Muelekeo wa Uwekezaji nchini chini ya uongozi wa Prof. Mkumbo, Tunatokaje tulipo?

... hata hao wa ndani wakiwekewa makodi makubwa makubwa ya kukomoana lazima watafunga shughuli zao. Kodi za kukomoana ni miongoni mwa matatizo makuu ya uwekezaji.
 
... bora Prof. Mkenda yeye anaongoza jeshi kuwasambaratisha nzige waliovamia Kaskazini kutokea nchi jirani. At least that's something tangible kwa mwananchi wa kawaida.
 
Huyu mzee hana ubuni wowote yeye anachowaza ni CHADEMA unaitwa kwenye kipindi kwenye TV badala ya kuongelea mipango wewe unakomaa na CHADEMA mwanzo mwisho, Wizara haina Waziri ina kivuli pekee
Yaani alishangaza wengi kwa kweli, muda wote ni yeye na chadema tu, hapo ndipo tunapohoji elimu za hawa wanaojiita maprofesa,
Anatakiwa atolewe kwenye hiyo nafasi haraka sana.

Maana hana uwezo wa kufanya chochote zaidi ya mipasho.
Atafutiwe kazi ya kuiponda CDM huko kwenye chama cha sisemu
Hana mbinu,maarifa,maono wala mikakati ya kuisongesha sector ya uwekezaji,
Sana sana huko kwenye hiyo sector,atawatafuta wawekezaji wanaoiunga mkono CDM awafungie shughuli zao, ndio mawazo yake hayo
 
... Covid-19 imeathiri uwekezaji duniani kote sio Tanzania peke yake japo Tanzania haina Corona kwa mujibu wa wataalamu wetu. Pili sheria za kodi nazo ni tatizo; Wizara ya Prof. Mkumbo ni mwathirika wa hayo.
Atatumbuliwa soon
 
Mada yako ni nzuri ila nilipofika hapa nikachoka kabisa...... Huwezi tegemea chama tawala kilichopitisha ilani ndio hiko hiko kifanye scrutiny kwa makosa yaliyozalishwa na serikali/TRA ambao ni zao lao!!
Nadhani ifike mahala Private sector ishirikishwe kabisa maana wao ndio wanajua wanataka nini..... tume zipo kibao kuanzia ya ushindani, baraza la uwezeshaji uchumi, Financial intelligence unit n.k lakini ufanisi wao umesaidia nni?

Ifike kipindi private sector nao watoe maoni na miongozo ya nni kifanyike sio kuwapangia tu. Kma ni timu ikiundwa basi nusu wachaguliwe na waziri na nusu watoke Private sector maana wao ndio wanajua kadhia yote but kuingiza vyama na serikali kujikagua wenyewe ni ngumu mnoo.

Ni vile tu mtasema sio uzalendo ila unaweza hta kuwapa tender kampuni za kikaguzi na consultancy za nje kma PwC kwa mkataba yaani wao kazi yao ni kufuatilia hayo yote na kutoa mapendekezo na ushauri wa kitaalam. Trust me ufanisi wao utakua mkubwa sababu wanaenda kibiashara zaidi ila haya ma-tume hayana faida zaidi ya vikao tu kutafuta umaarufu kwa matamko kwenye camera!
 
mkuu nmefurahi na ww umeona hilo tatizo.... Sijaelewa kwanini anawaza chama dola ndio kisimamie masuala ya kitaalam kama haya. Siasa ikiingizwa huko utashangaa wanajazwa UVCCM kufuatilia biashara wakati ilipaswa iwe na professional consultants wasio na vyama tena wana experience kwenye field!!
 
Serikali nyingi hutumia pesa nyingi na muda mwingi kutengeneza sheria na miongozo ya kufanya biashara chakushangaza biashara huwa hazifanikiwi hufa
 
Mkumbo na Sosholojia yake na uwekezaji - ni mafuta na maji. Huyu anchojua ni porojo.

Badala ya kuingelea uwekezaji, anaongelea CHADEMA, huo si ujinga wa hali ya juu? Hakuna faida Taifa litapata kwenye uwekezaji kwa kumtegemea huyo unprofessional Prof.
 
Huyu mzee hana ubuni wowote yeye anachowaza ni CHADEMA unaitwa kwenye kipindi kwenye TV badala ya kuongelea mipango wewe unakomaa na CHADEMA mwanzo mwisho, Wizara haina Waziri ina kivuli pekee
Wawekezaji wakubwa hawataki sijui nn? Wao wanataka predactibility. Haya mambo ya kulipishana mafaini kwa mashirika ya Madini mlizani mnawakomoa kina Lisu???
 
Mazingira ya uwekezaji siyo RAFIKI kabisa kwa mtu kuja kuwekeza Tanzania. Ndiyo maana hakuna hata muwekezaji mmoja aliyetokea kuja Tanzania baada ya Magufuli kuingia. Mwekezaji wa mwisho mwenye mtaji unaogusa uchumi wa nchi ni DANGOTE tu aliyekuja mwaka 2014 wakati wa JK akatumbukiza Dollars 0.5Trillion.

Wachawi wa mazingira ya uwekezaji Tanzania ni sheiria zetu tunazoandika kila siku, TRA, TAKUKURU na Mkuu wa nchi mwenyewe
 
Eti watu smart sana...
Mbona nyie wabongo mnapenda kusema
Mtu fulani bwana smart sana
Mtu akijua kupiga tantalila mtaskia aise jamaa
Smart sanaaa

Ova

Sent from my SM-N920T using JamiiForums mobile app
 
Hii sekta ngumu hasa kipindi hiki cha korona lakini bado kuna mambo mazuri yanayoweza kufanyika kama mifumo ikiboreshwa
Wewe achana na mambo ya korona, huko ni kuzunguka zunguka na kudeflect blames sehemu isiyohusika. Uwekezaji nchi hii umeanza kusua sua tangu 2016, korona imeingia 2019.

Takwimu za Tz kupokea wawekezaji wakubwa zipo, na juhudi zimerudi nyuma sana katika huu utawala wa awamu ya tano, Huyu baba alipoapishwa tu alianza kudeal na watu fulani fulani, Mfano ni yule mfanyabiashara mkubwa aliyeweka mtaji mkubwa na kuajiri maelfu ya waTz. Wamemharass we hadi akahamisha mtaji wake kwingine. Dunia nzima inafahamu alichofanyiwa yule mfanyabiashara, kufikiri wenye mitaji wataendelea kumiminika ni kujitoa ufahamu. Infact, Tz haijapokea mfanyabiashara mwenye mtaji mkubwa kama Dangote kipindi hiki cha Dk,Mtukufu, mheshimiwa sana Magufuli sababu ya mazingira ya uwekezaji kutokuwa rafiki na mabavu.

Tatizo la kiongozi wetu ni kudhani dunia inatuhitaji kuliko tunavyoihitaji, Mkiwaharass wafanyabiashara watapeleka mitaji yao kwa majirani zetu wakenya, uganda, Zambia etc. Tutakosa kodi na ajira za watu wetu.
 
Kitila hiyo nafasi siyo ya kupiga porojo, mazingira ya kufanya biashara ni mabovu na yanatakiwa kuboreshwa ili kuwawezesha wafanyabiashara waliopo ndani wawe na imani ya mitaji yao kukua na kupanua biashara zao. Kama wawekezaji wa ndani hawana imani na sera ya biashara, wafanya biashara wa nje hawatataka hata kusikia neno tanzania. Nani atakuja kama waliopo ndani wanachechemea na kufunga biashara zao?
 
Dola- Kiswahili - Daulatt- Kiarabu- Sovereignty - kingereza.

Mkuu pata maana yake kwanza mbona unaogopa sana Dola.

Sovereignty means some persons, assembly of group of persons in every independent state have the final legal authority to command and enforce obedience.
 
MMECHANGIA WENGI NI MICHANGO YA KILA MTUU AONAVYO, LAKINI HAKUNA HATA MMOJA ALIYE ADDRESS SAWA SAWA TATIZO AMBALO BIASHARA ZETU ZINAPAMBANA NAZO.

KWA PROJECTION YA MKUU LABDA AONGEZE KUKUSANYA KODI NA WAKATI HUO HUO A PRINT PESA NA KUTOSHA KUPAMPU KWENYE MZUNGURUKO WA SASA.

Tatizo pesa ama mitaji haipo huria, kwa hiyo biashara huria Haito wezekana.

Biashara huria bila mitaji huria ni sawa na gari lá bila mafuta yakuliendesha. Pesa iliyo nunua madege, meli za maziwa karibu yote, barabara zinazo jengwa na makontrakta wa njee, Ujenzi wa Bwawa lá Nyerere wamelipwa malipo yao na wamepeleka kwao zaidi ya billion 15 USD ( kama trillion 43 )zimenyofolewa kutoka kwenye mzunguuko wa pesa zetu, jee tumebaki na nini?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…