Wakuu kuna mahali nadai senti zangu sasa asubuhi nilitaarifiwa kwamba wametuma muamala kutoka akaunti yao ya CRDB kuja akaunti yangu ya NBC. Nimepita mchana kwa wakala pesa haijaingia. Nikapiga customer care NBC wakasema muamala haujawasili. Namuuliza mdada wa customer care kwa kawaida inachukua muda gani ananijibu inategemea imetumwa kwa njia gani. Sikumuelewa. Kule ninakodai nimeshindwa kumpata hewani mchana huu. Mwenye uzoefu na transactions kutoka CRDB kwenda NBC anijuze hutumia muda gani. Shukran.