Muda umefika nchi za kiislamu na dunia iiambie Israel wacha na inatosha

Muda umefika nchi za kiislamu na dunia iiambie Israel wacha na inatosha

Hatutapeliwi ukizunguka dunia ndio utajua kuna dini na utumwa. Waarabu wanakimbilia Ulaya na Marekani sio Dubai Wala Saudia. Nchi hii imeuzwa zaidi na wavaa makobazi kuanzia Mwinyi, Kikwete na Mama. Bugando na , KCMC imejengwa na waislamu ? Nitajie Hospitali au NGO kubwa ya waislamu au waarabu inayosaidia Tanzania. Amkeni aisee matajiri wenu wanawekeza kwenye mpira tu. Kuna Ka NGO kalikuwa kanalipia watu mahari na nyie mkapiga makofi juu 🤣🤣🤣🤣. Unafurahi kulipiwa mahari kama mahari unalipwa utaweza kumhudumia mke na watoto ? Aisee Tanzania tuna safari ndefu tumemuuzia Dubai bandari zote . Wakati Dubai hawana mafuta wanaendesha uchumi kwa kuikopa Abu Dhabi.
Unachotaka ni kipi kwani.
Unachozungumzia kuhusu bandari na Dubari ndio ushahidi kwanini wawekezaji kutoka nchi za kiarabu hawaonekani Tanzania.Nyinyi mna roho mbaya na uhasidi mkubwa kwa waislamu na mnatoa vipaumbele kwa wazungu japo mwisho wa yote huwa wanaleta ushoga.Mnaona bora huo ushoga kuliko kuachia pesa za waarabu zikawekezwa Tanzania.
Mitambo ya Dowans ilipomilikiwa na mwekezaji kutoka Oman ikazushiwa mengi na mwishowe iliponunuliwa na mmarekani ikatajwa haina tatizo lolote.
 
inachofanya Israel sasa kwenye jimbo la Gaza ni unyama ambao unapaswa kuzuiwa kivitendo na si kwa lawama za mdomo tu.

Kwa muda wote wa miezi 9 ya vita Israel imeachwa ifanye inavyopenda kwa watu wa Gaza.Wamehamishwa mara mia na sasa wamechoka na hata mikoba yao ya kuhama hama imewapotea.

Iwapo Israel inachotafuta haijakipata basi ni wakati wa kushikwa na kuambiwa inatosha na wacha.Ni kawaida ya binadamu kumzuia mtu katili anapoonekana anamuumiza mwengine kwa sababu yoyote ile.Hali ikifikia hapo huwa hatuanzi kuuliza nani mkosa bali tunazuia uovu na ukatili unaofanyika.

Hukumu za mahakama na lawama nyepesi hazina maana yoyote.Hata wale wanaojidai kuitambua Palestina hawajafanya lolote la maana kuwasaidia watu wa Gaza ambao hata sauti na machozi vimewakauka mwilini.
Bila kufanyika hivyo adhabu za kutoka kwa muumba tunaomba ziwashukie kila mmoja mwenye uwezo wa kuishika mkono Israel lakini amekaa kimya bila kufanya chochote cha maana.

Leo hii watu zaidi ya 70 wameuliwa eneo la Mawasi ambalo watu waliambiwa wakimbilie na ni sehemu salama.Watu na watoto wamebakia vipande vipande

An Israeli attack targeting the Hamas military commander kills at least 71 in southern Gaza

Sahihi kabisa. Lakini HAMAS siyo Palestine. Palestine wamefuga joka nyumbani kwao. Idi Amin alipotuchokoza tulimpiga mpaka akakimbilia Saudi Arabia alikofia na kuzikwa. Tusingemtoa hadithi ingekuwa ni nyingine leo hii. HAMAS wasirudie kuichokoza Israel. Palestine walifukuze joka walilofuga kutoka nyumbani kwao. Hiyo ndiyo itakuwa suluhu ya mambo yote.
 
Unachotaka ni kipi kwani.
Unachozungumzia kuhusu bandari na Dubari ndio ushahidi kwanini wawekezaji kutoka nchi za kiarabu hawaonekani Tanzania.Nyinyi mna roho mbaya na uhasidi mkubwa kwa waislamu na mnatoa vipaumbele kwa wazungu japo mwisho wa yote huwa wanaleta ushoga.Mnaona bora huo ushoga kuliko kuachia pesa za waarabu zikawekezwa Tanzania.
Mitambo ya Dowans ilipomilikiwa na mwekezaji kutoka Oman ikazushiwa mengi na mwishowe iliponunuliwa na mmarekani ikatajwa haina tatizo lolote.
Rafiki yangu nitajie kuna nini wamefanya waarabu Tanzania maana ukiangalia NGO zote kubwa zinafadhiliwa na wazungu Kuanzia Amref mpaka ICAP. Mwarabu amefanya nini ? leta ushahidi hapa unampa mtu miradi wakati hajafanya chochote ? Waarabu wakijitahidi sana mtaletewa maji ili mtawadhe misikitini hapo ndio mwisho wake. Nimekutana na wazungu wkatoliki huku ujerumani wanafadhili shule BUKOBA wanatuma euro 300 000 kila mwaka. Haujatembea tembea uone ndio utajua. Hiyo Serengeti tuliyowafukuza wamasai na kuwapa waarabu. Familia ya waren buffet na Frankfurt Zoology Society wamemwaga pesa za kutosha kuboresha uhifadhi. Mpaka Mchengerwa akakimbia na gari ambalo FZS waliwapa wizara ya utalii.
1721542661022.png
Leta NGO ya waarabu inayofanya makubwa Tanzania. Wao wenyewe wanabaguana wao kwa wao halafu waje watusaidie. kwenye nchi zao kuna watu wa tabaka lachini wanaoishi maisha ya tabu kushinda sisi. Waache kuwasaidia wao halafu ndio waje kutusaidia sisi ?
 
Saudi Arabia, UAE, Bahrain, Qatar, Jordan, Egypt na Morocco. Pia Oman na Algeria, zote zinaisaidia Israel wazi wazi au moja kwa moja au kupitia Marekani, Uingereza na nchi za NATO.

Uturuki wanafik, wanatangaza mengine wanatenda mengine.

Yemen, Syria, Iran, Lebanon na vikundi vya wapiganaji wa Iraq vinaiunga mkono Palestina bila unafik.

Sudan na Somalia wanawaunga mkono Palestina lakini wenyewe wana matatizo kwa sasa.

Kitaeleweka tu.
Mimi nakuuliza swali tu si mashindano. Je umesoma kwenye bibblia takatifu Mungu mwenyewe wa kweli amenena ukiibariki Israel na wewe UTABARIKIWA ukiilani Israel na wewe UTALAANIWA. Angalia hizo nchi za kiislamu zinazobariki Israel ulizozitaja zilivyo stable na uchumi mzuri. Na angalia hizo akina Iran.

GOD BLESS AND PROTECT ISRAEL

ISRAEL THE LAND JEWS THE PEOPLE
 
Na sisi Tanzania ni maskini kwasababu tumeilani israel au??? Au tumeibariki?

Hizi dini za kuletewa hizi zinashida sana, ndio maana nilishahacha kwenda kanisani kitambo tu, kwasasa nimekua neutral tu, sitaki dini yeyote, dini yangu ni (haki na kuishi maisha ya upendo kwa wote)
 
Nadhani pia muda umefika nchi za kiislamu zikubaliane kwamba ISRAEL asichokozwe kwa namna yoyote ile....
 
Mimi nakuuliza swali tu si mashindano. Je umesoma kwenye bibblia takatifu Mungu mwenyewe wa kweli amenena ukiibariki Israel na wewe UTABARIKIWA ukiilani Israel na wewe UTALAANIWA. Angalia hizo nchi za kiislamu zinazobariki Israel ulizozitaja zilivyo stable na uchumi mzuri. Na angalia hizo akina Iran.

GOD BLESS AND PROTECT ISRAEL

ISRAEL THE LAND JEWS THE PEOPLE
Wala usiwe na fikra za kubishana, tuelimishane tu.

Una uhakika upi biblia ni maneno ya Mungu?

Nakuuliza, maneno ya Mungu yanaweza kukinzana (contradictory)?
 
Saudi Arabia, UAE, Bahrain, Qatar, Jordan, Egypt na Morocco. Pia Oman na Algeria, zote zinaisaidia Israel wazi wazi au moja kwa moja au kupitia Marekani, Uingereza na nchi za NATO.

Uturuki wanafik, wanatangaza mengine wanatenda mengine.

Yemen, Syria, Iran, Lebanon na vikundi vya wapiganaji wa Iraq vinaiunga mkono Palestina bila unafik.

Sudan na Somalia wanawaunga mkono Palestina lakini wenyewe wana matatizo kwa sasa.

Kitaeleweka tu.
Yemen na Syria ziko kundi la Somalia
 
Back
Top Bottom