Muendelezo wa miujiza ya Mungu kwenye maisha yangu.

Muendelezo wa miujiza ya Mungu kwenye maisha yangu.

Mazima1

Senior Member
Joined
Dec 31, 2020
Posts
192
Reaction score
550
Habari wakuu,mara ya mwisho nilisimulia hapa jinsi ambavyo nilipitia kipindi kigumu kwenye maisha yangu baada ya kupoteza kazi ikafika kipindi nakosa hata shilingi 100 ndani na nina familia ila baada ya kuattend maombi ya fulani mambo yakafunguka hapo hapo

Story yenyewe hii hapa

TUENDELEE SASA
Basi bhna ndani ya kipindi ambacho nilikuwa nimepoteza kazi ikawa muda mwingi tunapishana maelewano na wife tena kwa sababu ndogo ndogo hadi tukishasolve tunajiuliza kwanini tulipishana kwa kitu kidogo vile basi maisha yakaendelea ni ndani ya kipindi hicho hicho
nikaanza kuumwa ugonjwa wa ajabu sana kwa walosoma boarding ulikuwa unaitwa pumbu erosion😂

Asee wale fungus walikula sehemu zangu za Siri vibaya mnoo🙌🙌🙌

Miwasho kila muda hadi ukijikuna ngozi inatoka,nikashangaa ugonjwa huu umetokea wapi?

Basi ikabidi nichome moto boxer zangu nikanunua nyingine mpya hapo nishatumia kila aina ya dawa za pharmacy zikiwemo hizo cream lakini baadaye nikapewa za vidonge pamoja na cream nitumie zote kwa pamoja,hizo nilipewa hospital lakini bado fungus walizidi kutafuna ngozi ya sehemu za siri,

kumbuka hizo dawa zote natumia gharama yaani nakopa hela ili ninunue dawa maana hata kazi Sina,

Hilo tatizo likaendelea hadi nilipopata kazi sasa nikawa nimepata safari ya kikazi asubuhi nilivoamka nikajifunga taulo nikaoge ndo nikajiangalia sehemu zangu za Siri zilivyolika na fungus asee nikasikitika sana kwani hali ile ilikuwa mbaya,

Basi kama kawaida yangu nikaanza na maombi Sasa wakati naomba nikamuuliza Mungu je huu ni ugonjwa wa kawaida au Kuna nguvu za giza zimehusika??

Kuna ishara Fulani nikamuomba anioneshe pale pale nikaoneshwa ishara fulani ambayo inaonesha kwamba ni nguvu za giza zimehusika na wala si ugonjwa halisi(hiyo ishara sitoeleza hapa)

Nikaendelea kuzama kwenye maombi huku nikiuliza kwanini nitupiwe huo ugonjwa nikapewa majibu kwamba lengo ni kunirudisha nyuma kimaendeleo,na kweli nilirudi nyuma kimaendeleo sana asee maana kila mara nilikuwa nikipata hela nanunua dawa na ugonjwa wenyewe hauponi,

Nikauliza nani anafanya yote hayo pale pale kwenye maombi nikafanikiwa kumjua mhusika ambaye ni family member kabisa ingawa miaka ya zamani niliwahi kusikia akishutumiwa kwa uchawi lakini nilidhani anasingiziwa nikajua pia na watu wote anaoshirikiana nao kufanya yote hayo (remember hayo majibu yote nayozungumzia hapa nilipewa on the spot wakati naomba ingawa najua nitaonekana muongo but Mimi nazungumzia mambo halisi kabisa yaliyotokea maishani mwangu tena mwaka huu)

Basi ghafla akili ikaniingia kwamba niombee maji Kisha nijisafishe sehemu husika na nikafanya hivyo basi ukawa ni utaratibu wangu wa kila siku na hapo nikasema siingii gharama tena kutibu huu ugonjwa,

Nikaendelea kuombea maji na kujisafisha sehemu husika kwa imani,basi ndani ya wiki na siku kadhaa ugonjwa ukaanza kupotea kidogo kidogo na finally ukapotea kabisa

Wakuu kiufupi nina shuhuda nyingi za kusimulia lakini Mimi binafsi nimeomba kwa jina la Yesu na nimevushwa katika mengi ndani ya huu huu mwaka 2026,

Najua wengi mtakuja hapa kunidhihaki kama Mimi ambavyo nilikuwa nawadhihaki wengine hasa walokole😄 lakini naomba kwa wale ambao mmejaaliwa imani kidogo basi msikate tamaa Mungu yupo

Shuhuda nyingine nitendelea kuzitoa kadri ya mambo yanavyozidi kutendeka maishani mwangu
 
Back
Top Bottom