Mudavadi: Tanzania iko sahihi kulinda Utaifa wake, Jumuiya ya Afrika Mashariki siyo Taifa ni Mwamvuli tu

Mudavadi: Tanzania iko sahihi kulinda Utaifa wake, Jumuiya ya Afrika Mashariki siyo Taifa ni Mwamvuli tu

Naona pongezi zinatoka kila mahali baada ya serikali kuyafurusha magenge ya wahuni waliodhani Tanzania ni shamba la bibi.

Pia soma > Pre GE2025 - Serikali ya Kenya yajitenga na sakata la Martha Karua kuzuiwa kuingia Tanzania

---
MKUU wa Mawaziri, Musalia Mudavadi ametetea matamshi ya Rais wa Tanzania Samia Suluhu kuhusu wanaharakati wa Kenya kuingilia masuala ya utawala nchini mwake.

Haya yanajiri huku mwanaharakati wa Kenya Boniface Mwangi akiendelea kuzuiliwa Tanzania.

Akizungumza Jumanne usiku (Mei 20, 2025) katika Citizen TV, Bw Mudavadi alikiri kwamba maoni ya Rais Suluhu kuhusu wanaharakati “kuingilia” masuala ya Tanzania yanaonyesha ukweli fulani.

“Sitapinga hilo kwa sababu nadhani kuna ukweli fulani. Hebu tukabiliane na mambo machache. Kiwango cha adabu, matusi, tunachoona nchini Kenya, ingawa tuna uhuru wa kujieleza, wakati mwingine kinazidi kupita kiasi. Ni ukweli anavyosema kuwa wakati mwingine matamshi yetu huku Kenya hupita kiasi,” alieleza Bw Mudavadi.

Aliongeza kuwa Wakenya wakati fulani wanakosa uadilifu katika matamshi yao.

“Mimi pia ni Mkenya, na ukweli wa mambo ni kwamba mtazamo wetu na matamshi yetu, kwa sababu tuna uhuru wa kujieleza, yamekosa uadilifu,” alisema.

Alipoulizwa ni kwa nini alimuunga mkono Bi Samia licha ya kutotaja uhalifu wowote uliofanywa na wanaharakati hao, Bw Mudavadi alisema anahitaji maelezo zaidi kuhusu operesheni hiyo.

“Yeye (Samia) amesema hana furaha, kwa sababu wanaangalia tunachofanya hapa, lakini nitahitaji muda kidogo kupata ushahidi zaidi kuhusu operesheni hiyo. Sizungumzii watu husika, lakini anazungumza kwa mtazamo wa jumla, na kama ni mtazamo wa jumla, basi nadhani ana hoja,” alisema.

Kando na hayo, Bw Mudavadi pia alifafanua kuwa ingawa uhuru wa kujieleza ni muhimu, kipaumbele cha rais kilikuwa kutetea uhuru wa nchi yake (Tanzania).

Pia soma
We huna akili kabisa ukisikiliza hapo kamtetea ? kadhibitisha kuwa udikteta ndio umetaradadi Tz wao wako vizuri zaidi kwenye Democracy.
 
We huna akili kabisa ukisikiliza hapo kamtetea ? kadhibitisha kuwa udikteta ndio umetaradadi Tz wao wako vizuri zaidi kwenye Democracy.
Kasema Kenya is so democratic, hakusema Tanzania sio democratic, democracy inaenda na mazingira
 
Martha karua ni mpinzani kenya, serikali ya huko haiwezi kumsemea vizuri kwa sababu pia ni mwiba kwao. Kuna gazeti moja la kenya liliandika martha karua afurushwa tanzania, ni kama linashangalia
 
We huna akili kabisa ukisikiliza hapo kamtetea ? kadhibitisha kuwa udikteta ndio umetaradadi Tz wao wako vizuri zaidi kwenye Democracy.
Umeelewa wewe zoba?
 
Martha karua ni mpinzani kenya, serikali ya huko haiwezi kumsemea vizuri kwa sababu pia ni mwiba kwao. Kuna gazeti moja la kenya liliandika martha karua afurushwa tanzania, ni kama linashangalia
Waziri wa Mambo ya Nje wa Kenya ametupa go-ahead kuwashughulikia, watakoma
 
Zenji mbona pametulia huku Tanganyika kuna nini??huyu mama mbona anatupelekesha,??kila kitu anamiliki yeye hizi zama namshauri awe mpole.
Juzi nimesikia madaktari wa mama wanaenda Njombe kutoa huduma! Nilishangaa sana
 
Back
Top Bottom