HDMI
JF-Expert Member
- Mar 10, 2018
- 672
- 1,332
Hiyo sheria inajulikana tatizo traffic atakuambia paki gari kituoni wakati unafuata leseni hapo ndio utaona bora nilipe 30k
Sent using Jamii Forums mobile app
Sent using Jamii Forums mobile app
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
unaenda mkuu 😛😛😛😀😀😀😀Nawaza hapa! Umekurupuka zako unawahi Morogoro! Kakukamata CHALINZE na driving license umeisahau Pugu! Anakupa ruksa ukaifate lkn uache gari pale CHALINZE
Sent using Jamii Forums mobile app
unaenda mdogo mdogo ha haaa ngoma ni ngumu utaomba uandikiwe yaishe haaaa sheria huwa hazikamiliki banaHiyo sheria inajulikana tatizo traffic atakuambia paki gari kituoni wakati unafuata leseni hapo ndio utaona bora nilipe 30k
Sent using Jamii Forums mobile app
Jaribu utakiona cha mtema kuni, wale ni miungu watu . Utageuziwa kibao kuwa unamzuia kutekeleza majukumu yake.Uzi huu lazima niubebe niwatunishie kifua askari siku nikidakwa bila leseni
Sent using Jamii Forums mobile app
Babu Msomali, Naamini kuwa kabla ya kupata leseni yako ulikwenda kozi ya udereva, kwa hapa kwetu ni mwezi mmoja. Naomba uniambie ni vitu gani muhimu sana unavyotakiwa kuwa navyo kabla hujaamsha gari, iwe kwa dharua au kwa starehe zako?.. Naomba unitajie angalau vitu vitatu kisha tupate pa kuanzia, nitakupa mifano kama unavyotaka.usi generalized kwa kusema dunia nzima kua specific na cite relevant authority kama mtoa mada alivyofanya..
Mtoa mada yupo sahihi watu wengi hatujui haki zetu na ndo maana tunaonewa na traffic barabaran.. Ukisimamishwa na traffic na huna lesen kwa wakat huo una haki ya kumtaka akueleze ni kituo gani ukaipeleke hiyo leseni yako.. someni hzi sheria jamani sio mnapinga pinga bila relevant authority.
Babu Msomali
Sent using Jamii Forums mobile app
Utaweza...!?Uzi huu lazima niubebe niwatunishie kifua askari siku nikidakwa bila leseni
Sent using Jamii Forums mobile app
Simpo tu, unampa tu mwaliko aje Kilimani PubTatizo mnapangaje kuonana ndani ya hizo siku tatu?
Amefafanua sheria inasemaje si mawazo yake.lakini kwa sasa jeshi letu lilipofikia ki-mawasiliano liwauwezo kuweka namba ya gari katika mifumo yao Kama kwa wadeni wa faini na popote nchi likakamatwa kulipa faini na riba kama wengineSwali: Utamthibitishia vipi askari kwamba utarudi kumuonyesha leseni kabla ya muda wa kisheria haujapita, ilhali mmekutana tu barabarani?
Sent using Jamii Forums mobile app
Nimeongeza kitu kwenye fuvu langu, Hongera kwa uelimishaji huu. Kuna shida moja barabarani siku hizi kinachofanyika ni zaidi ya udhibiti wa ajali za barabarani. Askari wa usalama barabarani wamekuwa ni kama kitengo cha kamishina wa Mapato ya ndani wa Mamlaka yetu ya kukusanya maduhuli (TRA) na ukichanganaya na ile kaului mbiu ya Boss wao ya "NYAKUA NYAKUA"inakuwa vurugu tupu.=========
ILANI: Makala hii hailengi wale wasio na leseni kabisa. Aidha, unashauriwa kupiga picha leseni yako ili angalau uwe na kumbukumbu ya namba ya leseni
=========
Kusimamishwa na trafiki barabarani, na ukawa huna leseni mfukoni kwa muda huo sio kosa. Mwambie huyo trafiki kuwa hilo sio kosa. Sheria inatutaka kutembea na leseni tunapoendesha vyombo vya moto, lakini pia haisemi kuwa utakapokuwa hauna pale unapoombwa na trafiki basi ni kosa.
Tunaongelea Sheria ya Usalama Barabarani, Sura ya 168. Wapo watu wameandikiwa faini kisa wameombwa leseni wakasema hawana, au wakasema wamezisahau majumbani. Hawa waliotozwa faini katika mazingira kama haya wameonewa. Na wanastahili kurudishiwa fedha walizotoa haraka.
Ni kweli kifungu cha 77 cha Sheria ya Usalama Barabarani kinamtaka kila mwendesha chombo cha moto kutembea na leseni barabarani. Ni kweli askari anayo mamlaka kumsimamisha mwendesha chombo cha moto. Na ni kweli pia kuwa askari anayo mamlaka ya kumtaka mwendesha chombo cha moto aoneshe leseni yake. Lakini sio kweli hata kidogo kuwa mwendesha chombo cha moto asipoonesha leseni kwa wakati huo basi tayari ametenda kosa. Sio kweli.
Kifungu cha 77(1) cha Sheria ya Usalama Barabarani kinasema kuwa mtu hatatiwa hatiani, kwa maana ya kulipa faini au kuandikiwa kosa au kuadhibiwa na chombo chochote ikiwamo mahakama, kwasababu tu hakubeba, au hakutoa/kuonesha leseni pale alipotakiwa kufanya hivyo, isipokuwa ana siku tatu za kutoa au kuonesha leseni hiyo tokea siku hiyo aliposimamishwa.
Tafsiri iko wazi kuwa unaposimamishwa, ukaombwa kuonesha leseni, ukawa huna kwa mda huo, unazo siku tatu mbele za kutakiwa kuleta na kuonesha. Anachotakiwa kufanya askari sio kukuandikia kosa, laa hasha, bali ni kukutaka umuoneshe leseni hiyo ndani ya siku tatu tokea siku hiyo. Ukishindwa kufanya hivyo ndani ya siku hizo hapo ndipo linaweza kuwa kosa.
Watu wasionewe. Wapo askari wengine pia hawajui hizi sheria. Hawa sisi madereva tuwaelimishe. Unaweza kudhani askari anakuonea kumbe naye hajui. Kwahiyo kazi unayo wewe kuhakikisha unamweleza huyo askari kuhusu kifungu hiki na namna kinavyotaka. Wewe ndiye mtetezi wa kwanza wa haki yako kabla ya kutetewa na mtu mwingine.
Na kama itatokea ukaandikiwa adhabu kwa lazima kwa kitu kama hiki, basi unayo haki ya kukataa kulipa na kuomba kufikishwa mahakamani ili sheria ikatafsiriwe. Mwambie “Sitalipa nataka sheria ikatafsiriwe mahakamani”.
Kukataa kulipa sio kosa au ukorofi na hivyo huna haja ya kukhofu. Kukataa kulipa ni haki katika haki ulizonazo ukihisi umeonewa. Na kama umeshalipa au ulilipa huko nyuma katika mazingira ya jambo kama hili na unao ushahidi basi unayo haki ya kudai hela uliyolipa. Unaweza kuidai huko ulikotozwa au mahakamani.
Sheria imetoa ahueni hii ikizingatia mazingira ya ubinadamu. Huwezi kila unapoamka asubuhi ukakumbuka leseni. Huwezi kila unapokuwa na safari ukakumbuka leseni. Safari nyingine ni za ghafla na za kushtua, mfano kuitiwa msiba, ugonjwa, matatizo kazini, bila kusahau msongo/stress za ada na kodi. Atapata wapi muda wa kukumbuka leseni mtu huyu?
Mwingine amebadilisha nguo na hivyo leseni kubaki kwenye nguo iliyovuliwa, mwingine amebadilisha gari na hivyo leseni kubaki kwenye gari jingine. Na mazingira mengine kama hayo. Zote hizi ni dharula za kibinadamu zilizowafanya watunga sheria kuweka muda wa siku tatu kwa ajili ya kutoa au kuonesha leseni.
Basi wote tubadilike, madereva na askari wasimamia usalama barabarani. Dereva asiwe mkorofi, kadhalika askari asimwonee dereva
Swali: Utamthibitishia vipi askari kwamba utarudi kumuonyesha leseni kabla ya muda wa kisheria haujapita, ilhali mmekutana tu barabarani?
Mwenye ile twiti ya Kangi Lugola kuhusu traffic wakikusimamisha na kuorodhesha makosa mengi, basi ihesabike kosa ni MOJA TU GARI NI MBOVU, unalipa 30,000/=
Linalokukamata ni Jeshi la Polisi ...askari kwa mamlaka anayopewa na jeshi anaweza kukuandikia notification na ukafika kituo chochote cha police ukaonesha hiyo leseni.Umwambie askari nitakuletea leseni serious? Labda Ulaya huko au Kenya. Bongo mzee kuna kakosa kao cha kifala cha kwamba umeizuia jamhuri kufanya kazi yake