Aisee halafu wamejikausha Tu na kuendeleza uchawa ,mambo ya msingi kama haya huwezi kuona wanafuatilia na kureportVyombo vya habari kama Ayo Tv wanatakiwa watujulishe issue kama hizi.
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Aisee halafu wamejikausha Tu na kuendeleza uchawa ,mambo ya msingi kama haya huwezi kuona wanafuatilia na kureportVyombo vya habari kama Ayo Tv wanatakiwa watujulishe issue kama hizi.
Balozi ChangamotoView attachment 2329202
Shikamoo Balozi!!!
kwani yeye ndiye kamtuma amtaje ktk ufala wake wa kulewa???Cc Mh. Simbachawene. Askari siyo wa kuwaachia eti wadili na mwanao, baadhi yao ni wauji.
Asantekwani yeye ndiye kamtuma amtaje ktk ufala wake wa kulewa???
mtoto wa kigogo unatakiwa ujue namna ya kutunza heshima ya mzee wako.
Ushaidi haitoshi wataachiwa huruHawa Jamaa kesi yao ikoje?
Upolisi ni kazi ya laana. Wanamuua mtu kwa sababu ya milioni 33? Hawa jamaa wehu kweli!Kila siku mauaji ya raia yanayofanywa na polisi yanaongezeka . Na imekuwa too much maana hatuoni IGP akichukua hatua.
=====
JESHI la Polisi Mkoani Mtwara limewakamata na kuwafikisha mahakamani Maafisa wa Polisi saba kwa tuhuma za mauaji ya Mussa Hamisi Hamisi (25) mkazi wa Kijiji cha Ruponda wilayani Nachingwea Mkoani Lindi aliyekuwa akiwadai askari hao zaidi ya Sh milioni 33.7.
Inadaiwa maafisa hao wa polisi walijipatia kiasi hicho cha pesa wakati wakimfanyia upekuzi mfanyabiashara huyo. Taarifa iliyotolewa na Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Mtwara, ACP Marck Njera imesema mauaji hayo yalifanyika Januari 5, 2022 na mwili wa marehemu ulitupwa kitongoji cha Majengo kijiji cha Hiari Wilayani Mtwara.
Maafisa wanaoshikiriwa ni Mrakibu wa Polisi Gilbert Kalanje -Mkuu wa Upelelezi wa wilaya ya Mtwara, Mrakibu Msaidizi wa Polisi Charles Onyango - Mkuu wa Kituo cha Polisi Mtwara, Mrakibu wa Polisi Msaidizi Nicholaus Kisinza - Mkuu wa Kikosi cha Intelejensia ya Jinai mkoa wa Mtwara, Mkaguzi wa Polisi John Msuya Mganga - Mkuu wa Zahanati ya Polisi Mtwara, Mkaguzi wa Polisi Msaidizi Marco Mbuta, Mkaguzi wa Polisi Shirazi Mkupa na Koplo Salimu Juma Mbalu.
Uchunguzi wa tukio hilo bado unaendelea.
Chanzo: Habari leo
Pia soma: Mtwara: Askari Polisi mmoja kati watuhumiwa wa mauaji ya mfanyabiashara alikutwa mahabusu akiwa amejinyonga tarehe 22 Jan 2022
- SIMULIZI: Mauaji ya Mfanyabiashara Musa Hamis Mtwara, Machozi na Damu
Simuamini Polisi yeyote,hata IGP,mbona naye ametokea ranks za chini.Wanyongwe wote waliohusika na tukio hili this is too much very painful
IGP say something
Ukisoma injili ya Luka, sura ya 3 msitari wa 14, wanachofanya hawa jamaa kilishaandikwa kitambo sana. Msimshitaki mtu kwa uwongo, msidhulumu, toshekeni na mishahara yenu!Upolisi ni kazi ya laana. Wanamuua mtu kwa sababu ya milioni 33? Hawa jamaa wehu kweli!
Kuna watu wengine uwezo wao wa kufikiri ni mfupi sana, alafu kibaya zaidi wamebahatika kuingia kwenye mfumo wetu wa utowaji haki! kuna watu wengine huko wanachukua hadi M100 kwa sound tu,alafu mwisho wa siku inabaki kua kesi ya madai mnaenda mdogomdogo huku maisha mengine yakiendelea!!Upolisi ni kazi ya laana. Wanamuua mtu kwa sababu ya milioni 33? Hawa jamaa wehu kweli!