Mtwara: Mjomba wa mfanyabiashara aliyeuawa adai alitishiwa kupewa kesi ya ugaidi endapo ataendelea kufuatilia suala la mpwa wake

Mtwara: Mjomba wa mfanyabiashara aliyeuawa adai alitishiwa kupewa kesi ya ugaidi endapo ataendelea kufuatilia suala la mpwa wake

Nilitoa Rai kwamba Mheshimiwa Rais anakosea Sana anapotembea na watu wa kurithi ambao wamejaa hujuma ndani yake. Sijui ni Kwa nini hajaamua kuingia kwenye hizi taasisi. Nimesikitika mno.
Hata amibadilisha IGP haitasaidia. Jk alikuja na saidi mwema lakini bado Hali ilikua mbaya, akatafuta IGP mwingine Ernest mangu bado hali mbaya.

Magufuli akambadilisha mangu na kumweka sirro, bado hali ilikua mbaya.

Labda ufukuze polisi wote, kitu ambacho hakiwezekani
 
Aliyejinyoga alipewa ukweli na muhusika na ukute alikuwa hajui chochote ,sasa akwapigia wahusika kuwajulisha ndo wakamfanya kitu kibaya marehemu ,sasa huyu anayesemekana kajinyonga ukute kauawa na wenzie ili wamuangushie zigo kuwa yeye ndo alimpokea hawajui alikompeleka mpaka kakutwa maiti.

Sent from my TECNO CF7 using JamiiForums mobile app
 
IGP abwage manyanga, hii Ngoma aliyowafundisha na kuwazoeza vijana wake, sasa haiwezi. Aliwalaumu wazazi wa Hamza kuwa hawakumfunza vizuri mtoto wao, Kwa uoza huu na mingine iliyotokea, hapo ni Nani hakumfunza vizuri mwanae?
Mi huwa najiuliza ni nn haswa hawa polisi hufundishwa wanapokuwa chuoni? Mambo wanayofanyaga huwezi watofautisha na majambawazi!.. hata mahita aliwai kuwa boss wa polisi!
Kama wanafundishwa vzr wale wema wanashindwaje kuwabaini polisi ambao niwahalifu?

Kama wanawaficha mapolisi ambao ni wahalifu na kuwatetea ina maana polisi wote ni wahalifu waliorasimishwa! Mfno wa matukio kama la mwangosi, lisu nk..

Kabla siro hajawasema wazazi wengine kuzaa watoto wa hovyo, angetuonyesha ubora wa watoto wake.

Huyu mzee kaxhokaa, sijui kama atachukua hatua yeyote ya maana kwenye tukio hili.
 
Aliyejinyoga alipewa ukweli na muhusika na ukute alikuwa hajui chochote ,sasa akwapigia wahusika kuwajulisha ndo wakamfanya kitu kibaya marehemu ,sasa huyu anayesemekana kajinyonga ukute kauawa na wenzie ili wamuangushie zigo kuwa yeye ndo alimpokea hawajui alikompeleka mpaka kakutwa maiti.

Sent from my TECNO CF7 using JamiiForums mobile app
Ukisoma vizuri hapo juu ni kwamba huyo Grayson nae alihusika
 
Watafurahi labda wakituua watanzania wote wabaki police wenyewe nchi nzima
 
IGP Sirro atoe ufafanuzi, kati ya wazazi wa Hamza na wazazi wa hao askari wake, ni nani wa hovyo?
 
Huu hapa ndio ujumbe uliosambazwa mitandaoni

Hizi_kesi_za_kuchonga_wanapewa_wengi_sana_kuonewa._Serikali_dhalimu_hizi_zinapaswa_kuondolewa_...jpg

===
Mjomba wa aliyeuawa adai alitishiwa kupewa kesi ya ugaidi

Akizungumza na waandishi wa habari jana mkoani hapa, mjomba wa marehemu, Salum Ng’ombo, alidai Januari 5, mwaka huu, alimsindikiza mwanawe Kituo cha Polisi Wilaya ya Mtwara baada ya kuelezwa akachukue vifaa vyake.

Hata hivyo, alidai alimtahadharisha wafuatane wasije wakampa fedha bandia na kumfungulia kesi nyingine.

Alidai walipofika kituoni walikutana na askari aliyejitambulisha kwa jina la Grayson, na kumueleza kuwa anamkabidhi mwanawe na kumuomba ahakikishe anarudishiwa vifaa vyake ikiwa ni pamoja na fedha alizokuwa akidai.

“Gryason ninamfahamu alipokuja nikamkabidhi mwanangu akiwa na barua ya mwanasheria baada ya kuona hiyo barua aliwasiliana na mwenziwe na kumwambia kuna barua kutoka kwa mwanasheria wa serikali inataka kijana arudishiwe mali zake,” alidai Ng’ombo.

Alisema baada ya muda kijana wake alifikishwa katika chumba cha mahojiano na alikaa kwa zaidi ya saa mbili hali iliyompa wasiwasi na kuamua kwenda kuangalia kinachoendelea.

Alisema alipofika kwenye chumba hicho alimkuta mjomba wake akiwa amekalishwa chini hali iliyomfanya ahoji kinachoendelea wakati aliitwa kwa ajili ya kuchukua mali yake.

Vile vile, alidai siku hiyo hiyo saa nane mchana alirudi kituoni na kuomba ampatie chakula ndugu yake, lakini hakufanikiwa na badala yake akaambiwa na mkuu wa upelezi wilaya kuwa aondoke eneo hilo vinginevyo atapewa kesi ya ugaidi.

Ng’ombo alidai siku ya pili alipata taarifa kuwa kuna mtu ameuawa na hakutilia maanani kama ni mjombake, hadi Januari 7, alipoenda kwa Mkuu wa Upelezi mkoa kwa ajili ya kufungua faili la kumtafuta nduguye pamoja na mali zake.

Alisema akiwa kwa RCO, wakati anatoa maelezo na mama wa marehemu, wakaelezwa kuwa suala hilo limehusisha mpaka ofisi ya mwanasheria wa mkoa kwa na kwamba kutakuwa na tatizo na kuombwa wavute subira lifuatiliwe.

Mama Musa

Mama wa Musa, Hawa Bakari, akizungumza nyumbani kwa ndugu zake, alisema kama sheria ingefuatwa kwa wakati mwanawe asingefia mikononi mwa polisi.

Alisema kwa mara ya kwanza polisi walipofika katika kijiji cha Luponda, Wilaya ya Nachingwea, walitaka waonyeshwe fedha zilipowekwa na kijana wake aliposita kuwaonyesha walimuelekezea bunduki.

Aliomba serikali isaidie haki kutendeka ikiwa ni pamoja na fedha za mtoto wake kurejeshwa.

IGP Sirro

Juzi Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mtwara, Mark Njera, akihojiwa na chombo kimoja cha habari aliahidi kulitolea ufafanuzi jana, hata hivyo ha kueleza chochote baada ya kuwa katika vikao na viongozi wa ngazi ya juu wa jeshi hilo wakiongozwa na IGP.

Kwa upande wake IGP Simon Sirro, alipoombwa na waandishi wa habari azungumzie tukio hilo, alieleza kuwa yupo na Waziri wa Mambo ya Ndani, Hamad Masauni na kwamba jambo lolote kwa wakati huo atalitolea ufafanuzi waziri huyo.
 
Haya ndio matumizi ya kesi za Ugaidi nchi Tanzania , Suala la Utakatishaji pesa wamelisimamisha kwa muda kutoka na nchi kukumbwa na umasikini wa kutisha

Suala sio nchi kukumbwa na umasikin ndo kupelekea polis kufanya ujambazi wa kupora Mali za raia ila imekuwa ni kawaida yao kufanya mauaji wakijua una pesa au madini. Wanatamaa ya fisi sanaaaa.

Rejea kesi ya Zombi Na wenzake wakati wanafanya mauaji ya wafanyabiashara wa Madini toka Mahenge, hicho nacho kilikuwa ni kipindi Cha nchi kukumbwa Na umasikini?
 
Ndo maana hamza ilikuwa anapiga askari tu raia anawaacha.
 
Back
Top Bottom