Muda wote tu unawaza Kusafiri 'Majuu' kwanini huku nyuma Wajanja 'wasikupige' na Kujitajirisha?

Muda wote tu unawaza Kusafiri 'Majuu' kwanini huku nyuma Wajanja 'wasikupige' na Kujitajirisha?

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan aeleza kutoridhishwa na kasi ya uendeshwaji wa bandari.

Chanzo: ikulu_mawasiliano

Na kwa Kukusaidia hupigwi tu hapo Bandari bali unapigwa zaidi katika Utalii, Wizara ya Fedha na katika Madini.

Si ulisema Wewe utakuwa Mpole na ukampiga hadi Madongo Mtangulizi wako ( sasa Kalala Mazima ) kuwa alikuwa Mkali na anaharibu, ila Wewe utakuwa Unatuchekea tu Watanzania ili tukuone Unatupenda na Unatuhurumia?

Sasa unalalamika nini tena? Nakushauri tu Mama ( Rais ) tafadhali endelea tu Kutudekeza, Kutupetipeti Sisi Wanao na wala 'Usitufokee' na hata 'tukikuibia' Wewe tutoe 'Kiupole' na Uteue Wengine sawa?

Ninapenda mno Marais walio Wakali.
Kuna issue ya ndege ikilipuka nitakukumbusha.
 
Ada gani ambayo tumelipiwa na serikali?

Mimi nimelipa ada kuanzia darasa la Kwanza hadi mwaka wa 5 chuoni.

Hizo kodi zenu mmenitolea lini?
Umeshalipia ulinzi wako binafsi na ulinzi wa maeneo yote unayopita na kufanya biashara? Ukishalipia hayo uje na risiti onyesha upewe jambo lingine la kulipia ili usitolewe kodi na wengine.
 
Nilikwenda hosptali ya Serikali kuanzia juzi sijapata huduma nimepanga foreni ndefu kila nikikaribia kumuoma Dr. Mara anaondoka kama vile ameitwa sehemu! Kuna wakati nimemsikia Dr anasema anakwenda kunywa chai nami nikaheshimu Kwani huwezi kufanyakazi bila Kula lakini alirudi baada ya masaa manne!

Ngoma ikalala kesho yake ikawa kama Jana mara kalipie pale mara x-ray mbovu njoo kesho na nilipokwenda kesho kunakipimo unatakiwa ukapime nje ya hosptali maabara elekezi!

Yote haya sikuwahi kuyaona inaweza Kuwa ni kipindi hiki Tu lakini kilichoniuma ni Wale wagonjwa wenzangu waliojaa Sura za kukata tamaa Waliokuwa wamezidiwa mlangoni Kwa Dr. wakipitwa kama vile kufika kwao pale ni kosa kubwa linalowaudhi hawa wauguzi wa taifa.

Nadhani kabla ya katiba mpya na mambo kadha wa kadha tuungane kuona utumishi wa umma unawekewa mikakati na sheria za kipekee Kwani nilichojionea nashindwa kukitofautisha na Ujambazi unaofanyika TENA ule wa kutumia silaha Jamani Kuna watu wanaroho mbaya.
Kwani katiba ya sasa au kanuni zinasema watumishi wa umma wawe wazembe? Issue ni usimamamizi wa hao wafanya kazi. Sasa kama SSH amesema wafanya kazi walijengewa nidhamu ya uoga lakini si kuwa eti wanafanya kazi kwa budii kutoka moyoni. TUtaona mengi mwaka huu.
 
Back
Top Bottom