Muda wa kumuonesha trafiki leseni ni mpaka siku tatu kama umesimamishwa na huna

Kusahau leseni kupo. Nadhani tahadhari nzuri ni kutoa copy ya leseni yako na kuweka garini sambamba na kadi ya gari ili ikitokea umesahau na ukasimamishwa na Trafiki umweleze kuwa umesahau leseni nyumbani na umwoneshe copy. Hapo akiendelea kukomaa ana lake jambo hata hivyo, ninamshauri mleta thread hii ambaye bila shaka na mwanasheria atuwekee (attach) hivi vifungu vya sheria hasa kifungu cha 77 (1)
 
Swali: Utamthibitishia vipi askari kwamba utarudi kumuonyesha leseni kabla ya muda wa kisheria haujapita, ilhali mmekutana tu barabarani?

Sent using Jamii Forums mobile app

nami nilitaka kuuliza hili swali na je askari anaweza kuzuia chombo ulichonacho ili ukamletee leseni uliyoisahau nyumbani?
 
Nawashangaa sana wengi wenu humu munaendesha magari na hamjui hili.
Mimi moja ya mbinu ya kukwepa faini namuambia traffic police nimesahau leseni home. Wakati ninayo mfukoni. Kwa nn nafanya hivi, hawa ni wajinga sana. Akiishika leseni yako anaanza kukuandikia.
Sasa basi nikiwa nawaambia sina leseni sheria inasema ninatakiwa niilete leseni ndani ya masaa 48 (correct me if I am wrong hapa). Sema wengi wananiambia inabidi niwache gari kituo cha polisi (nadhani hii nayo ni sheria japo sijahakikisha).
Hivyo basi usumbufu unaoweza kupata ni huu tu wa mtuke hapo muelekee kituoni mkawache gari ndio uende home ukalete leseni. Camooooon sijawahi Fanya huu upupu huwa tunamalizana kiutuuzima baada ya hapo, if u noo warra amm seingi
 
gerara hia
 
Hilo la kupiga leseni picha kwa simu nimelipenda. Sijawahi kusahau simu hata siku moja ila leseni nasahau mara nyingi tu..👍🏾
 
Mkuu shida hapa hawa jamaa ukiwa huna lesseni wanakutaka ukalipaki gari kituoni kwao hadi utakapowakubali leseni. Hii kisheria imekaaje, na kama ikinitokea ni nn nnachotakiwa kufanya?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nipe elimu kidogo maana sasa hivi unaandikiwa tu police hachukui cash mkjibishana mpaka siku saba faini inaongezeka kwenye systems hapa inakuwaje?

Sent using Jamii Forums mobile app
Hawezi kukuandikia bila kumpa leseni kwakuwa lazima aweke kumbukumbu zako kwenye document anayokuandikia so kama hana leseni hana particulars zako
 
Japo cjaspma comments nyingi lkn sasa ukimwambia sheria inataka ndani ya siku 3 uwe umeshamuonyesha askari! Sasa huyu askari MTAACHANAJE pale wakati wewe unakwenda kufuata leseni?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ama kweli 'ignorance of the law is not an excuse' Jamaa hawa wanachukua advantage ya ujinga wetu.
Ahsante sana kwa elimu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…