulaumiwa Sana kwa kutii maagizo ya wanasiasa.
Kama mwanasiasa ndie Mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama police watakuaje huru sasa. Na Mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama ni lazima uwe ccm Ili mshirikiane na wakuregenzi kuiba kura.
Kumbuka ukiwa police ni marufuku kuhoji, kupinga amri yeyeto toka juu uwe unapenda upendi.
 
Jeshi la Polisi lifumuliwe lote kuanzia IGP mpaka mfumo wake wote. Ni wazi, kuna uozo (saratani) usiopona.

Tatizo husababishwa na wakuu wa mikoa na wakuu wa wilaya (kamati za ulinzi) hata Rais au mawaziri wenye dhamana kubwa kubwa wanapolitumia jeshi la polisi kama nyenzo yao binafsi ya kufanyia watu "extortion".

Hata uwe mkuu vipi, ukishampa na kumuachia polisi akufanyie na au akufichie dhambi zko, inakuwa umeshampa yeye mpini na wewe umeshayashika makali. Umeshamfanya kuwa jambazi wewe mwenyewe, kwa dhambi zako tu.

Tuwaiteni Waingereza waje kuliunda na kulinoa upya jeshi la polisi, walipoondoka nnaamini hawakutuachia uozo huu.
1647433727661.png

bibi upooooo!!
 
Kila siku mauaji ya raia yanayofanywa na polisi yanaongezeka . Na imekuwa too much maana hatuoni IGP akichukua hatua.

=====

JESHI la Polisi Mkoani Mtwara limewakamata na kuwafikisha mahakamani Maafisa wa Polisi saba kwa tuhuma za mauaji ya Mussa Hamisi Hamisi (25) mkazi wa Kijiji cha Ruponda wilayani Nachingwea Mkoani Lindi aliyekuwa akiwadai askari hao zaidi ya Sh milioni 33.7.

Inadaiwa maafisa hao wa polisi walijipatia kiasi hicho cha pesa wakati wakimfanyia upekuzi mfanyabiashara huyo. Taarifa iliyotolewa na Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Mtwara, ACP Marck Njera imesema mauaji hayo yalifanyika Januari 5, 2022 na mwili wa marehemu ulitupwa kitongoji cha Majengo kijiji cha Hiari Wilayani Mtwara.

Maafisa wanaoshikiriwa ni Mrakibu wa Polisi Gilbert Kalanje -Mkuu wa Upelelezi wa wilaya ya Mtwara, Mrakibu Msaidizi wa Polisi Charles Onyango - Mkuu wa Kituo cha Polisi Mtwara, Mrakibu wa Polisi Msaidizi Nicholaus Kisinza - Mkuu wa Kikosi cha Intelejensia ya Jinai mkoa wa Mtwara, Mkaguzi wa Polisi John Msuya Mganga - Mkuu wa Zahanati ya Polisi Mtwara, Mkaguzi wa Polisi Msaidizi Marco Mbuta, Mkaguzi wa Polisi Shirazi Mkupa na Koplo Salimu Juma Mbalu.

Uchunguzi wa tukio hilo bado unaendelea.

Chanzo: Habari leo

Pia soma: Mtwara: Askari Polisi mmoja kati watuhumiwa wa mauaji ya mfanyabiashara alikutwa mahabusu akiwa amejinyonga tarehe 22 Jan 2022

- SIMULIZI: Mauaji ya Mfanyabiashara Musa Hamis Mtwara, Machozi na Damu
Nasisitiza ukiwa na shida ukaenda polisi kupata haki yako yaweza kuwa mauti yako.
Maharamia na majangili kabisa hawa…
 
Back
Top Bottom