Muafaka CCM na CUF, pande mbili za shilingi!

Muafaka CCM na CUF, pande mbili za shilingi!

Ras Nungwi,
mengi uliyo andika ni ukweli unaumiza hasa tunapokutana viongozi kama Maalim Seif. Huyu Seif aliwahi kuwa waziri kiongozi chini ya CCM na ni wakati huo Wa Unguja walikuja gundua kuwa alipeleka Wapemba wengi nje kusoma na kuboreshga Elimu Pemba kuliko hata Unguja.. Katika wakati wake wa Uongozi hakuna jema ambalo Wazanzibar hasa Wa Unguja, wanaweza kusimama kumpa sifa anazo stahili kama Waziri kiongozi. As a fact, kama sikosei alistaafishwa kiungwana..(naomba kusahihishwa)
Leo hii kwa bumbuazi gani walopigwa Wazanzibar hata kufikiria kuwa Huyu Maalim Seif anaweza leo kuleta changes akiwa nje ya chama tawala?...
Muafaka wa CCM na CUF ni kwa manufaa ya baadhi viongozi ambao wanataka nao kupata share ya ULAJI unaotokea. Karumes sasa hivi ni matajiri wakubwa, wana miliki kila kilichojengwa na marehemu baba yao kwa manufaa ya Taifa...Utajiri wa Zanzibar umekuwa mirathi yao pamoja na viongozi wengine, hivyo kama kweli CUF wana nia nzuri kwa nini wasianze na kupinga Ufisadi unaotendeka Zanzibar!..Hao kina Juma duni tunawasikia tu nje ya mabaraza lakini sijawahi kumsikia Maalim Seif wala kiongozi wa CUF akisimama bungeni ama nje kuelezea mabaya haya..
Kila siku tunachosikia wakisema ni kuhusu Muafaka, dhulma ya kura za wananchi, vifo vya wananchi wakati wa upigaji kura, Zanzibar ilivyoshamir wakati wa Sultan na kadhalika, halafu hawa hawa ndio tunawakuta wakila sahani moja na viongozi mafisadi.. Je, huu ndio mchezo mchafu wa siasa zetu!

Hivyo sii kazi ndogo kuweza kupata suluhu ya muafaka hasa ikizingatiwa kwamba Zanzibar nzima haina vyama viwili tu... Navyosikia mimi pendekezo kubwa la CUF ni kwamba ikiwa rais atatoka CCM basi waziri kiongozi lazima atoke CUF, hoja kama hii ina raise question toka vyama vinginevyo!..

Mwiba,
Unaposema mapinduzi yalikuwa haramu kwa sababu hakuna maendeleo ni matusi makubwa kwa wananchi wa Zanzibar.. nilisha kwambia kwamba kabla ya mapinduzi pamoja na ushindi wa chama cha Hizbu, Sultan alikabidiwa nchi kama mtawala.. WHY?.. Je, wananchi waliambiwa kuwa hizbu ikishinda Sultan atarudishwa!...na kulikuwepo na haja gani ya kumrudisha Sultan..
Mkuu acha Upemba kutazama upande mmoja tu wa shilingi, sioni kabisa sababu ya kupindisha maneno ya Nungwi ambaye kisha sema tujadili Upande wa pili wa shilingi..Na ndio upande aliozungumzia kama una hoja inayopingana nadhani utatusaidia sana kama utaizungumza tukotana na sura hii..
 
,sasa unataka kutwambia Juma Duni ni mwarabu ,Machano ni Mwarabu,Mloo umaarufu wanamwita kuchi ni Mwarabu ,yuko yule aliekuwa jaji mkuu nae ni mwarabu ,kama huwajui magogo wa Afro Shiraz basi itazame na ichambue CUF kwa kina utaona CCM kuna wapiga debe tu lakini hakuna Afroshirazi,Juma Duni mikono yake imejaa damu kwa kuilinda ASP ,ila watu hayo ndio wanayotaka kuyaweka kando na kuiweka Zanzibar mpya kila mmoja atabeba mzigo wake mwenyewe.
Juma Duni na Machano ni Watumbatu (Kaskazainin Unguja) Ali Haji Pandu-aliyekuwa Jaji (Mmakunduchi- Kusini Unguja) Mloo Mzanzibari mwenye asili ya Bara. Waliingia CUF kumfuata Seif, kwa sababu Duni (walifukuzwa pamoja-Godfather wake Seif) Ali Haji Pandu ( sababu ya urafiki)Mloo kaambiwa apumzike Mzee. Ali Haji Pandu katelekezwa hivi sasa, Duni na Machano wamepewa vilemba vya ukoka (wana vyeo lakini hawawashi hawazimi) Hiyo Ndiyo CUF wenyewe wanasemna ni ya Wapemba. Muunguja hana satuwa huko.
 
Wait and see. Chama cha mapinduzi kwa sasa kina udhaifu mkubwa, kwenye suala la muafaka kurudisha kwa wananchi ni kuchemsha, kwa mtu yeyote anayependa madaraka huwa hakubali ku-share madaraka, lakini kama ku-share madaraka kuna manufaa ya taifa kunatakiwa kufanyike bila mtu au kundi fulani kupenda!

Muafaka Zanzibar ni must, delay tactics zinaiumiza Zanzibar kwa ujumla.
Unapo-dakhil mambo usiwe na papara ndugu yangu. yasome kwa utuo ili uyasarifu vizuri. CCM haijasema haitaki Serikali ya kuchanganyika (iite mseto au shirikishi au upendavyo). Lakini inachosisitiza ni huo mchanganyiko usifanyike kiholela. Kwani tunataka mchanganyiko madhubuti ambao hautaiingiliwa na ile michezo (mnayoita ya kisanii). Nimesoma watu wameshadidia kuwaita CCM wasanii. Lakini mimi kwa mtizamo na uchambuzi wangu CUF ndio wasanii wakubwa (wamezidi kete). Muangalieni vizuri Seif Sharif Hamad na wapambe wake wakuu. Huo ndio upande wa pili wa shilingi.
 
Ahsante Ras-Nungwi kwa maelezo yako ya kina na yenye manufaa kwa wasomaji juu ya siasa za Zanzibar.

Hakika mimi sijaishi Unguja wa Pemba bali mara kadhaa nimekuwa nikisafiri kwenda Unguja na Pemba kwa shughuli mbalimbali. Nimepata bahati ya kufika vijijini kabisa na kufanya kazi na wananchi wa maeneo mengi. Nakubaliana na wewe kabisa kuna miendelezo mikubwa ya kimatabaka kadri unavyowafikia watu wa kawaida. Kwa hiyo kiongozi yeyote anayehubiri jukwaani utengano wa Wazanzibar basi nadhani hawatakii mema wananchi walio wengi hususan wale ambao wanaishi katika maisha ya ufukara kule vijijini. Sikuwepo wakati wa utawala wa KiSultan huko Zanzibar, lakini ukiangalia maisha ya leo ya kimatabaka kule visiwani unajaribu kupiga picha je ilikuwaje wa kati wa kipindi cha Usultani? ni wazi kuwa madhila makubwa yalikuwa yanawapata wananchi wenyewe asili ya kiafrika.

Mimi binafsi simwoni Maalim Seif kama ni kiongozi anaefaa kwa wakati huu kwa vile amekuwa ni kiongozi mwenye malengo ya kuingia madarakani kwa ajili ya ku-serve maslahi ya kundi maalum nalo ni Wapemba. Hii ni hulka mbaya sana ni hulka ya kisultan, yaani unawa-brainwash watu ili waweze kukuabudu na hakuna mtu yeyote anayerusiwa kumpinga Maalim kwenye jambo lolote (hata Lipumba). Analoamua Maalim ndiyo final, hii mbaya sana na ndiyo sababu nasema kuwa Maalim hafai kuwa Kiongozi kwa wakati huu.

Ukiangalia kwa undani yatokanayo na kauli za CUF baada ya Kikao cha CCM-NEC kule Butiama ni misimmamo binafsi ya Maalim Seif na wala si vinginevyo. Laiti kama angesema anakubaliana na kura ya maoni, basi CUF wote wangekuwa wanaongea kukubali kura ya maoni.

Kutokana na sera zake za kugawa watu, leo hii tunashuhudia cirle isiyo rasmi ndani ya CUF, kuna inner circle ambayo hiyo Mwenyekiti wa CUF anaetambuliwa na kuendesha vikao ni Maalim Seif, hii circle inawajumuisha wale watokao Pemba tu, na circle nyingine ni ile ya Mwenyekiti Lipumba. Lakini hadi leo sijaskia mtu yeyote akimhoji Seif juu ya hili.
 
CCM mtajaribu sana kumgeuza Seif kuwa monster lakini ukweli utabaki palepale kuwa waliovunja makubaliano ya amani ni CCM na mkutano wao wa Butiama. Mambo yote yalikuwa yakiendelea vyema kabla ya mkutano wa BUtiama. Swali kubwa ni kuwa, what happened in BUtiama?
 
1. Sitapenda kujadili historia ya Zanzibar, asili ya mtanziko wa kisiasa huko; lakini mimi naomba nichangia suala la principle tu hapa- kwamba pande mbili zimekaa zimajadiliana na kukubaliana mambo Fulani Fulani; baadaye upande mmoja umeanza kwenda tofauti. It’s a political problem, that needs a political solution.
2. Nimesoma neno kwa neno rasimu ya makubaliano ya CUF na CCM ambayo ilishakubaliwa na kamati zote mbili. Suala la serikali ya pamoja linapaswa kutekelezwa kabla ya mwaka 2010.
3. Nimesoma ripoti ya Kamati ya CCM iliyopeleka Butiama kwa ajili ya Kamati Kuu na baadaye halmashauri Kuu; ukweli ni kuwa hoja ya kura ya maoni haikuzuka kikaoni- iliandaliwa kabla kwa pendekezo la Karume na kukubaliwa na wanakamati. Pamoja na uzuri wa dhana ya kura za maoni, lakini nia(motive) yake hapa si nzuri! Kwa serikali ambayo haifanyagi referendum katika masuala muhimu kihistoria kama Muungano, Katiba, Mfumo wa Vyama vingi, kumuundoa Rais wa Zanzibar kama makamu wa Rais(ambalo lilikuwa ni suala katika makubaliano mama ya muungano); inatia shaka serikali kama hiyo itakapo suala la kura za maoni Zanzibar. Ni Kikwete huyu huyu ambaye alipokwenda Kenya hakutaka wakina Raila na Kibaki wafanye kura za maoni, akata wasaini makubaliano na kuyatekeleza. Wakati wa kuibwa kwa kura hakuitishwa kura za maoni, kosa moja haliwezi kuhalalisha kosa, lakini kosa moja linaweza kutoa ishara ya kosa lingine! Kwa ujumla ukiisoma ripoti hii ya Kamati ya CCM; ukisoma na Barua ya Mwisho ya Makamba; utagundua kuwa Makamu Mwenyekiti Msekwa na Mwenyekiti wa CCM, Rais Kikwete- hawakusema kweli wakati wakieleza mchakato wa Maazimio ya NEC ya CCM na Matokeo yake!
4. Nilikuwepo Diamond Jubilee jana na nimemsikiliza Lipumba toka mwanzo mpaka mwisho. Nilichokielewa ni kwamba CCM imekuwa ikiwatapeli CUF toka baada ya uchaguzi, ikiwafanyia unafiki wa hali ya juu- CUF nayo kwa upande wake ilikuwabali ku-give in too much; ikakubali ghilba za aina zote ikiwa na matumaini makubwa kwamba Kikwete yuko genuine! Na kwa kiasi kikubwa mambo yote haya yalifanyika kwa siri ya pande mbili; kwa mategemeo makubwa ya CUF kwamba pengine serikali ya mseto ingetokea. Kumbe CCM wakati wote ilikuwa ikiweka kadi chache mezani na nyingine nyingi zaidi kuzificha chini ya meza.Ukiangalia mtiririko wa matukio katika hii miaka mitatu kuhusu Zanzibar utagundua ama Rais Kikwete anafanya unafiki wa hali ya juu wa kisiasa, au ni kiongozi dhaifu katika CCM kama mwenyekiti anayezidiwa nguvu na makundi mengine ndani ya chama chake. Kwa vyovyote vile, hali hii ikiachwa bila panga kuitwa panga na si kisu kikubwa ni ishara mbaya kwa utangamano wetu kama taifa haswa kwa kuwa kwa sasa CCM ndicho chama tawala!
5. Tunaungana mkono na CUF katika hili, kwani kitisho cha demokrasia mahali Fulani ni kitisho cha demokrasia mahali pote. Maandamano ya jumamosi, hayapaswi kuwa maandamano ya CUF, yanapaswa kuwa maandamano ya umma! Ama hakika, uwongo una mwisho- lakini ukweli unapaswa husimama milele, na ukweli hauna itikadi. CUF wanaweza kuwa walijikwaa mahali Fulani katika mchakato huu; lakini sasa ni wakati wa kutazama mbali zaidi, kutazama picha kubwa zaidi- CCM ikiwachwa ikapita katika hili, itandelea kuacha na ufisadi mwingine ukatawala kwenye RICHMOND, BOT nk na hatimaye kuweka misingi ya ufisadi wa kudumu zaidi katika uchaguzi mkuu 2010. Hatupaswi kuacha utadamuni wa ufisadi, usanii wa kisiasa, uchezeaji wa haki, na wananchi kukaaa pembeni kama watazamaji na wanyooshaji vidole kuendelea katika taifa letu. Ni wakati mwingine wa kuandelea kuchukua hatua!
JJ

PS:
• Mwenye Hotuba ya Jana ya Lipumba atuwekee hapa tafadhali
• Mwenye rasimu ya makubaliano ya CUF na CCM iliyokubaliwa na kamati za pande mbili aiweke hapa pia tafadhali
 
Juma Duni na Machano ni Watumbatu (Kaskazainin Unguja) Ali Haji Pandu-aliyekuwa Jaji (Mmakunduchi- Kusini Unguja) Mloo Mzanzibari mwenye asili ya Bara. Waliingia CUF kumfuata Seif, kwa sababu Duni (walifukuzwa pamoja-Godfather wake Seif) Ali Haji Pandu ( sababu ya urafiki)Mloo kaambiwa apumzike Mzee. Ali Haji Pandu katelekezwa hivi sasa, Duni na Machano wamepewa vilemba vya ukoka (wana vyeo lakini hawawashi hawazimi) Hiyo Ndiyo CUF wenyewe wanasemna ni ya Wapemba. Muunguja hana satuwa huko.

Umejitahidi kujenga hoja ya kuonyesha kuwa CUF ni ya wapemba. Lakini ukiangalia majina ya watu unaowahusisha na kukataliwa kukubalika ndani ya CUF, baadhi yao waliwahi pia kuwa CCM. Imeelezwa huko nyuma pia kuwa hata maalim Seif naye alikuwa CCM na mtu mmoja akahoji anawezaje leo kuleta mabadiliko wakati alishindwa kufanya hivyio akiwa ndani ya CCM, tena akiwa na madaraka makubwa tu.
Je, kuna uwezekano kuwa hao CCM na CUF lao moja? Kwamba kwa upande wa Bara viongozi wameungana kuifisadi nchi kwa namna ambayo wanajua wenyewe (wizi na ubadhirifu mkubwa mkubwa). Na ninaposema viongozi kumbuka naamanisha viongozi wa pande zote, serikalini na kwenye vyama vyote).
Ninaanza kupata hisia kuwa hata visiwani nako, viongozi (wa pande zote) nao wameungana na kuna aina fulani ya ufisadi wanaoufanya ambao wananchi bado hawajaushtukia.
Inakuwa kama wamepangana kuwa wewe piga huku, ikilia wananchi watakimbilia kuja kuangalia, wakatyi wanashangaa hayo, mimi nitapiga huku na watakimbilia pia kuja kusikiliza, wakati wananchi wanahangaika kufuata milio, viongozi wanajilia vyao taratibu bila wananchi kwua na habari.
Hwa wote asili yao ni CCM, chama amabcho kinatuhumiwa kwa kila aina ya ufisadi, nadhani wengine wameamua kuingia upinzani kama kivuli cha kuficha ufisadi huo huo unaomuumiza mwananchi wa kawaida.
 
Haya matatizo ya Zanzibar Ni uroho wa madaraka na kutokua na dhamira njema kwa wananchi pia kwa nchi.

Ndio maana utaona focus zao zote za watu wasio na nia njema hua wakati wa uchaguzi tu,watatumia gharama/maisha ya watu ili tu wapate njia ya kutekeleza nia yao mbaya.

Suluhu ya Zanzibar ni Rahisi mno ila kwa vile wote watafuta madaraka na wasivyo na nia ya nchi yao na wananchi wao bali mabwana wao watafanya kila hila kuwatumia wananchi ili wafikie malengo yao.

CUF na CCM kama wanania njema kwa nchi na wazanzibari ,mimi nafikiri wangekubaliana hivi ktk muafaka wao-
wabadirishe kifungu ktk katiba ya ZANZIBAR na MAWAZIRI wateuliwe kutoka wananchi wakawaida wasiwe WABUNGE(WAWAKIRISHI),nusu watoke pemba na nusu watoke ugunja.
Hapo ukisikia watu wanauliwa ama wanaandamana kwa ajiri ya CUF ama kutembelea ulaya wanashitakiana basi tatizo litakua sio siasa.
Kwanini CUF hawataki kupropose njia hii?? Kwani mpaka CUF iingie madarakani ndio matatizo ya Pemba yataisha????
 
Haya matatizo ya Zanzibar Ni uroho wa madaraka na kutokua na dhamira njema kwa wananchi pia kwa nchi.

Uliyoyasema ni sehemu ya ukweli. Matatizo ya Z'bar yanakwenda zaidi ya hapo. Ni tatizo la kihistoria zaidi. Mbaya zaidi wapo watu ambao wanaifuata hiyo historia bila kujua ukweli wake ukoje. Wengi wa wanaharakati za sasa ni vijana ambao walizaliwa baada ya mapinduzi na wengine baada ya Muungano. yaliyotokea nyuma ya hapo wanasimuliwa tu, lakini kutokana na uhafidhina, wametiwa sumu kiasi kwamba wanajiona kana kwamba na wao walikuwepo wakati huo
 
Hakuna makelele wala mivutano kama CCM wanasema wao ni wengi hapo Unguja na CUF hawana ubavu wa kuwatoa kapa ,basi yanini mivutano na majigambo kuunda makamati tume miafaka na sasa maoni hii ni kuharibu fedha ni aina fulani ya ufisadi,kama ukweli unaweza kupatikana basi uchaguzi wa Zanzibar usimamiwe na vyombo vya kimataifa kama ilivyofanyika Zaire ulinzi na usalama na uratibu wote ulifanywa na vyombo vya kimataifa hii itajulikana au utajulikana kama uchaguzi wa knockout,lala salama.
Ila ukiwafikisha katika kauli ya uchaguzi usimamiwe na vyombo vya kimataifa ,CCM wataruka kama moshi na usiwajue wamekwenda wapi maana ni jambo ambalo wanaliogopa kama maradhi yanayouwa.
Leo hii Raisi wa Muungano akiamua kusimamia kikweli na kutaka kulimaliza jambo hili aruhusu usimamizi wa kimataifa,Kama Raisi anazo nguvu za kuweza kusema kama raisi wa Tanzania naamini kabisa hakuna chama kitakachoweza kupinga kama Raisi Kikwete akiamua kufanya kweli liwalo na liwe tuwaone hao akina Karume walithubutu kuwapia CCM bara ikiwa wataupitisha mseto basi warudishiwe ASP....hivi ni kweli maneno haya ya Jeuri yalitamkwa mbele ya NEC ,huu ni ubabe ulio wazi kusema kama hamtafanya hivi basi turudishieni ASP ni dharau ya hali ya juu kuweza kufanywa na CCM Zanzibar hapa inaonyesha wazi kuwa kwenyewe nani ya CCM hakuna umoja wa kweli.
Inanifanya sasa nione kuna miungano ya Tanzania na CCM mambo manne hayo (Zanzibar na Tanganyika ,TANU na ASP ),weka kiporo hilo.
Nikirudi kwenye ukweli ni kuwa Wahafidhina wa CCM Zanzibar hawana sapoti ya wananchi na ndio maana ukiwatajia kuwa uchaguzi usimamiwe na UN ili kuona nani ni mshindi ,jamani mechi ya CCM na CUF Zanzibar ni kali na kwa mantiki hiyo haihitaji refarii wa ndani lazima Refarii watoke UN ili kuona mechi inachezeshwa kwa kiwango cha kimataifa ambacho kila upande itabidi uwe na wachezaji waliojizatiti kwa wapenzi wao kuwa ushindi utapatikana kwa fair play ,hivo tukishindwa basi ni kweli tumeshindwa.
Mambo ya kusema tutashughulikia wenyewe hayana dhamana na ndio kila siku upande mmoja unasema umeonewa ,sasa wale wanaoonekana kuonea kwa nini nao wasikubali awekwe msimamizi wa Kimataifa je ushindi wao ni wa kweli ?? Je CCM mpo tayari ??Yaani CUF ukiwatajia hili basi watakwambia na kama fedha haitoshi wataongezea ,CCM mpo wacheni kubabaisha watu ,ukweli ni uchaguzi kusimamiwa na UN ,hapo ndio watu watajua kama embe ni tunda.
 
CCM mtajaribu sana kumgeuza Seif kuwa monster lakini ukweli utabaki palepale kuwa waliovunja makubaliano ya amani ni CCM na mkutano wao wa Butiama. Mambo yote yalikuwa yakiendelea vyema kabla ya mkutano wa BUtiama. Swali kubwa ni kuwa, what happened in BUtiama?

Nimesoma post nyingi katika thread na nikiangalia wengi wanaenda nje ya hoja ya kutokutekelezwa Muafaka - kuna wanaotaja viongozi wa CUF wasiokuwa Wapemba na mimi nawaongezeeni orodha kuwa kuna Jussa, Dedes,Bimani,Dr.Muchi na wengineo, kuna wanaosema Maalim Seif ni mbaguzi na kutaja ubaguzi wa Elimu alipokuwa Waziri wa Wizara hiyo , ndugu zangu mbona hamsemi wakati ambapo uchaguzi wa wanafunzi kuendelea na sekondari ulifanywa kwa kuangalia nywele za mtu, rangi na asili yake, alichokuja kufanya Maalim ni kurekebisha hayo na mukitaka musitake Wapemba wanapenda kusoma kwani wanajua ndio njia moja itayowanyanyua kimaisha kwa vile hawana mamlaka ya kufaidi Mapinduzi baada ya kuondoka yeye yamerudi yale yale naende mtu yeyote akafanye utafiti mdogo wa wanafunzi walioko vyuo vya kati au vikuu wanaopata nafasi kupitia SMZ na ataoana ni wapemba wangapi wamo vyuoni. Hayo ni madogo tu kama kuna kuzungumzia ubaya na udhalilishaji wa Wapemba angalieni matokeo ya watu kupigwa, kubakwa knajisiwa, kuharibiwa mali zao kutiwa vilema vya milele na Serikali ya CCM.

Hayo yote hayana msingi katika hoja ya kwa nini Muafaka haukufikiwa kwani inaonekana vyama hivi viwili viliingia katika mazungumzo ili kuondoa hali ilokuwepo na wengi tulifurahi tukadhani angalau nchi itakuwa na amani lakini inaonekana CCM haikujua nini inakitaka katika mazungumzo yale na kama alivyosma Mnyika kuwa sababu ilotolewa ingawa inaonekana ni ya kipimo cha juu cha demokrasia lakini haina nia nzuri kutokana na uzoefu wa CCM kuwa ndumilakuwili.

Sasa Rss Nungwi na wenzako wanaokuunga mkono kama unaona huo ubinafsi wa Maalim Seif kuwa ni sababu tosha ya kuyavuruga makubaliano ya Muafaka basi natutulie na tuangalie matokeo yake.
 
J.J Mnyika,
Mkuu umesema umezisoma hizo rasimu ya makubaliano kati ya CUF na CCM, kwa nini wewe usiiweke hapa...
Navyofahamu mimi ni kwamba makubaliano ya rasimu hizo yalikuwa yamepitiwa na kamati za pande mbili ambazo baada ya makubaliano yao zilitakiwa kuwakilishwa kamati kuu ya vyama vyote viwili -KUPITISHWA, ili kila upande upate kuangalia na kuchanganua kabla ya kuweka mkataba..
.
Hivyo yawezekana JK na Makamba waliziona poa lakini ilipofikia Kamati kuu ya Chama chao yalikutwa mapungufu fulani, mapungufu ambayo yalipowakilishwa CUF kufanyiwa marekebisho yalikataliwa..Muhimu kama alivyosema Mwafrika wa kike, mabli na kujiuliza kilitokea nini huko Butiama nadhani pia tunangalie ni mapendekezo gani yalitolewa na CUF... haiwezekani watu wawili JK na Makamba wapitishe muafaka unaosimamia uongozi wa nchi nzima na hasa swala la Rais wa Zanzibar na makamu rais wa Muungano..besides sidhani kama ni busara kuamua muafaka unaohusu nafasi hizo toka vyama viwili tu, what if kesho wakishinda chama kingine na hawataki utaratibu uliopitishwa na CCM na CUF..

Mimi binafsi kutokana na upeo wangu mdogo ktk siasa zetu, nina wasiwasi mkubwa na mabadiliko ya aina yoyote ktk tawala zetu ikiwa wananchi wenyewe wamegawanyika.. Leo hii tunayaona Zimbabwe, wengine wameisha sahau yanayotokea Somalia kwa sababu hizo hizo za siasa za Kiafrika ambazo badala ya kujenga taifa moja mara nyingi hutugawa mafungu.
Sijaona hata siku moja vyama vyetu vikisimamia maslahi ya wananchi wote zaidi ya kuwa vyama vyetu hismamia kundi fulani la watu, jambo ambalo tumeanza kulijengea ukuta wa Demokrasia...Hivyo basi badala ya mwananchi kutazama chama kama ni mwongozo wa wananchi wote mpiga kura hujitazama yeye yupo fungu gani...na kibaya zaidi ni kwamba hadi leo hii CCM wanacheza na karata kubwa mkononi kama chama kinachosimamia wananchi wote!..na kama Mugabe hutumia weak point zinazomvuta mwananchi na hasa maskini (Asilimia 80), hivyo inapofikia checking time CCM huangusha dume!..

Bi kirembwe,
Mimi nimezungumzia elimu kwa mapana zaidi ya kusema nani anapenda kusoma.... unajua nashindwa kabisa kuelewa mtazamo wa bnaadhi ya watu, serikali na hasa viongozi wanaposema kabila ama rangi fulani wanapenda kusoma, wakati wale wanyonge wanaosemekana hawapendi kusoma hawana hata shule moja!...Hawa watasoma wapi ikiwa hawana shule kama zilivyo upande wa pili!
Hizi hesabu zenu huwa mnazikusanya vipi! zamani tuliambiwa kuwa sijui Wahaya waliendelea kwa sababu walipenda kusoma lakini ukija tazama hesabu ya shule kati yake na mkoa mwingine mathlan Mara utashindwa kuelewa hizi hesabu zimetokana na kitu gani..Mara ilikuwa na shule chache mara tatu (kama sio zaidi) ya mkoa wa Kagera, walimu wengi kwa watoto wachache kuliko mkoa wa Mara na kadhalika..lakini bado watasema Wajita walikuwa hawapendi shule ndio maana hawana elimu!
Hizi ndio sababu huzungumziwa na hata wazungu wanaposema watu weusi hatupendi kusoma wakati hakuna uuwiano wa shule na walimu kati yetu na wao acha mbali kabisa na hizo standard.
Kibaya zaidi kwa Unguja ndani ya Uongozi wa Maalim Seif ni kwamba Unguja yenye population kubwa zaidi ya Pemba ndio ilipewa nafasi chache za kusoma tofauti kabisa na bara ambako unaweza sema population ya Kagera ilikuwa kubwa kuliko Mara hivyo kuhalalisha wingi wa shule mkoani humo na pengine kupata hesabu zaidi wa wanafunzi kuliko Mara..

Hata hivyo inabidi niachie hapa maanake haya maswala ni marefu zaidi hayana mwisho!
 
CCM mtajaribu sana kumgeuza Seif kuwa monster lakini ukweli utabaki palepale kuwa waliovunja makubaliano ya amani ni CCM na mkutano wao wa Butiama. Mambo yote yalikuwa yakiendelea vyema kabla ya mkutano wa BUtiama. Swali kubwa ni kuwa, what happened in BUtiama?

Hivi haya yote yanasemwa ili ku justify mambo ya CCM kule Butiana ama inakuwaje tena ?
 
Lunyungu,
Hivi haya yote yanasemwa ili ku justify mambo ya CCM kule Butiana ama inakuwaje tena ?
Bila shaka...hata mapendekezo ya kamati ya Mwakyembe yalipelekwa Bungeni, now maamuzi yoyote yatakayo pitishwa na Bunge yanaweza kuwa na dosari ikiwa tutaelewa sababu za kile kilichopitishwa!..
What happened in Butiama ni muhimu zaidi tukifahamu kwanza kabla hatujanyoosha vidole vyetu.. tusifanye ushabiki wakati hatufahamu sababu zilizofanya kamati kuu ya CCM kukataa muafaka huo..Hata Bush hukataliwa baadhi ya mapendekezo yake pamoja na kwamba yanaweza kuwa na muafaka fulani..
 
Umejitahidi kujenga hoja ya kuonyesha kuwa CUF ni ya wapemba. Lakini ukiangalia majina ya watu unaowahusisha na kukataliwa kukubalika ndani ya CUF, baadhi yao waliwahi pia kuwa CCM. Imeelezwa huko nyuma pia kuwa hata maalim Seif naye alikuwa CCM na mtu mmoja akahoji anawezaje leo kuleta mabadiliko wakati alishindwa kufanya hivyio akiwa ndani ya CCM, tena akiwa na madaraka makubwa tu.
Je, kuna uwezekano kuwa hao CCM na CUF lao moja? Kwamba kwa upande wa Bara viongozi wameungana kuifisadi nchi kwa namna ambayo wanajua wenyewe (wizi na ubadhirifu mkubwa mkubwa). Na ninaposema viongozi kumbuka naamanisha viongozi wa pande zote, serikalini na kwenye vyama vyote).
Ninaanza kupata hisia kuwa hata visiwani nako, viongozi (wa pande zote) nao wameungana na kuna aina fulani ya ufisadi wanaoufanya ambao wananchi bado hawajaushtukia.
Inakuwa kama wamepangana kuwa wewe piga huku, ikilia wananchi watakimbilia kuja kuangalia, wakatyi wanashangaa hayo, mimi nitapiga huku na watakimbilia pia kuja kusikiliza, wakati wananchi wanahangaika kufuata milio, viongozi wanajilia vyao taratibu bila wananchi kwua na habari.
Hwa wote asili yao ni CCM, chama amabcho kinatuhumiwa kwa kila aina ya ufisadi, nadhani wengine wameamua kuingia upinzani kama kivuli cha kuficha ufisadi huo huo unaomuumiza mwananchi wa kawaida.

Ah maoni yako It is food for thought. Ukweli ni kwamba wananchi wa kawaida wamechoshwa na hali hiyo inayoendelea huko (wote wa Pemba na wa Unguja, wanaoshabikia CCM na wanaoshabikia CUF)Wamo tu katika ugomvi huu wa kutengenezwa. Ukisikia wanashabikia ni frustrations tu hizo.Lakini kila mtu anaona enough is enough..
 
J.J Mnyika,
Mkuu umesema umezisoma hizo rasimu ya makubaliano kati ya CUF na CCM, kwa nini wewe usiiweke hapa...
Navyofahamu mimi ni kwamba makubaliano ya rasimu hizo yalikuwa yamepitiwa na kamati za pande mbili ambazo baada ya makubaliano yao zilitakiwa kuwakilishwa kamati kuu ya vyama vyote viwili -KUPITISHWA, ili kila upande upate kuangalia na kuchanganua kabla ya kuweka mkataba..
.
Hivyo yawezekana JK na Makamba waliziona poa lakini ilipofikia Kamati kuu ya Chama chao yalikutwa mapungufu fulani, mapungufu ambayo yalipowakilishwa CUF kufanyiwa marekebisho yalikataliwa..Muhimu kama alivyosema Mwafrika wa kike, mabli na kujiuliza kilitokea nini huko Butiama nadhani pia tunangalie ni mapendekezo gani yalitolewa na CUF... haiwezekani watu wawili JK na Makamba wapitishe muafaka unaosimamia uongozi wa nchi nzima na hasa swala la Rais wa Zanzibar na makamu rais wa Muungano..besides sidhani kama ni busara kuamua muafaka unaohusu nafasi hizo toka vyama viwili tu, what if kesho wakishinda chama kingine na hawataki utaratibu uliopitishwa na CCM na CUF..

Mimi binafsi kutokana na upeo wangu mdogo ktk siasa zetu, nina wasiwasi mkubwa na mabadiliko ya aina yoyote ktk tawala zetu ikiwa wananchi wenyewe wamegawanyika.. Leo hii tunayaona Zimbabwe, wengine wameisha sahau yanayotokea Somalia kwa sababu hizo hizo za siasa za Kiafrika ambazo badala ya kujenga taifa moja mara nyingi hutugawa mafungu.
Sijaona hata siku moja vyama vyetu vikisimamia maslahi ya wananchi wote zaidi ya kuwa vyama vyetu hismamia kundi fulani la watu, jambo ambalo tumeanza kulijengea ukuta wa Demokrasia...Hivyo basi badala ya mwananchi kutazama chama kama ni mwongozo wa wananchi wote mpiga kura hujitazama yeye yupo fungu gani...na kibaya zaidi ni kwamba hadi leo hii CCM wanacheza na karata kubwa mkononi kama chama kinachosimamia wananchi wote!..na kama Mugabe hutumia weak point zinazomvuta mwananchi na hasa maskini (Asilimia 80), hivyo inapofikia checking time CCM huangusha dume!..

Bi kirembwe,
Mimi nimezungumzia elimu kwa mapana zaidi ya kusema nani anapenda kusoma.... unajua nashindwa kabisa kuelewa mtazamo wa bnaadhi ya watu, serikali na hasa viongozi wanaposema kabila ama rangi fulani wanapenda kusoma, wakati wale wanyonge wanaosemekana hawapendi kusoma hawana hata shule moja!...Hawa watasoma wapi ikiwa hawana shule kama zilivyo upande wa pili!
Hizi hesabu zenu huwa mnazikusanya vipi! zamani tuliambiwa kuwa sijui Wahaya waliendelea kwa sababu walipenda kusoma lakini ukija tazama hesabu ya shule kati yake na mkoa mwingine mathlan Mara utashindwa kuelewa hizi hesabu zimetokana na kitu gani..Mara ilikuwa na shule chache mara tatu (kama sio zaidi) ya mkoa wa Kagera, walimu wengi kwa watoto wachache kuliko mkoa wa Mara na kadhalika..lakini bado watasema Wajita walikuwa hawapendi shule ndio maana hawana elimu!
Hizi ndio sababu huzungumziwa na hata wazungu wanaposema watu weusi hatupendi kusoma wakati hakuna uuwiano wa shule na walimu kati yetu na wao acha mbali kabisa na hizo standard.
Kibaya zaidi kwa Unguja ndani ya Uongozi wa Maalim Seif ni kwamba Unguja yenye population kubwa zaidi ya Pemba ndio ilipewa nafasi chache za kusoma tofauti kabisa na bara ambako unaweza sema population ya Kagera ilikuwa kubwa kuliko Mara hivyo kuhalalisha wingi wa shule mkoani humo na pengine kupata hesabu zaidi wa wanafunzi kuliko Mara..

Hata hivyo inabidi niachie hapa maanake haya maswala ni marefu zaidi hayana mwisho!

Kaka Mkandara

Sina soft copy, nina hard copies ndio maana nimeshindwa kuweka. Makubaliano hayo ya CUF na CCM kimsingi baada ya kusainiwa wananchi wanaweza kushirikishwa bado kwani lazima yapitie kwenye baraza la wawakilishi ambacho ndio chombo cha wawakilishi wa wananchi. Na kama yatahitaji mabadiliko makubwa ya muundo wa serikali ni wazi yanapaswa kushirikisha umma katika mchakato wa mabadiliko ya katiba. Sasa swali la kujiuliza; kura ya sasa ya maoni ni ya nini? Ni ya kwenda kuuliza ridhaa ya wananchi kama makubaliano yasainiwe au yasisainiwe? Wakati mwafaka wa kuwashirikisha wananchi si kabla ya makubaliano kusainiwa(kwa maoni yangu). Suala la makubaliano kusainiwa ni swala la pande mbili zizilizomo kwenye majadiliano- CUF na CCM. Ikifika sasa kubadili katiba ili makubaliano ya pande fulani- hata kama ingekuwa ni chamba embe na chama ndizi; hapo ndipo linapokuwa suala la umma wote. Ni kweli swala la Zanzibar ni zaidi ya CUF na CCM; nimekuwa nikisisitiza hivyo wakati wote, ndio maana kuna haja ya serikali ya umoja wa kitaifa.

Ama kuhusu historia uliyoitoa- sina sababu ya kuipinga wala kuikataa; ninachoweza kusema tu ni kwamba I reserve my comment!

JJ

Ps: Hapa ni suala la Principle tu- vyama viwili vimejifungia vimekubaliana mambo fulani fulani; mwingine anatoka na kuchukua uamuzi tofauti; nani anapaswa kuwajibika?

Ukisoma minutes za vikao vya kamati hizo unaona kwamba walishakubaliana misingi toka mwanzo; na kila hatua vikao vya juu vya vyama hivyo vilikuwa vikipewa mrejesho. Why about turn at the last minute on the part of CCM?

I agree that referundum is one of the cardinal democratic tool when it comes to engaging the populace; but CCM has an ill motive- if the end justify the means then the end defies the means as well. Since CCM's end is dragging time, events and in the process drifting the agenda; their referundum leaves much to be desired! Its a public opium..
 
J.J Mnyika,
Nipo nawe mkuu sasa tazama jibu la swali lako kuhusu maamuzi ya kamati kuu ya CCM lipo ktk usemi wako mwenyewe...nitanukuu hapa chini..

" Makubaliano hayo ya CUF na CCM kimsingi baada ya kusainiwa wananchi wanaweza kushirikishwa bado kwani lazima yapitie kwenye baraza la wawakilishi ambacho ndio chombo cha wawakilishi wa wananchi. Na kama yatahitaji mabadiliko makubwa ya muundo wa serikali ni wazi yanapaswa kushirikisha umma katika mchakato wa mabadiliko ya katiba.".

Nadhani ndicho walichokifanya CCM... Hapa hatufahamu kilichoshindikana kuweka muafaka lakini uataratibu wa kuwapelekea wawakilishi wa wananchi -Wana CCM, umefanyika na ndiko muafaka huo umekataliwa!..
 
Sicho walichokifanya CCM; kabla ya kukubali au kukataa kwa kina na kusaini au kukataa kusaini makubalino ya pande mbili kati ya CUF na CCM; CCM wameamua kwenda kwanza kukusanya maoni ya wananchi wote ikiwemo wanaCHADEMA, na wasio na vyama huko Zanzibar. Huku ni kukwepa wajibu wa kuamua ama ni kuhamisha mzigo wa lawama. Trust me; this guys are looking for an excuse and an escape route! Ndio maana ilo wazo la referundum katika nyaraka yao waliyowasilisha kamati kuu na baadaye NEC utaona wameliita kabisa ubunifu wa kuwapiku CUF- sasa kama wameliita hili wazo hivi unaweza kuniambia haswa nia yao nini nini? Hebu kasome kwenye qurani ile aya inayozungumzia wanafiki unikumbushe tabia tatu za mnafiki- akisema anadanganya; akiahidi hatekelezi; akiaminiwa haaminiki!

Kabla ya kupeleka kwa umma wa watanzania; CCM waweke kwanza makubaliano ya pande mbili kati ya CCM na CUF- halafu sisi watanzania ndio tuletewe tuyajadili hayo makubaliano yao; short of that- CCM has no political will to find a solution to Zanzibar impasse. Wanafanya jig saw tu yenye vipande ambavyo wanajua kabisa havijakamilika; mwisho wa siku picha haitakamilika. Na wanatafuta sababu ya picha kuvurugika kabla vipande havijaisha ili wasijulikane kwamba vipande viko pungufu

JJ
 
Mnyika jaribu kuondoa ukamarade wenu na CUF katika hili. Kama ni suala la kukosa/kuvunja "Good will" kati yao nani alianza? Sio CUF walivyoripuka kusheherekea ushindi/kulazimisha ushindi wakati wakijua wazi ASP/CCM Unguja walikuwa wanapinga. Baada ya matamshi ya Seif ilitegemea nini kutoka kwa "wakorofi" wa Zanzibar. Yaani mlitegemea wakubali kilaini hali ya kwamba hiyo ingeonyesha kuwa wao ni dhaifu na wameshindwa....

Na hili suala la ninyi kushabikia huu ujinga wa CUF na CCM kujifanya Zanzibar ni wao na si wengine linatoka wapi?

Kingine, huu ni muafaka wa CCM na CUF, sasa iweje now ndio watake kuwahusisha watanzania/wazanzibari? Nadhani huu ndio ulipaswa kuwa msimamo wenu na sio kufumba macho ujanja wa wenzenu CUF?

Tanzanianjema
 
Tanzania Njema

Nikiangalia tarehe za matamshi ya CUF baada ya Kikao cha Baraza Kuu lao na Tarehe kamati ya CCM ilipokamilisha kazi yake. Ina nipa picha ya haraka kwamba walichokifanya CUF ni pre emptive strategy. Walishajua kabla ya kikao cha butiama kwamba CCM inakwenda kuwacheza shere. Kwamba hao wahaifidhina walishashinda kabla kwa Karume 'kuishinikiza' kamati iweke wazo lake la kura za maoni kwenye ripoti yao. Hivyo, njia pekee ya kisiasa ilikuwa ni kuanika makubaliano yalivyo kabla ya kikao cha Butiama- ili umma ujue kabla nini ambacho CCM ilipaswa kubariki Butiama; pengine Mwenyekiti Kikwete aingilie kati kurudi katika mstari. Lakini ambacho CUF walikuwa hawakijui ni kuwa CCM lao moja; na wala hawasukumwi kwa njia kama hizo. Kwao CCM, lililoandikwa-limeandikwa!

Swala liwe la CCM na CUF au vipi mimi si la muhimu sana; la muhimu zaidi ni kuwa kitisho kwa demokrasia mahali pa moja ni kitosha cha demokrasia mahali pote. CCM kama chama tawala ikiachwa ikafanya usanii wa kisiasa katika hili itaendelea kufanya usanii wa kisiasa hata katika masuala ya ufisadi wa BOT, Richmond na mingineyo. Justice ni justice, iwe ya CUF au ya shetani- ni justice tu. Na wazanzibar wakiacha justice ikachezewa katika suala kama hili la kisiasa itakuwaje kuhusu justice katika maisha yao ya kila siku?

Sina nia ya kufungua pandora box ya Zanzibar ila kwa maoni yangu anayekwenda kufanya refurundum ndio anayefungua box la uchaguzi tena kabla ya majeraha ya awali kuweza kutibiwa; ni kutia chumvi katika kidonda.

Unakumbuka Vuguvugu la Chungwa kule kenya wakati wa mjadala wa Katiba? Itakuwaje vuguvugu kama lile likifanyika Zanzibar wakati wa kura za maoni? Litakuwa tofauti gani na kampeni za uchaguzi Mkuu? Tofauti yake ni kwamba; hilo litakuwa ni uchaguzi wenye chuki ya kuibiwa uchaguzi mwingine. Ni kama leo Kibaki aamue kuitisha kura za moani kule Kenya kuuliza kama waunde serikali ya mseto au nini? Wakati akipita kuuliza swali hilo atakutana na swali lingine la kwanini yuko ikulu wakati ameiba kura? Sasa ni heri tu wananchi waulize swali hilo kwa heri; wakiuliza kwa shari matokeo yake unayajua- ni VURUGU!

Ama kama wazanzibar na wazanzibara miaka yote hiyo tumewaacha CUF na CCM wajifungie wenyewe- leo tusilalame kuhusu hili; inamaana kuna waliokuwa na imani na mazungumzo hayo kuwa yatazaa suluhu. Kama dalili za suluhu zimezaliwa kwa rasimu ya makubaliano; basi ni wajibu wa wote kuoana hao wenye makubaliano wanakubaliana kabla ya kuyaleta kwetu; kama kuna yoyote kati yao anakenda kinyume basi ni wajibu wa wote kusema. Kwa kuwa mwisho wasiku ya kuibuka ya kuibuka haisemwi kwamba ni CUF au CCM wako ukimbizini- ni Watanzania ndio waliokuwa pale Shimoni. Sasa kwanini ukombozi tunauvika itikadi? Au ndio divide and rule?

JJ
 
Back
Top Bottom