Muda tunaopoteza katika msururu/foleni za magari, Dar es Salaam

Poleni wandugu mlioko kwenye foleni. Hiyo ndio 'bongo flavour'
 
Yaani leo mjini kulikuwa ni majanga...mtu unatumia masaa mawili toka airport mpaka posta...
 
Kuna siku nilitembea kutoka Posta mpaka Moroko (Airtel). Jinsi siku zinavyozidi kwenda hali inazidi kuwa mbaya.
 
Mji huu haukuandaliwa kuhimili watu waliopo sasa na hata kuurekebisha ni gharama kubwa maana itabidi nyumba nyingi zivunjwe.
 
...pole sana!
Watanzania inabidi tuchukua hatua! tubadilike. Tunapoteza muda mwingi kwenye foleni!

...kuna umuhimu wa kuanza kutumia usafiri wa pikipiki na baiskeli...
 

Duh... Poleni sana, hamieni huku ushagooo!!!
 
Kwa mamlaka zanye utajiri wa akili.zilitakiwa kutoa vibari vya ujenzi nnje ya city cetre.
Kila siku majengo yanajengwa na barabara zinapanuliwa pia.lakin kasi ya majengo ni zaidi ya barabara.hivyo folen ni maisha ya kuyazoea.
 
...dawa ya foleni ni kujizoesha kutumia PIKIPIKI & BAISKELI...
 
Shughuli za serikali zote peleka Dom, pale Magogoni pawe nyumba ya makumbusho walau Dar itapumua huku ikibaki na biashara pamoja na bandari.
 
Hakuna ufumbuzi ila kurudisha UDA na Ikaruz zao. Hii ya kila mtu ana gari haina maana inafanya mji unakuwa wa kuchukia
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…