Muda wowote Nitaeleza kwa kina juu ya wote wanaotaka Kumyumbisha Rais Samia na kuleta Vurugu na kuigawa CCM

Muda wowote Nitaeleza kwa kina juu ya wote wanaotaka Kumyumbisha Rais Samia na kuleta Vurugu na kuigawa CCM

Mkuu kwa Nini Msimshauri Mama juu ya Mapungufu yanayo Honekana wazi wazi kwenye Uongozi wake?

Uzembe mazoea pamoja na Ufisadi umerudi kwa Kasi sana tofauti na Utawala wa mtangulizi wake.

Anaweza akawa Anafanya vizuri kwenye Kutafuta fedha lakini Usipo simamia Nidhamu na Uwajibikaji ni sufuri.

Mtangulizi wake Alizingatia sana Nidhamu na Uwajibikaji na Matokeo makubwa yalionekana kwa haraka.


Mwisho siyo Vema kuona kila Anae kosoa ni Adui. Bali Mnaweza mkachukua kama fursa ya kujitathimini na Kujitengeneza Upya kuliko kusifiana na Uchawa.
Wewe tulia tu utapata kufunguliwa akili na macho yako muda siyo mrefu
 
Ukishaanza kusema mimi ni nani it confirms, you have lost the plot.

Wewe unapambania fursa kama wengine. Mungu Mwenyezi ataamua kwa haki, nani anayestahili fursa fulani kwa wakati wake.

Kwa Taifa letu lilivyo, hata kama mtu amepewa dhamana ya uongozi, haina maana ndio amepewa hati miliki.
Uongozi unakuja na pia unaweza kwenda. Mbona una macho na unashindwa kuona...mbona una masikio na hutaki kusikia?

Kiburi sio maungwana, wahenga walisema.
Wewe unapambania fursa kama wengine. Mungu Mwenyezi ataamua kwa haki, nani anayestahili fursa fulani kwa wakati wake.
 
Ndugu zangu Watanzania,

Kaeni mkao wa kula ,kaeni mkao wa kufunguliwa akili na macho,kaeni mkao wa kufumbuliwa vitendawili na mabano ,kaeni mkao wa kuonyeshwa ya sirini na gizani ,kaeni mkao wa kujua ajenda ya kakikundi kanakotaka kujipachika jina la uzalendo kutimiza ajenda zake ovu na zenye nia ovu kwa Taifa letu.

Ndugu zangu Watanzania kuna kakikundi kanataka kujaribu kumyumbisha Rais Samia,kutaka kumtisha Rais kwa kutaka kuonyesha kana nguvu kubwa nyuma yake au kenyewe ndio chama chenyewe kuliko hata Mkutano Mkuu wa chama Taifa au kamati kuu ya chama Taifa au vikao vyovyote vile halali vya chama.

Kakikundi haka msingi wake umejikita katika chuki binafsi ,Udini ,ukabila na ukanda. Kamejikita katika kujihalalisha na kujiaminisha ya kuwa kenyewe ndiyo kanapaswa pengine kuamua nani awe Rais ,Makamu ,waziri Mkuu ,speaker wa Bunge na viongozi wengine wakuu katika vyombo vingine mbalimbali.

Ni kakikundi kanakofikiri pengine kana haki ya kufikiria na kuamua kwa niaba ya watanzania wote.ni kakikundi ambako kanaongozwa na maslahi binafsi na uroho wa madaraka pamoja na uchu wa madaraka na vyeo mbalimbali. Kana kiu ya kuiteka Ofisi Kuu kwa gharama ya aina yoyote ile iwayo.

Ni kakikundi ambako kanajaribu kwa namna yoyote ile kujaribu kumchafua Rais Samia na kuharibu haiba yake mbele ya macho ya watanzania. Shabaha yake kuu ni kuhakikisha kuwa Rais Samia anachafuka , kuchafuliwa,kupakwa matope ,kusilibwa,kuzushiwa uongo na uzushi pamoja na kumchonganisha yeye binafsi na watanzania. Kamedhamiria kutaka RAIS Samia achukiwe na kuonekana ndiye adui wa Taifa hili na watu wake.

Ndio Maana mtaona na mtaendelea kuona kuwa mashambulizi Yoote yataelekezwa katika kumchafua yeye pekee tu .kwa sababu huyu ndiye aliyeshikilia nafasi ambayo wao wanaimezea mate usiku na mchana na kuiota. Wao shida yao ni Urais tu ili waweze kupanga sasa safu zao zooote zinazobakia na ambazo ni nyeti na muhimu.

Hii ni baada ya maamuzi ya Mkutano Mkuu wa CCM kuwapiga msasa kwenye kidonda kibichi pasipo wao kutegemea au kujiandaa au waweza kusema ya kuwa walipigwa shambulizi la ghafla bila wao kujiandaa. Na kibaya zaidi shambulio hilo lilifanywa kikatiba na kikanuni kabisa kwa kujibu wa katiba ,kanuni na miongozo ya katiba ya CCM. Yaani hakuna kipengele chochote kile kilichokiukwa.

Hivyo kakikundi hako kanataka kujaribu kutumia nafasi yake ya mwisho mwisho kujaribu kuigawa CCM na kuleta vurugu ambazo wao wanafikiri pengine zinaweza kuchochea uasi , Mapinduzi ya kikatiba na mivurugano mbalimbali na kukosekana kwa maelewano ndani ya chama ili kupata upenyo wa kutimiza lengo lake la kuimendea ofisi kuu kwa kumpachika mtu wanaofikiri atalinda maslahi yao binafsi.

Hata hivyo ni kuwa hawawezi kamwe na katu kufanya Mapinduzi ya aina yoyote ile ndani ya CCM wala kuleta mgawanyiko au kuchochea ugomvi na kuvunja umoja na mshikamano. Kwa kuwa CCM ni chama imara na madhubuti na chenye mfumo imara na wa kipekee sana.

CCM ndio Tanzania na Tanzania ndio CCM yenyewe.huwezi kuitikisa CCM pasipo kuitikisa Nchi yenyewe na watanzania. Hivyo anayewaza kufanya hivyo anajidanganya yeye binafsi na wanaomtuma na kumdanganya. CCM ni kubwa kuliko mtu yeyote yule au kikundi chochote kile. Cheza na kitu chochote kile lakini usicheze na CCM. Hii ni taasisi imara na yenye intelligensia kali sana yenye kuona hadi gizani.

Rais Samia ndio Mboni Ya Taifa letu. Tutamlinda, kumtetea na kumpigania kwa gharama yoyote ile iwayo.View attachment 3411197

Kazi iendelee, Mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa Maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.

Lucas Hebel Mwashambwa, Mama ANATOSHA kuendelea kuliongoza Taifa letu kwa muhula wa pili.
Vipi kuhusu utekaji, uhuru wetu, na Ufisadi unaoendelea nchini
 
Subiri tu uone moto nitakao uwasha humu jukwaani
Leo jino kwa jino weka andiko lako nilipangue kwa hoja nataka battle na Wewe. Maana unatuabisha sana Vijana wa Kitanzania kutufanya tuonekane Machawa na watu tusiokuwa na uwezo wa kifikra.

Weka andiko lako leo Mimi na Wewe jino kwa jino
 
Mbona wewe upo humu na wala hujatekwa.
WaTanganyika wengi sana wameumizwa kwa kutekwa, kupotezwa na wengine kuuliwa kabisa ili kulinda upumbavu unaoendelea.

Mimi nilianzia Tanu youth league 1974 na Ccm hii imezaliwa tunaona kwa macho na akili zetu. Haikuwa hivi ya kunyamazisha watu. Haikuwahi kuwaona wananchi kama maadui bali wazalendo. Hii ya kwenu ni kikundi cha mafisadi ktk koti la uongozi. Na ndiyo mnamuona kila mTanganyika ni adui.
 
Heshima yako mkuu ,nimelipenda andiko lako ila nikitaka kusema kuwa sikupati kwenye namba yako.

Yule boss wangu amenichimba biti tena eti hakuogopi kaka
 
Binafsi namuombea sana sana Rais Samia. Hao watu ni hatari hata kwa usalama wake. Ee Mwenyezi Mungu mlinde mama yetu na hao wabaya wanaomzunguka.
October tunatiki
 
Back
Top Bottom