Asante kwa maelezo murua mkuu.
Nina maswali mengine mawili naomba pia niulize;
1. Nina boxer Bm150 nyuma kwenye shock ups haigusi wala haigongi (iko comfortable) lakin nikipita kwenye bums (hasa nikipakia mtu) wakati wakunesa shock ups zinatoa kamlio flan hivi "kwich kwichi" kwa mbaali,, nilienda kwa fundi akaniwekea oil lakin bado inaendelea kutoa hako kamlio,, tatizo inaweza kuwa ni nin boss?
2. Pia kwenye hio boxer battery yake naona imechoka nimeshauriwa nikabadili maji ya battery,, naomba kufahamu ni kwa muda gani betri itakua na nguvu yakutosha ikiwa na maji mapya kabla yakubadili tena.
Nawasilisha