Muda tunaopoteza katika msururu/foleni za magari, Dar es Salaam

Muda tunaopoteza katika msururu/foleni za magari, Dar es Salaam

Toka saa 11 nipo hapa karume natoka maeneo ya kariakoo ila hii foleni sijawai kuiona kwa miaka yote nlo kaa hapa dar ni hatari magari hayaendi wala kuja..na ukiongezea hii mifumo ya kupeana likizo za bila mipango sijui kma matatizo kama haya yatakuja kua solved hapa nchini.
Poleni wandugu mlioko kwenye foleni. Hiyo ndio 'bongo flavour'
 
Yaani leo mjini kulikuwa ni majanga...mtu unatumia masaa mawili toka airport mpaka posta...
 
Kuna siku nilitembea kutoka Posta mpaka Moroko (Airtel). Jinsi siku zinavyozidi kwenda hali inazidi kuwa mbaya.
 
Mji huu haukuandaliwa kuhimili watu waliopo sasa na hata kuurekebisha ni gharama kubwa maana itabidi nyumba nyingi zivunjwe.
 
...pole sana!
Watanzania inabidi tuchukua hatua! tubadilike. Tunapoteza muda mwingi kwenye foleni!

...kuna umuhimu wa kuanza kutumia usafiri wa pikipiki na baiskeli...
 
Salaam wakuu.

Kwa wale wakazi wa Dar es Salaam, na maeneo ya jirani kwa leo(15.01.2014) tumeweza kushuhudia foleni ilivyoweza kuwa kubwa, kiasi kwamba barabara takribani zote toka asubuhi muda saa kumi na mbili na nusu hivi hadi muda huu, barabara zilikuwa "hazipitiki'..Sijajua kama ni "wikiendi" ndefu(kuambatana na mapumziko na siku kuu, au labda kufunguliwa kwa shule,n.k.

Lakini hii ikanifanya kutafakari muda tunaoupoteza tuwapo katika foleni. Mfano, iwapo mtu anapoteza masaa mawili(2) kwa siku yaani wastani wa masaa kumi kwa wiki, mtu huyu hupoteza masaa 500 kwa mwaka ambayo ni sawa na takribani siku 21(WIKI TATU).

Je, kwa wale wenye mizunguko zaidi, au wenye kupoteza masaa zaidi ya mawili kwa siku, muda huu tunautambua?
Kwa wale tulio/tunaoishi Dar es Salaam kwa miaka kadhaa tumepoteza miaka mingapi?

Duh... Poleni sana, hamieni huku ushagooo!!!
 
Kwa mamlaka zanye utajiri wa akili.zilitakiwa kutoa vibari vya ujenzi nnje ya city cetre.
Kila siku majengo yanajengwa na barabara zinapanuliwa pia.lakin kasi ya majengo ni zaidi ya barabara.hivyo folen ni maisha ya kuyazoea.
 
...dawa ya foleni ni kujizoesha kutumia PIKIPIKI & BAISKELI...
 
Shughuli za serikali zote peleka Dom, pale Magogoni pawe nyumba ya makumbusho walau Dar itapumua huku ikibaki na biashara pamoja na bandari.
 
Hakuna ufumbuzi ila kurudisha UDA na Ikaruz zao. Hii ya kila mtu ana gari haina maana inafanya mji unakuwa wa kuchukia
 
Back
Top Bottom