Muda ndio umemchagua Benzema aonekane Straika Bora mbele ya Luis Suarez lakini takwimu zinamkataa

Naomba kujua market value ya Benzema na Suarez tufunge uzi
Umekuja na kitu kingine kabisa ambacho hakiingii hapa mkuu.
Yani uulize Market Value ya saiv ya
Ronaldo na Kane?
Yani Ronaldo kashazeeka vile ana staafa unauliza market value unataka ku compare na mtu anaecheza kama Kane?
Ndio hicho kwa Benzema na Suarez.
Suarez katoka Lini Ulaya?
Leo unataka kuulizia Market Value dhidi Ya mtu alietoka Juzi Ulaya?
 
Nimeuliza ivo kwa kuwa luis suarez na KB9 wote ni wazaliwa wa mwaka 1987 nataka tuanzie hapo na wote wanecheza soka la ulaya mashindano ya club ulaya na ligi ya uhispania.
Nikukumbushe tuu UMRI WA MODRIC na umri wa iniesta ni sawa kabisa.
 
U
Meishasema muda, basi zama ziheshimiwe.
 

Km KB9 asingekubali kucheza nyuma ya CR7
Huenda hzo takwimu zingekuwa tofauti
 
Benzema ni false nine meanwhile suarez ni natural nine.
Mbingu na ardhi unajaribu kuzilinganisha mkuuu.
Kama KB9 angeamua kusimama kama natural nine pasi angemuacha suarez mbali sana.
Umeandika vitu vya ajabu tu sijui haujawai watazama!! suarez na benzema hawatofautiani uchezaji wao wote wanaweza kucheza kutokea pembeni, wanaweza kucheza nyuma ya mshambuliaji wa mwisho na pia wote wanaweza kucheza striker wa mwisho namba 9.

Mambo ya false nine ni uongo, benzema hajawai kucheza false nine hapo real Madrid, benzema amekuwa akicheza namba 9 yenyewe hapo Madrid.

Suarez anamzidi benzema kila kitu hasa ukatili kwenye box la adui suarez ni king'ang'anizi ni mbishi na msumbufu sana.

Wote wanaweza kutokea pembeni na kufunga hapa wanalingana, ila wote wakiwa kwenye form zao suarez anaanza mbele ya benzema
 
Ni kweli kabisa suarez ni msumbufu sana na king'ang'anizi ndani ya box kuliko benzema
 



Kila mmoja ana mataji mangapi na mataji yepi?

Hiyo pia ni kigezo.
 
Usisahau Ajax Amsterdam alipoanzia soka lake la ulaya kila msimu ALIKUWA anapiga 30-35goals kwa misimu mitatu mfululizo ndio Liverpool wakamsajili
[emoji3][emoji3][emoji3] sasa unaanza kutupanga mkuu, Suarez alipokuwa Ajax ni msimu mmoja tu ndio alifika goli 35 na katika msimu huo alifunga Jumla ya magoli 49 Katika mashindano yote,

Sasa mkuu hizo habari za kusema misimu mitatu mfululizo jamaa anatupia 30-35 goals umezitoa wapi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…