Muda tunaopoteza katika msururu/foleni za magari, Dar es Salaam

Muda tunaopoteza katika msururu/foleni za magari, Dar es Salaam

Hapo tutafika soon!! Wanaanza Ubungo na Tazara, sasa hv wapo kwenye kipindi cha kuandaa michoro!!
Soon? ili tutoke Dar kwenda mikoani, hao wanaochora washauri wachore Ubungo iwe hivi.

 

Attachments

  • image.jpg
    image.jpg
    18.4 KB · Views: 163
kuna umuhimu wa kurudi kijijini sasa dar duuu
 
Waendeshaji magari wote Dar hawafuati sheria na hawana discipline barabarani. Kila mtu ana haraka. Kila mtu anatanua. Kila mtu anachomekea. Hata zijengwe flyovers kama za Texas ama beltways za DC hazitasaidia hadi watu wafuate sheria
 
Wafanyakazi wengi wanaokwenda posta/kariakoo hutumia karibia masaa 4 kwa siku kwenye foleni
 
Tangu nianze kufanya kibarua posta, leo nime experiance foleni kubwa sana. Najiuliza nini sababu?

Kwan mnacho ng'ang'ania hapo dar n nn utafkr hamna makwenu? kla m2 akaendeleze mji wao, karbuni morogoro mji kasoro foleni
 
Money Stunna...pole sana mkuu kwa foleni hiyo lakini nadhani hakuna means tena kwa sasa zaidi ya uvumilivu tu.
 
Last edited by a moderator:
nasemaaaaa tenaaaa siyo lazimaaaaa kila mtu awe anaenda na gari lake town paki home au liwache sehemu ukirudi lipitie fool stop......tumieni daladalaaaaaa ila kila mtu mbishi anataka aonekane na gari kazini au town tupande daladala tu .....tupunguze foleni
 
nasemaaaaa tenaaaa siyo lazimaaaaa kila mtu awe anaenda na gari lake town paki home au liwache sehemu ukirudi lipitie fool stop......tumieni daladalaaaaaa ila kila mtu mbishi anataka aonekane na gari kazini au town tupande daladala tu .....tupunguze foleni

Mkuu nadhani ulimaanisha FULL stop and not otherwise...lakini tatizo liko pale pale, Je, sehemu za maegesho ya magari(parking) zipo? kama zipo, zipo za kutosha? kama zipo za kutosha vipi gharama zake(kwa saa/siku)?
 
Mkuu nadhani ulimaanisha FULL stop and not otherwise...lakini tatizo liko pale pale, Je, sehemu za maegesho ya magari(parking) zipo? kama zipo, zipo za kutosha? kama zipo za kutosha vipi gharama zake(kwa saa/siku)?
acha gari lako sheli au sehemu ya usalama wape vojana 500 tu ilimradi sehemu iwe safe...nakubali hakuna sehemu ya maegesho maana nchI au serikalI hii hawajui kuplan mambo kama hayo...
 
acha gari lako sheli au sehemu ya usalama wape vojana 500 tu ilimradi sehemu iwe safe...nakubali hakuna sehemu ya maegesho maana nchI au serikalI hii hawajui kuplan mambo kama hayo...

Sasa issue inakuja ni sheli(Gas filling stations) gani na ngapi zitakuruhusu wewe kwa shida zako kuegesha gari pale, zitaruhusu magari mangapi? Then wapi ni sehemu ya usalama mfano hapa Dar Es Salaam?
 
Habarini,
Yaaani sikuamini,
Mi nimkazi wa Dar sawa, lakini nature ya kazi yangu na mahala nikaaapo huwa sikutani sana na haya niliyoyaona leo.
Nilikwenda mbezi ya kimara kulala huko na leo asubuhi nikasema "nirauke" asubuhi na mapemaaa ili niwahi nyumbani kwangu nikalale maana huko mbezi kulikua na shughuli flani.

Saa 11 asubuhi naingia barabarani kuelekea maeneo ya ubungo. Nimekutana na foleni ndefu sana.
Nikajiuliza hawa watu wanawahi makazini sawa. Lakini kazini unatakiwa uripoti labda saa mbili. Wewe unaamka kwako say saa10 alfajiri ili by saa 11 alfajir uwe barabarani.

Mwili wako unakua unafikiria na kufanya kazi jumla yamasaa 13. Yaani kuanzia saa 10 alfajir mpaka 11 Jioni.
Je utendaji wa kazi hapa kweli utakua wa ufanisi? Akili itakua active kweli kwa massaa yote haya? Adha yote ya nini hii? Dah!


Mkuu hii ndiyo 'Darisalama'.
 
hakuna kitu kinachonikera na kuniondolea furaha kama kero ya foleni hapa Dar.


Nawaza jinsi ninavyoamka saa 10 alfajiri na kufika posta saa mbili, ili niwahi kazini maana muhindi haelewi foleni wala nyanyaake miundombinu.

Nawaza hivi kwa miaka yote hiyo aliyokua waziri wa ujenzi kama alishindwa je akiwa raisi akipita na ving'ora itakuaje??

Sishawishiki kumpa kura yangu bora aiibe kutoka Chadema tar 25 oct.

Hahaha..Magufuli kazi anayo!
 
Wizara nyepesi kuliko zote kuziongoza na watu wakakukubali.

1)Ni wizara ambayo vitu vyake vinaonekana kwa macho ya kawaida(Tangible),haihitaji uwe msomi uone hili ni daraja.

2)Unapewa pesa kisha unatangaza tenda kuwa mwenye uwezo wa kufanya ujenzi fulani aje,uzuri ni kwa kuna utitiri wa makampuni ya ujenzi.

3) Matokeo yake huonekana kwa haraka kama lile jengo refu kuliko yote Africa Mahariki na Kati lililochukuwa miaka minne tu.

4) Sio watanzania wengi waliotembelea nchi za nje hivyo watu hawajilinganishi na nchi za nje kwa maendeleo yao ya barabara bali hujilinganisha na wao wenyewe walivyokuwa kabla.(Reference point)

Ila huwa ninashangaa kuwaona watu wanaotoka Kariakoo hadi Mwenge kwa saa 1 na nusu,umbali wa dakika 20 Bado wanasema huyu mtu ni jembe.

Kuna ukweli hapa.

Lakin maliasili,kilimo na maji nazo ni tangible au kwakuwa humkubali na humpendi basi hata lile jema linakuwa baya????

Kilimo, maji na Maliasili kote ni yale yale, ni aibu nchi inayozungukwa na maziwa, mito, bahari na tuna mibaraka ya mvua kuwa na tatizo la maji, haoa Dar Es Salaam yenyewe kuna shida ya maji unategemea nini?

Utalii na Maliasili ndiyo tabu kabisa hakuna lolote Tembo/Ndovu walimalizwa sasa wakahamia kwa Twiga wakiisha sijui wataenda wapi!

sirikambi, si suala la kumpenda ba kutompenda nani hapa kwenye barabara tusilete mchezo, ni vioja tupu.
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom