Muda wa kumuonesha trafiki leseni ni mpaka siku tatu kama umesimamishwa na huna

Nawaza hapa! Umekurupuka zako unawahi Morogoro! Kakukamata CHALINZE na driving license umeisahau Pugu! Anakupa ruksa ukaifate lkn uache gari pale CHALINZE

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Babu Msomali, Naamini kuwa kabla ya kupata leseni yako ulikwenda kozi ya udereva, kwa hapa kwetu ni mwezi mmoja. Naomba uniambie ni vitu gani muhimu sana unavyotakiwa kuwa navyo kabla hujaamsha gari, iwe kwa dharua au kwa starehe zako?.. Naomba unitajie angalau vitu vitatu kisha tupate pa kuanzia, nitakupa mifano kama unavyotaka.
 
Swali: Utamthibitishia vipi askari kwamba utarudi kumuonyesha leseni kabla ya muda wa kisheria haujapita, ilhali mmekutana tu barabarani?

Sent using Jamii Forums mobile app
Amefafanua sheria inasemaje si mawazo yake.lakini kwa sasa jeshi letu lilipofikia ki-mawasiliano liwauwezo kuweka namba ya gari katika mifumo yao Kama kwa wadeni wa faini na popote nchi likakamatwa kulipa faini na riba kama wengine

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Iwapo askari atachukua leseni na kuondoka nayo wakati nikiwa safarini nifanyeje?

Mimi nashauri kuwa leseni ziwe kwenye dijitali pia iwapo dereva hatakuwa na leseni basi waitazame kwenye mtandao kama wanavyotaka kufanya CCM kuwa na digital id
 
Nimeongeza kitu kwenye fuvu langu, Hongera kwa uelimishaji huu. Kuna shida moja barabarani siku hizi kinachofanyika ni zaidi ya udhibiti wa ajali za barabarani. Askari wa usalama barabarani wamekuwa ni kama kitengo cha kamishina wa Mapato ya ndani wa Mamlaka yetu ya kukusanya maduhuli (TRA) na ukichanganaya na ile kaului mbiu ya Boss wao ya "NYAKUA NYAKUA"inakuwa vurugu tupu.
 
Mwenye ile twiti ya Kangi Lugola kuhusu traffic wakikusimamisha na kuorodhesha makosa mengi, basi ihesabike kosa ni MOJA TU GARI NI MBOVU, unalipa 30,000/=
 
Umwambie askari nitakuletea leseni serious? Labda Ulaya huko au Kenya. Bongo mzee kuna kakosa kao cha kifala cha kwamba umeizuia jamhuri kufanya kazi yake
Linalokukamata ni Jeshi la Polisi ...askari kwa mamlaka anayopewa na jeshi anaweza kukuandikia notification na ukafika kituo chochote cha police ukaonesha hiyo leseni.

Mbona zamani ulikuwa unashikwa singida unaandikiwa notification na unakuja kuiclear dar. Hili linawezekana.

Shukrani kwa mtoa mada umenifungua sikujua hili.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…