Muda tunaopoteza katika msururu/foleni za magari, Dar es Salaam

Muda tunaopoteza katika msururu/foleni za magari, Dar es Salaam

hippocratessocrates

JF-Expert Member
Joined
Jul 1, 2012
Posts
3,598
Reaction score
1,544
Salaam wakuu.

Kwa wale wakazi wa Dar es Salaam, na maeneo ya jirani kwa leo(15.01.2014) tumeweza kushuhudia foleni ilivyoweza kuwa kubwa, kiasi kwamba barabara takribani zote toka asubuhi muda saa kumi na mbili na nusu hivi hadi muda huu, barabara zilikuwa "hazipitiki'..Sijajua kama ni "wikiendi" ndefu(kuambatana na mapumziko na siku kuu, au labda kufunguliwa kwa shule,n.k.

Lakini hii ikanifanya kutafakari muda tunaoupoteza tuwapo katika foleni. Mfano, iwapo mtu anapoteza masaa mawili(2) kwa siku yaani wastani wa masaa kumi kwa wiki, mtu huyu hupoteza masaa 500 kwa mwaka ambayo ni sawa na takribani siku 21(WIKI TATU).

Je, kwa wale wenye mizunguko zaidi, au wenye kupoteza masaa zaidi ya mawili kwa siku, muda huu tunautambua?

Kwa wale tulio/tunaoishi Dar es Salaam kwa miaka kadhaa tumepoteza miaka mingapi?
 
wamerudi..leo ofisi nyingi wameanza kazi zao baada ya likizo, asubuhi tatizo lilikua kubwa zaidi
 
dar es salaam leo imetisha. Si bure kutakua na mkono wa mtu. Duh!..
yaani mjini kati kila barabara imefunga.
Kwa leo panya road zinahusu zaidi.

Ngoja niagize helicopter yangu ile ninayoipark kwenye roof ya Holiday Inn ijekukuchukua...hebu nipe coordinates fasta.
 
Tangu nianze kufanya kibarua posta, leo nime experiance foleni kubwa sana. Najiuliza nini sababu?
 
Ngoja niagize helicopter yangu ile ninayoipark kwenye roof ya Holiday Inn ijekukuchukua...hebu nipe coordinates fasta.

Naamin bado unasikilizia kwenye foleni hapo red cross hahahaaaa....!!!
 
Tangu nianze kufanya kibarua posta, leo nime experiance foleni kubwa sana. Najiuliza nini sababu?
Umeanza lini mkuu? Anyway,ni barabara ipi? Muda fulani wa mchana nlipita barabara ya nyerere maeneo ya mbele ya quality plaza kuna daladala mbili zimegongana ... may be the cause
 
Ni OVERTIME ya kazi waajiri wa mafundi barabara hawataki kutoa kiasi cha kwamba sikukuu zote walikula sikukuu halafu leo mapema wameanza pale JMall ,na kule shoprite wanatandika rami ya kiufisadi kujustfy matumizi . Over
 
Toka saa 11 nipo hapa karume natoka maeneo ya kariakoo ila hii foleni sijawai kuiona kwa miaka yote nlo kaa hapa dar ni hatari magari hayaendi wala kuja..na ukiongezea hii mifumo ya kupeana likizo za bila mipango sijui kma matatizo kama haya yatakuja kua solved hapa nchini.
 
Leo saa sita mchana kulikuwa na foleni ndefu sana mfano kutoka Shaban Robert School hadi Kariakoo nilitumia saa nzima (dakika sitini).
 
Back
Top Bottom