Mwl Athumani Ramadhani
JF-Expert Member
- Sep 10, 2022
- 1,280
- 2,522
WAKUU
Nianze KWA kunukuu
"Kule kwenye miradi ya maendeleo waliachiwa wanasiasa"
Hii ni kauli ya mwandishi ninaye mhusudu Sana HAPA jukwaani,kwamba miradi mingi Sana HAPA nchini inasimamiwa na wanasiasa walioshinda chaguzi zao tangu tupate uhuru,lakini hadi leo bado kuna kizungumkuti Sana Katika utoaji wa huduma KWA jamii HASA elimu,maji,umeme,AFYA,pembejeo za kilimo na huduma nyinginezo.
Ipo haja ya dola kutoishia tu kwenye ulinzi na USALAMA wa nchi badala yake kusimamia miradi ya maendeleo nchini,angalau nina imani dola ipo makini kuliko wanasiasa walioshinda chaguzi kwani wameshindwa kabisa kufikia matazamio ya wananchi Katika huduma za msingi,leo wananchi wanalilia maji,umeme, AFYA, pembejeo za kilimo na mengineyo kana kwamba tumepata uhuru juzi MWAKA 2002 kumbe ni zaidi ya miaka 45 iliyopita!
Sasa kuendelea kujikita kwenye usalama pekee bila KUJALI hao mnaowalinda wanapataje huduma za kulindwa huko au kulindwa huko kuna tija kiasi Gani kwao bila huduma ni kukwepa majukumu yenu na kufanya nusu jukumu!Ni sawa na Mimi Baba kuilisha tu familia bila kuwapatia malazi na mavazi wala elimu Watoto huko ni kukwepa majukumu yenu ya msingi KWA Taifa hili.
Kuendelea KWA vilio KUHUSU huduma za kijamii HAPA nchini ni kiashiria kuwa Mliowapa majukumu wameshindwa na wanahitaji msaada kutoka kwenu!
Nawaomba muingilie jukumu hili zito KWA mstakabali wa Taifa letu hili.
Nina imani Bandiko langu mtalisoma na Sasa mtaanza kuhoji hao Mliowapa majukumu kwanini hiki kipo hivi au kipo vile na tumewapa Mamlaka KWA Muda mrefu nao wasiwape majibu ya kisiasa ya majukwaaani kama hayo tunayoyapata KILA siku!
Mungu ibariki Tanzania yetu
Asanteni KWA kusoma