Mufindi: Afungwa Jela miaka 20 kwa kukutwa na kilo 32 za nyama ya Tandala

Wewe kama ni Mpemba hakuna ulijuwalo kuhusu nyama pori.

Wenye Leseni za mabucha ya wanyama pori ni wachache sana Tanzania nzima, ila wawindaji wanatumia vibali halali ni wengi.

Binafsi huwezi kunifunga kwa kesi ya kipuuzi kama hiyo, nyama nimenunuwa kwa wawindaji ambao wamewinda kihalali na huu ni msomi wa uwindaji.

Nyama pori tunauziana mtaani kwa ajili ya kitoweo sawa na muuza utumbo au muuza mchicha hakuna kwenye Leseni ya kufanya hizo biashara.

Isitoshe siwezi kukaa kijiji Jirani na game reserve halafu nisile nyama pori wakati hivyo vitoweo katupa Mungu mwenyewe.

Ni sawa na watu wa pwani au ziwani uwaambie kuvuwa Samaki wavuwe kwa kibali ni upuuzi mtupu.
Well Noted Mkuu....
 
Daaah inauma Sana wanyama wetu njaa zetu
2019 ndg yangu alikutwa anapika kilo moja swala kainunua kutoka Kwa muuzaji simkumbuki jina bana nyie pale Arusha alikaa jela zaidi ya siku 90
Huyo ni mnunuzi tuu

Ifike mahali kuwe na limit ya wanyama kuuwawa Ila wengine wafanywe kitoweo please
 
Mambo kama hayo ndio starting point ya kudai haki kwa wananchi wanyonge hapo ilitakiwa kukinukisha kwa maandamano Nchi nzima kupinga huo uonezi miaka 20 kisa nyama ya tandala!!! What's a shithole country?
 
Kesi za kipuuzi hizi, law society muwe mnatembea nchi nzima kuwasaidia bure watu wanaofungwa kwa upuuzi kama huu.

Wanyama ni viumbe tumepewa na Mungu bure kutumia kwa kotoweo.
hivi hizi mahakama Huwa hazihusiki na yale majizi yanayotajwa kwenye ripoti ya CAG? wanahangaika na watu na vitoweo, kuwaonea tu watu!!!!

shithole countries!
 
Mahakama ya Wilaya ya Mufindi, imemhukumu Mbogo Tinda (45), Mkazi wa Kijiji cha Ihoanza Tarafa ya Malangali, wilayani hapa, kutumia kifungo cha miaka 20 gerezani, baada ya kumtia hatiani kwa makosa mawili.

Makosa hayo ni lile la kukutwa na nyara za Serikali (nyama ya Tandala – Kudu, yenye uzito wa kilo 32), lakini pia kujihusisha nyara za Serikali bila kuwa na kibali.

Hukumu hiyo imetolewa jana September 4, 2023; na Hakimu Mkazi Mwandamizi wa Mahakama hiyo, Benedict Nkomola, ambapo imedaiwa mshtakiwa huyo alipatikana na nyama ya Tandala yenye thamani ya Sh7, 859, 136 milioni.

Akisoma shtaka hilo, hakimu huyo amesema mnamo August 26, 2023 katika Kijiji cha Idope, Kata ya Ihoanza, wilayani hapa, mshtakiwa huyo alikutwa na nyama ya Tandala ambayo alikuwa anaiuza bila kuwa na uhalali wa kufanya shughuli hiyo.

Inadaiwa kuwa mshtakiwa alinunua na kuuza nyama ya Tandala kilo 32, yenye thamani ya kiasi hicho cha fedha ambayo ni mali Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania bila kuwa na vibali au leseni ya kuuza nyama hiyo.

Pia hakimu huyo amesema kosa hilo ni kinyume na kifungu namba 86(1) (2) (a) na kifungu (3) cha sheria ya uhifadhi wa wanyapori sura 283 rejeo la Mwaka 2022, ikisomwa pamoja na aya ya 14 Jedwari la kwanza la vifungu vya 57(1), na 60 (1) (2) vya sheria ya makosa ya uhujumu uchumi na makosa ya kupangwa, sura 200 rejeo la Mwaka 2022.

Aidha katika kesi hiyo ya uhujumu uchumi namba 11, 2023; mshtakiwa alikiri kutenda makosa hayo, ndipo mahakama ikamtia hatiani na kumhukumu kwenda jela miaka 20 kwa kosa la kwanza na pili ambapo adhabu hizo zitaenda sambamba.

Awali akizungumza kabla ya kutolewa hukumu hiyo, Mwendesha Mashtaka wa Serikali, Ahmad Magenda, aliiomba mahakama itoe adhabu kali kwa mshtakiwa.

"Niombe mahakama yako itoe adhabu kali kwa washtakiwa wote ambao wanafanya makosa kama haya ya kuhujumu wanyapori ambao ni vivutio kwa watalii, sanjari na kukuza pato la mtu mmoja mmoja na Taifa kwa ujumla," amesema Magenda.

MWANANCHI
akate rufaa, tutamchomoa kabla ya saa nne asubuhi
 
Sheria tunazojiwekea ni kandamizi kws upande mwingine, Na watu wanakutwa na ufisadi wa mabilioni ya pesa, anapewa kifungo cha nje au faini laki 5, Binadamu tulikubaliana tuwekeane utaratibu wa kuishi duniani, Ila waliopo chini ndo wanaumia na kutengwa. Mahakama ingemsamehe na kumpa kitalu cha uwindaji kama wale wengine.
 
Huu ni uonezi kabisa,hukumu hizi mbona zinatolewa Kwa wazawa tu,kila siku wageni wanakamatwa na hizo nyara ila wanalipa faini,yaani Mwananchi mwenye mali yake anahukumiwa kiasi hiki..... Mahakimu na Mahakama huu Muhimili lazima ujitafakari sana katika kutekeleza haki
wapo pia wawindaji wanaozidisha idadi kwenye vitalu vyao
 
Back
Top Bottom