Mtwara: Wazazi wanawaficha watoto wenye VVU

Mtwara: Wazazi wanawaficha watoto wenye VVU

BARD AI

JF-Expert Member
Joined
Jul 24, 2018
Posts
3,591
Reaction score
8,826
Afisa Muuguzi Mwandamizi wa Hospitali ya Mangaka Wilaya ya Nanyumbu, Janeth Chikawe ameeleza kuwa Mkoa huo umekuwa na idadi kubwa ya wazazi ambao hawawapeleki watoto kupata dawa za kufubaza makali ya Virusi Vya Ukimwi kwa kuwafungia ndani.

Amesema watoto wengi wanaokosa huduma hiyo ni wenye umri chini ya miaka mitano ambao wazazi wengi hawataki watoto wajue hali zao kiafya jambo linalochangia ugumu katika utoaji wa elimu huduma muhimu.

Ametaja sababu nyingine kuwa ni wazazi kutowapeleka watoto Kliniki ili kujua maendeleo ya afya na ukuaji wa watoto.
 
Back
Top Bottom