Webabu
JF-Expert Member
- Apr 29, 2010
- 8,870
- 14,258
inachofanya Israel sasa kwenye jimbo la Gaza ni unyama ambao unapaswa kuzuiwa kivitendo na si kwa lawama za mdomo tu.
Kwa muda wote wa miezi 9 ya vita Israel imeachwa ifanye inavyopenda kwa watu wa Gaza.Wamehamishwa mara mia na sasa wamechoka na hata mikoba yao ya kuhama hama imewapotea.
Iwapo Israel inachotafuta haijakipata basi ni wakati wa kushikwa na kuambiwa inatosha na wacha.Ni kawaida ya binadamu kumzuia mtu katili anapoonekana anamuumiza mwengine kwa sababu yoyote ile.Hali ikifikia hapo huwa hatuanzi kuuliza nani mkosa bali tunazuia uovu na ukatili unaofanyika.
Hukumu za mahakama na lawama nyepesi hazina maana yoyote.Hata wale wanaojidai kuitambua Palestina hawajafanya lolote la maana kuwasaidia watu wa Gaza ambao hata sauti na machozi vimewakauka mwilini.
Bila kufanyika hivyo adhabu za kutoka kwa muumba tunaomba ziwashukie kila mmoja mwenye uwezo wa kuishika mkono Israel lakini amekaa kimya bila kufanya chochote cha maana.
Leo hii watu zaidi ya 70 wameuliwa eneo la Mawasi ambalo watu waliambiwa wakimbilie na ni sehemu salama.Watu na watoto wamebakia vipande vipande