Muda wa Che Malone kukaa bench umefika

Muda wa Che Malone kukaa bench umefika

Tambala mbovu unaongea kitaalam Sana
Shida ya malon anajikutaga bonge la beki kumbe n wakawaida tu safu nzima ya ulinz n wazito ukienda viungo wazito sana ndomana simba inacheza taratibu sana
Timu Inayo cheza possession lini imewahi kucheza Kwa Kasi kubwa kuliko timu Inayo cheza direct ? Mashabiki Wana hitaji msingi wa falsafa ya Simba wa kumiliki mpira kwa kupasiana pasi fupi fupi ndio maana jina la utani ni Lunyasi Yani mpira una tembea kwenye nyasi na sio una butuliwa. Sasa nikusaidie Barca walikuwa na kazi wakati enzi za Pep ? Nisaidie una taka soka la aina gani ? Alafu Simba yenye viungo wa Zito ndio imefunga goli nyingi ligi kuu ndio imefungwa goli chache ligi kuu na Ina point sita Kimataifa....nitajie timu yenye Kasi kuliko Simba msimu huu Tanzania alafu Ina Namba nzuri kuliko Simba Ili hoja Yako ipate nguvu
 
Tambala mbovu unaongea kitaalam Sana.
Asante kaka yangu, mara ya mwisho ulininunulia mdogo wako chakula safi Sana pale kwa mama Msomali.Kwa kweli yule mama ana pika vizuri sana.Msalimie Msomali , Karibu Sana Makao makuu ya nchi kaka yangu.Kifupi Wewe ndio umenijenga zaidi niwe na jadili kwa hoja.Nina furahi kuwa na kaka kama wewe, mwenye maarifa ya kutosha.
 
Kuwa na utulivu kijana, kunywa Maji na ushushe Sukari.Kucheza mpira hakukupi kibali Cha kufahamu mpira !!! Kucheza mpira ni kipaji na ukocha ni taaluma...hapa tuna jadili jambo la kitaalamu.Alafu usitafute huruma ya kusema eti nimecheza, Sasa ukiwa umecheza ndio hoja Yako iwe imara ?
Hivi back pass ngapi kipa Kacheza mechi hiyo ? Kunaswa hiyo ndio una taka kuhalalisha kwamba Che ni beki mbaya au wa kawaida ?
Nimesema kwamba, kujiamini kupita kiasi ni kosa katika mpira kwa sababu ipo siku utaigharimu timu.

Mimi sijasema Malone ni beki mbaya, hapana! Hoja ilianzia kwamba, kujiamini kupita kiasi ni kosa katika mpira. Wewe ukaonesha kujiamini kupita kiasi ndio sahihi wakati si kweli.

Narudia tena, Malone ni beki mzuri lakini kujiamini kupita kiasi ni kosa lake na akiendelea hivyo atakuwa anaigharimu timu tu.

Kwa ule mpira angekuwa anajiamini kwa kiwango kati asingeweza kugeuzia ndani bali angegeuzia nje ukawa hata mpira wa kurusha mana aliuwini mapema sana lakini akaendelea kuusindikiza kwa sababu ya kujiamini kupita kiasi mpaka kugeuzia kwa kipa!
 
Kile KICHWA alicho piga alitakiwa awepo mtu afanye cover....!!!
Kwenye mpira timu Ina jikinda kwa kanuni beki akikaba au kucheza mpira ana takiwa awepo mtu wa kucover hiyo nafasi Kisha ana kuwepo mtu mwingine wa kutengeneza balance.
Sasa kwa mantinki hii Che Malone alicheza mpira kwa KICHWA je nani alikwenda cover kwa mshambuliaji?
Swali langu nani alikwenda kucheza drop ball Baada ya KICHWA Cha Che Malone ? Balance nani alifanya.

Karibu tujadili kiufundi ndugu yangu.

Hoja ya tackle ambayo aliifanya kule Libya....!!! Kwanza Ile ilikuwa behind the opponent hivyo Che alicheza kwanza mpira Kisha acheza mguu na mwili wa mshambuliaji wa Al ahly Tripoli.
Nakusaidia tu, hakuna mtu ambaye ana weza kucheza tackle behind the opponent aka cheza mpira asiguse mwili wa mtu.Kwa sababu wakati aliye cheza Tackle ana shuka chini lazima balance yake iwe ni mwili wa aliye pembeni.
Kwaiyo refa ana angalia tukio la kwanza,Je alicheza mpira kwanza ? Au mguu aidha mwili wa opponent?
Kwa sababu haujui mpira kwako Hilo ni kosa ndugu mtaalamu!!
Duniani beki wa kati ana takiwa awe anajua kucheza standing tackle, behind tackle kwa usahihi na hizi Che ana zifanya kwa ustadi mkubwa.
Ndugu taja makosa mengine nikuelekeze kitaalamu.

KIFUPI KIKOSI KIZIMA CHA SIMBA HAKUNA BEKI ANAE WEZA KUMWEKA BENCHI CHE MALONE.
HUYU NDIYE BEKI BORA WA KISASA.
Umemuona beki wako?
 
Simba watafute Beki mwingine, kila siku anaigharimu timu mechi muhimu. Habadiliki
 
Hata ile mechi dhidi ya Sfaxien hapa dar alifanya makosa ya kipuuzi ni vile tu wale jamaa hawakufunga . Hapo hamna beki labda abadilike ila sio beki tegemeo.
 
Huyu beki wa simba amekuwa na makosa mengi ya kijinga ambayo yamekuwa yakiigharimu timu.

Jana kasababisha goli kwa kosa la ajabu na lisilo ingia akilini kabisa.

Kwenye mechi ya Algeria aliokoa mpira kwa kupiga kichwa cha kindezi akasababisha goli, bado hatujaongelea makosa yake ambayo yamefutwa na goli kipa na mabeki wenzie.
Hiyo nimetoa kama mifano lakini ni huyu jamaa anafanya makosa karibia kila mechi.

Watu wana husisha makosa yake na kujiamini kupita kiasi lakini sio kweli bali ndo uhalisia wake ,kwa sababu makosa yake yamekuwa yakijirudia karibia kila mechi.

Sasa nadhani ni muda wa kuanzia bench labda ataanza kufanya majukumu yake kwa umakini.
Huu ushauri ufanyiwe kazi
 
Mimi nimecheza mpira siyo wa kutazama tu. Kwa mfano, kocha alikuwa anasema, ni kosa kubwa kugeuzia ndani, ni lazima ugeuzie nje na ukishindwa toa mpira nje ili wenzako wasogee mjipange upya.

Makosa anayofanya Malone ni ya kitoto si ya kufanywa na mtu mwenye jina kama lake. Kwanini hakugeuzia nje bali akageuzia ndani kwa pasi fupi? Tofautisha kati ya confidence (kujiamini) na over confidence (kujiamini kupita kiasi). Over confidence ina hasara pia. Malone akiendekeza over confidence atakuwa anachomesha tu!

Malone alikuwa na uwezo wa kugeuzia nje na kupiga volley au kutoa nje ila volley ndio ilikuwa sahihi
Nakazia tena. Nafikiri leo mmejionea wenyewe uzito wa kutafsiri matukio ya haraka unaomkabili Malone, kwamba afanye nini na wapi. Hayo siyo makosa ya kufanywa na beki mkubwa. Asipobadilika ataendelea kuigharimu Simba. Huko mbele wanapambana halafu yeye analeta masihara
 
Chemalone apumzishwe kwanini awe anarudia makosa yaleyale Kila Mara.
Hamza naye ajifunze kufanya marking, mfungaji alikuwa peke yake badala ya kumkaba akawa anamuangalia mpaka alipopokea mpira.
Huu mchezo wa back pass tulishausema lakini wanapenda nandio unasababisha magoli ya hovyo.
 
Ndugu yangu mpira sio sehemu Yako changua kitu kingine.Dunia nzima Ina hitaji beki anae jiamini alafu Wewe una taka beki mwenye hofu daaah.
Kujiamini kwa beki ndio Kuna tengeneza uwiano mzuri wa timu kujenga mashambulizi!!! Hebu jifunze kwanza mpira ndio uje uchangie kwanza.
Ndugu yangu, vipi leo umemuonaje Malone? Bado haujaamini kwamba mimi nimecheza mpira wa mchangani na kocha alikuwa hataki kabisa kugeuzia ndani! Nilikwambia huyu jamaa anajiamini kupita kiasi na atakuwa anaigharimu sana Simba ukaniona mimi mshamba sijui soka.
Baada ya lile kosa la kufungisha, alianza kujiamini kawaida kama inavyotakiwa. Kuna mpira alitoa nje, ili Bravo warushe kwa sababu alikuwa ni kama mtu wa mwisho na ndivyo ilivyopaswa kuwa hivyo lakini angeendelea kujiamini kupita kiasi angeanza mambo ya chenga au kurudisha kwa kipa bila uhakika
 
Back
Top Bottom