Muda umefika kukaa ukumbini kuangalia televisheni ni dalili za umasikini

Muda umefika kukaa ukumbini kuangalia televisheni ni dalili za umasikini

Webabu

JF-Expert Member
Joined
Apr 29, 2010
Posts
8,870
Reaction score
14,258
Historia ya upashanaji habari ni ndefu sana. Sitaki nianzie mbali sana. Kutokana na kasi ya maendeleo ya kielimu na ukuaji wa teknolojia tumeshuhudia kupungua kasi ya usomaji magazeti mpaka magazeti makubwa duniani ikabidi yapotee au kujibadili kuwa ya kielektonik.

Miaka si mingi sana na redio maarufu duniani nazo hazina wasikilizaji nazo zikajaribu kujiingiza kwenye mitandao na bado hazijasalimika na mabadiliko ya dunia.

Tangu kuwepo kwa televisheni na radio za mitandao ambazo zinaweza kusikika duniani kote na urahisi wa kila mtu kuanzisha ya kwake imekuwa shida sana kupata wasikilizaji. Imefika muda kila mtu anajisikiliza mwenyewe au na rafiki zake wachache.

Kwa pesa ambazo sio nyingi sana kila mmoja anaweza akaanzisha televisheni au redio yake baada ya kuuza machungwa na kujidanganya kuwa anasikika au kuangaliwa na ulimwengu mzima.

Wale ambao hawana televisheni na redio zao za mtandao utawakuta wamejiinamia au kujikushanya wakiangalia kitu kinaitwa clip ama za vichekesho au wafungaji magoli na kadhalika. Hawana muda kabisa na kuangalia hizi televisheni za taifa na za mashirika zinazotokea kwenye majengo maalumu ndani ya miji.

Tofauti na ilivyokuwa zamani ambapo video ilikuwa ni kitu cha kifakhari mpaka kila gari lilitangaza kuwa lina video ndani kuwavutia wasafiri.Ukifika majumbani unakuta televisheni na watu wanajikushanya kuangalia habari au vipindi vyengine muhimu.

Mambo ni tofauti kabisa miaka hii michache iliyopita.Unaweza ukawasha mitambo ya televisheni na kurusha matangazo maeneo ya karibu na kuunganisha na intaneti ukijidanganya kuwa unatazamwa na dunia nziam kumbe matangazo yenyewe yanapotea hewani bure na kuangaliwa na wachache sana.

Waangaliaji wa televisheni mara nyingi ni wageni kutoka shamba ambao wameingia mijini au wale wavivu ambao hawafanyi kazi au hawajapata kazi za kufanya.Hawa ni watazamaji ambao hawana faida sana kwa vituo vya televisheni.

Ukata wa wasikilizaji na watazamaji naamini umewakumba wote wanaomiliki vituo hivyo na hakuna wa kujidai mbele ya mwenzake. Mimi mwenyewe nilikuwa na cha kwangu nilipoona naangalia mwenyewe nikaamua kukifunga ili nisizidi kutumbukia kwenye umasikini.

Vituo vya televisheni vinavyopumulia mashine ni vile vinavyoonesha mechi za mipira tu na wengi wa waangaliaji huamua kujikushanya pamoja kwenye mabanda badla ya kukaa majumbani mwao.Hii nayo ni dalili ya ushamba na umasikini.
 
Historia ya upashanaji habari ni ndefu sana.Sitaki nianzie mbali sana.
Kutokana na kasi ya maendeleo ya kielimu na ukuaji wa teknolojia tumeshuhudia kupungua kasi ya usomaji magazeti mpaka magazetu makubwa duniani ikabidi yapotee au kujibadili kuwa ya kielektonik.
Miaka si mingi sana na reidio maarufu duniani nazo hazina wasikilizaji nazo zikajaribu kujiingiza kwenye mitandao na bado hazijasalimika na mabadiliko ya dunia.
Tangu kuwepo kwa televisheni na radio za mitandao ambazo zinaweza kusikika duniani kote na urahisi wa kila mtu kuanzisha ya kwake imekuwa shida sana kupata wasikilizaji.Imefika muda kila mtu anajisikiliza mwenyewe au na rafiki zake wachache.
Kwa pesa ambazo sio nyingi sana kila mmoja anaweza akaanzisha televisheni au redio yake baada ya kuuza machungwa na kujidanganya kuwa anasikika au kuangaliwa na ulimwengu mzima.
Wale ambao hawana televisheni na redio zao za mtandao utawakuta wamejiinamia au kujikushanya wakiangalia kitu kinaitwa clip ama za vichekesho au wafungaji magoli na kadhalika.Hawana muda kabisa na kuangalia hizi televisheni za taifa na za mashirika zinazotokea kwenye majengo maalumu ndani ya miji.
Tofauti na ilivyokuwa zamani ambapo video ilikuwa ni kitu cha kifakhari mpaka kila gari lilitangaza kuwa lina video ndani kuwavutia wasafiri.Ukifika majumbani unakuta televisheni na watu wanajikushanya kuangalia habari au vipindi vyengine muhimu.
Mambo ni tofauti kabisa miaka hii michache iliyopita.Unaweza ukawasha mitambo ya televisheni na kurusha matangazo maeneo ya karibu na kuunganisha na intaneti ukijidanganya kuwa unatazamwa na dunia nziam kumbe matangazo yenyewe yanapotea hewani bure na kuangaliwa na wachache sana.
Waangaliaji wa televisheni mara nyingi ni wageni kutoka shamba ambao wameingia mijini au wale wavivu ambao hawafanyi kazi au hawajapata kazi za kufanya.Hawa ni watazamaji ambao hawana faida sana kwa vituo vya televisheni.
Ukata wa wasikilizaji na watazamaji naamini umewakumba wote wanaomiliki vituo hivyo na hakuna wa kujidai mbele ya mwenzake.Mimi mwenyewe nilikuwa na cha kwangu nilipoona naangalia mwenyewe nikaamua kukifunga ili nisizidi kutumbukia kwenye umasikini.
Vituo vya televisheni vinavyopumulia mashine ni vile vinavyoonesha mechi za mipira tu na wengi wa waangaliaji huamua kujikushanya pamoja kwenye mabanda badla ya kukaa majumbani mwao.Hii nayo ni dalili ya ushamba na umasikini.
Eti unasema???
 
Mkuu TV,simu,Magari ni anasa zina kodi kubwa wacha tuendelee kukaa mabandani tu hakuna namna..maana kuangalia mpira kwa kutumia boss huku jamaa kajikunja na LG 65" ni bora nifate rangi huko mabandani isingekua anasa tungeangalia home tu..
 
Hivi wewe unaongelea nchi gani Marekani au hapa bongo? Hapa Tanzania kati ya kaya 1200 waliopo kwenye kijiji kaya 20 tu wana Tv,smart phone 100,Redio hapa kila kaya ina angalau karedio kadogo ka sola au betry 1,hizo ndoto zako labda kuanzia mwaka 2500
Kudhibitisha hilo angalia sensa ya watu na makazi 2022, usidanganye ,watu wengi sana wanasikiliza redio na kuangalia Tv,mfano kila ikifika saa 2 usiku watu hujikusanya baa na pub kuangalia taarifa ya habari
 
Mimi nashangaaga vimeza vya wauza magazeti! Kwa siku anaweza asiuze hata moja lakini bado anakomaa!
Anasubiri apige porojo na wale wanaokuja kuchungulia ukurasa wa mbele.Mara nyingi ni mashushu na hawanunui chochote halafu wanakwenda vijiwe vya kahawa
 
Sijasoma rhread yote ila aliyekwambia kuwa kuangalia tv kwenye kumbi tunafanya sisi tu Africa ni nani? Hata huku ughaibuni lounge kibao wazungu wanangalia mpira and etc sijui ushamba huu umeanzia wapi.
 
Ngoja nitoke church. Nikifika home navunja vunja TV zote ya chumbani kwangu na sebleni. Sitaki kuwa mshamba Mimi.
Usikaribishe umasikini nyumbani kwako.Baki na simu yako tu mpaka hapo baadae
 
Back
Top Bottom