Kiranga
Platinum Member
- Jan 29, 2009
- 89,019
- 156,726
Senator Jeanne Shaheen wa Marekani (New Hampshire, D) ana nia ya kupeleka hoja kwenye bunge la Senate la Marekani akisema kuwa chama tawala cha Tanzania CCM kimehatarisha usalama wa raia wa Tanzania na watalii na kuiba kura, na hivyo baada ya wizi huu wa kura, na mauaji hayo, uhusiano wa Tanzania na Marekani ni lazima uangaliwe upya.
Hiyo ni lugha ya kidiplomasia zaidi, lakini hapo maana yake viongozi wa Tanzania wanaweza kuwekewa vikwazo wasikanyage Marekani na mali zao zilizopo Marekani zikazuiwa. Inawezekana pia vikwazo zaidi vikawekwa na misaada inayowawezesha kufanya uhalifu wao ikazuiwa.
Hili ni jambo la muhimu, hata kama ni kwa kuongeza uelewa tu kuhusu mauaji yaliyotokea Tanzania.
Nawaomba Watanzania, hususan Watanzania-Wamarekani na Wakazi wa Kudumu wa Marekani wenye asili ya Tanzania, wamuandikie Senator Shaheen kumshukuru kwa kulivalia njuga hili na kumpa data zaidi.
Tunaweza pia kuwandikia ma Seneta wengine wa US Foreign Relations Committee HAPA Home | United States Senate Committee on Foreign Relations
On X see @SenatorShaheen
Ranking Member's Press | United States Senate Committee on Foreign Relations
United States Senate Committee on Foreign Relations
Contact her
Contact | U.S. Senator Jeanne Shaheen of New Hampshire
The Official U.S. Senate website of Senator Jeanne Shaheen of New Hampshire