Kile KICHWA alicho piga alitakiwa awepo mtu afanye cover....!!!
Kwenye mpira timu Ina jikinda kwa kanuni beki akikaba au kucheza mpira ana takiwa awepo mtu wa kucover hiyo nafasi Kisha ana kuwepo mtu mwingine wa kutengeneza balance.
Sasa kwa mantinki hii Che Malone alicheza mpira kwa KICHWA je nani alikwenda cover kwa mshambuliaji?
Swali langu nani alikwenda kucheza drop ball Baada ya KICHWA Cha Che Malone ? Balance nani alifanya.
Karibu tujadili kiufundi ndugu yangu.
Hoja ya tackle ambayo aliifanya kule Libya....!!! Kwanza Ile ilikuwa behind the opponent hivyo Che alicheza kwanza mpira Kisha acheza mguu na mwili wa mshambuliaji wa Al ahly Tripoli.
Nakusaidia tu, hakuna mtu ambaye ana weza kucheza tackle behind the opponent aka cheza mpira asiguse mwili wa mtu.Kwa sababu wakati aliye cheza Tackle ana shuka chini lazima balance yake iwe ni mwili wa aliye pembeni.
Kwaiyo refa ana angalia tukio la kwanza,Je alicheza mpira kwanza ? Au mguu aidha mwili wa opponent?
Kwa sababu haujui mpira kwako Hilo ni kosa ndugu mtaalamu!!
Duniani beki wa kati ana takiwa awe anajua kucheza standing tackle, behind tackle kwa usahihi na hizi Che ana zifanya kwa ustadi mkubwa.
Ndugu taja makosa mengine nikuelekeze kitaalamu.
KIFUPI KIKOSI KIZIMA CHA SIMBA HAKUNA BEKI ANAE WEZA KUMWEKA BENCHI CHE MALONE.
HUYU NDIYE BEKI BORA WA KISASA.