Muda hadi kukamilisha ujenzi (Msingi-Finishing)

Muda hadi kukamilisha ujenzi (Msingi-Finishing)

Northern Lights

JF-Expert Member
Joined
Sep 24, 2013
Posts
395
Reaction score
357
Habari za mchana wajenzi...
Napenda kufaham, ina chukua muda gani kujenga nyumba ya vyumba vitatu kutoka msingi hadi finishing? Hapa ninakuwa na pesa yote inayohitajika. Ni mtu ambaye nimeajiriwa kwa hiyo natafuta kuomba likizo ya siku 30 ili nisimamie shughuli yote ya ujenzi hadi ikamilike. Na kama haiwezekani kukamilisha kwa siku 30, naweza kufika hatua gani?
Note.. Hii ni nyumba yangu ya kwanza kujenga/kusimamia na eneo la ujenzi ni DSM

Asante kwa ushauri
 
Ukiwa na mafundi chapa kazi kweli kweli, ndani ya muda huo utakuwa umefanikiwa mpaka kuezeka
 
Hongera kwa hatua ndugu,sasa unaenda kuitwa baba mwenye nyumba.
Msingi ni siku 3
Boma siku 5
Renta siku 2
Hatua zote hapo juu hakikisha unamwagilia vyema.
Tofali za mwisho baada ya renta siku 1
Siku moja unapumzika.
Kuezeka siku 4 pamoja na blander ndani na nje.
Grill siku 1.
Mfumo wa umeme na maji siku 2
Plaster siku 5 nje ndan
Skimming siku 2
Body siku 2.
Vigae siku 5,ila time flame yako itakuwa imeisha.
Vingine vinawezekana kufanyika wakati wa weekend kama fund umeme na maji kuja kumalizia kazi zao,rangi,viio na other decorations.
All the best.
 
Asante sana mkuu, kwa hiyo hamna haja ya kusubiri ikauke kwanza hata nikiunganisha hamna shida
 
Siku 30 HAZITOSHI, hata Kama una pesa yote.
Mchanganuo wangu upo hivi, Kama una mafundi wazuri na wapo makini;
  • Msingi siku 6(kuchimba na kumwaga zege chini siku 1, kujenga Msingi siku 2, na kupinga mkanda siku 1, siku 1 ni kumwagilia na kuacha mkanda kukomaa vizuri ili nyumba ije ikae juu, kujaza Mchanga ndani siku 1)
  • Nyumba siku 9(course ya kwanza hadi ya 11 siku 5, lintel siku 1, siku 1 ni kuacha ikauke vizuri, course 3 za juu ni siku 2)
  • Bati siku 6(siku 2 mbao, siku 3 bati na siku 1 blunder)
  • Grill siku 1. Ila unatakiwa kuanza kuandaa grill pindi unapomaliza boma.
  • Umeme/wiring siku 3
  • Plumbing siku 3
  • Plaster siku 5
  • Mkeka siku 1
  • Gypsum siku 3
  • Skimming siku 4(hapa ndio kuna uchawi, wafanya kwa utaratibu na umakini ili nyumba ije kuvutia, pia utaskim gypsum)
  • Tiles siku 3
  • Windows installation siku 1
  • Colouring siku 4(hapa pia Usiwe Sana na haraka, pia utapaka rangi gypsum)
  • usafi na kuweka sawa nyumba siku 1
N.b; kazi ya septic tanks ifanyike sambamba na wakati wa kujenga boma, gawanya mafundi wengine wachimba shimo na kuanza kulijengea huku wengine wakiendelea na boma.
Hadi hapo ni siku 50, na kumbuka hapo watu lazima wawe wengi kidogo. Na hapo ni kazi inaenda haraka sana.
Nakusisitiza hapo Ni endapo una mafundi wengi na wapo speed na wapo makini.
Ukisema utumie chini ya siku 50 Kuna sehemu utakuja kulia.
Wanaokuambia siku 30 zinatosha ni waongo wakubwa Sana.
Nimekushauri nikiwa Kama mtaalam mbobezi wa masuala ya ujenzi na pia ni civil contractor.
 
Itategemea idadi ya mafundi,vibarua, na vitendea kazi walivyonavyo.mfano; watu 10 watamaliza kulima ekari moja ya shamba kwa siku 1,lakini watu 2 watamaliza kulima shamba hilo kwa siku 25
 
Habari za mchana wajenzi...
Napenda kufaham, ina chukua muda gani kujenga nyumba ya vyumba vitatu kutoka msingi hadi finishing? Hapa ninakuwa na pesa yote inayohitajika. Ni mtu ambaye nimeajiriwa kwa hiyo natafuta kuomba likizo ya siku 30 ili nisimamie shughuli yote ya ujenzi hadi ikamilike. Na kama haiwezekani kukamilisha kwa siku 30, naweza kufika hatua gani?
Note.. Hii ni nyumba yangu ya kwanza kujenga/kusimamia na eneo la ujenzi ni DSM

Asante kwa ushauri
Siku 30 nyingi sana kama upo na pesa ya kutosha
 
Hapo inategemea vipimo vya grill za dirisha na milango zitapatikana lini na fundi ataweza kukamilisha kwa muda gani.

Inakuja kwenye bati kupata running meter ili upate idadi ya bati zitakazotumika uweke order kiwandsai/ kwa wakala waanze kukuandalia order yako. Vinginevyo ukanunue yale mabati ya kawaida uunge.

Hivyo ni vitu ambavyo vinakua nje ya muda unaoutaka wewe.

Kama walivyoeleza wengine, itategemea sana na idadi ya mafundi ulionao. Ila kuna baadhi ya kazi zinategemeana, lazima ikamilike moja ndio ifanyike nyingine.

Siku 30 zinaweza isiwe ni kadirio zuri kwa ubora wa nyumba.
 
Hapo inategemea vipimo vya grill za dirisha na milango zitapatikana lini na fundi ataweza kukamilisha kwa muda gani.

Inakuja kwenye bati kupata running meter ili upate idadi ya bati zitakazotumika uweke order kiwandsni/ kwa wakala waanze kukuandalia order yako. Vinginevyo ukanunue yale mabati ya kawaida uunge.

Hivyo ni vitu ambavyo vinakua nje ya muda unaoutaka wewe.

Kama walivyoeleza wengine, itategemea sana na idadi ya mafundi ulionao. Ila kuna baadhi ya kazi zinategemeana, lazima ikamilike moja ndio ifanyike nyingine.

Siku 30 zinaweza isiwe ni kadirio zuri kwa ubora wa nyumba.
Asante kwa ushauri mkuu, njia mbadala nayoona hapa ni kupandisha boma kwanza na kuezeka halaf natulia tena hata miezi sita
 
Siku 30 ni chache,, kwa maana kwenye ujenzi kuna vitu vingi huwa haviendi kwa muda unaotaka wewe...Na kuna vingine pesa inamaliza kwa haraka zaidi..

Ila Nafikiri miezi miwili inatosha sana kumaliza ujenzi wa nyumba yote.
 
Unataka hoja gani? Soma comment yangu hapo juu nimeeleza kila kitu.
Mkuu kwenye comment yako hapo juu umeainisha shughuli husika na siku utakazotumia kuikamilisha hiyo kazi ...swali ni kuhusu nguvu kazi, je hayo makadirio yako ya idadi ya siku yapo na mafundi na watenda kazi kiasi gani?je kama utaongeza nguvu kazi utaokoa muda kiasi gani?
 
Hapo nimeweka maximum ya hiyo nguvu kazi. Huwezi kuweka mafundi 100 kwenye nyumba moja (practically haiwezekani)
 
Back
Top Bottom