Muda wa Che Malone kukaa bench umefika

 
Tambala mbovu unaongea kitaalam Sana.
Asante kaka yangu, mara ya mwisho ulininunulia mdogo wako chakula safi Sana pale kwa mama Msomali.Kwa kweli yule mama ana pika vizuri sana.Msalimie Msomali , Karibu Sana Makao makuu ya nchi kaka yangu.Kifupi Wewe ndio umenijenga zaidi niwe na jadili kwa hoja.Nina furahi kuwa na kaka kama wewe, mwenye maarifa ya kutosha.
 
Nimesema kwamba, kujiamini kupita kiasi ni kosa katika mpira kwa sababu ipo siku utaigharimu timu.

Mimi sijasema Malone ni beki mbaya, hapana! Hoja ilianzia kwamba, kujiamini kupita kiasi ni kosa katika mpira. Wewe ukaonesha kujiamini kupita kiasi ndio sahihi wakati si kweli.

Narudia tena, Malone ni beki mzuri lakini kujiamini kupita kiasi ni kosa lake na akiendelea hivyo atakuwa anaigharimu timu tu.

Kwa ule mpira angekuwa anajiamini kwa kiwango kati asingeweza kugeuzia ndani bali angegeuzia nje ukawa hata mpira wa kurusha mana aliuwini mapema sana lakini akaendelea kuusindikiza kwa sababu ya kujiamini kupita kiasi mpaka kugeuzia kwa kipa!
 
Umemuona beki wako?
 
Simba watafute Beki mwingine, kila siku anaigharimu timu mechi muhimu. Habadiliki
 
Hata ile mechi dhidi ya Sfaxien hapa dar alifanya makosa ya kipuuzi ni vile tu wale jamaa hawakufunga . Hapo hamna beki labda abadilike ila sio beki tegemeo.
 
Huu ushauri ufanyiwe kazi
 
Nakazia tena. Nafikiri leo mmejionea wenyewe uzito wa kutafsiri matukio ya haraka unaomkabili Malone, kwamba afanye nini na wapi. Hayo siyo makosa ya kufanywa na beki mkubwa. Asipobadilika ataendelea kuigharimu Simba. Huko mbele wanapambana halafu yeye analeta masihara
 
Chemalone apumzishwe kwanini awe anarudia makosa yaleyale Kila Mara.
Hamza naye ajifunze kufanya marking, mfungaji alikuwa peke yake badala ya kumkaba akawa anamuangalia mpaka alipopokea mpira.
Huu mchezo wa back pass tulishausema lakini wanapenda nandio unasababisha magoli ya hovyo.
 
Ndugu yangu, vipi leo umemuonaje Malone? Bado haujaamini kwamba mimi nimecheza mpira wa mchangani na kocha alikuwa hataki kabisa kugeuzia ndani! Nilikwambia huyu jamaa anajiamini kupita kiasi na atakuwa anaigharimu sana Simba ukaniona mimi mshamba sijui soka.
Baada ya lile kosa la kufungisha, alianza kujiamini kawaida kama inavyotakiwa. Kuna mpira alitoa nje, ili Bravo warushe kwa sababu alikuwa ni kama mtu wa mwisho na ndivyo ilivyopaswa kuwa hivyo lakini angeendelea kujiamini kupita kiasi angeanza mambo ya chenga au kurudisha kwa kipa bila uhakika
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…