Mufindi: Watu 18 wamefariki katika ajali ya Coaster na lori

Watu 18 wamefariki katika ajali ya Coaster na lori Rais Hana habari na hajatuma Hata salami Za Rambi Rambi kwa wafiwa na majeruhi? Nchi ya ajabu sana hii​

 
Imetokea ajali mbaya iliyohusisha basi dogo aina ya Coaster na lori

Watu 18 wamekufa eneo la tukio

Source ITV habari
 
Hakuna hata shuhuda wa kusema nini kilitokea...?

Moja ya barabara bora kabisa hii, barabara pana, alama zote zinezibgatiwa... . Poleni sana wafiwa.
 
Imetokea ajali mbaya iliyohusisha basi dogo aina ya Coaster na lori

Watu 18 wamekufa eneo la tukio

Source ITV habari
Toa taarifa kamili wewe Mzee Mgaya. Nina maslahi na hilo eneo la Wilaya ya Mufindi kwa ujumla wake.

Coaster ilikuwa inatoka wapi, kwenda wapi! Chanzo cha ajali ni nini!!
 
hapo lazima kuna mmoja alikuwa wrong lane
Mwenye Coaster ndiye mwenye makosa alikuwa kushoto linakopanda lorry mwenye lorry yeye alikuwa ameshawajibika kwa kosa lake kwa kuhamia upande wa kulia ila coaster ghafla akarudi upande wake ndo yakatokea hayo.

Ukiangalia Costa ilivyoharibika vibaya inaonekana hiko kishindo siyo cha gari iliyotoka mbali pana distance ndogo sana ndo maana bado kwa kiasi makalio ya coaster yapo upande wa kushoto.
 
Toa taarifa kamili wewe Mzee Mgaya. Nina maslahi na hilo eneo la Wilaya ya Mufindi kwa ujumla wake.
Taarifa kilo itatolewa na RPC

Ila coaster Ilikuwa inatoka Dar ikagonga lori bovu lililokuwa limeegeshwa barabarani

Wakati wa uokozi lori lingine likatokea na kugomga majeruhi
 
Mungu awape pumziko jema na kuwafariji wafiwa, majeruhi awape upinyaji wa haraka, binafsi kazi zangu zunahusisha sana safari, huwa nawaza na kujiachia kwa Mungu, kama binadamu hatuna uwezo nazo, matukio ni mengi sana huko barabarani, tusiache kusali wakuu kila inapobidi.
 
Poleni Sana Dah njia yangu hii napita Mara nyingi
 
Madereva wengi hawafuati sheria ,wanabahatisha. Ukisafiri na basi halafu ukakaa siti ya mbele madereva wanaovatake pasiporuhusiwa ila bahati tu mbele hakuna gari inayokuja. Na bado abiria tuna/wanacheka na dereva.
Ajali haina kinga ila ka huna roho ngumu kwny bus usikae mbele asee jamaaa wanaovateki kihasara sana hata mkifika salama kosa kosa za uso kwa uso na malori huwa kibao....

Mtu anaovateki semi 4 afu anarudi kwake dk ya mwsho kbs unasikia vuuu
 
Mkuu hivi umejipa hata muda wa kusoma habari kamili? Maana hiki ulichoandika na ambacho RPC amezungumza ni tofauti kabisa.
Hakuna driver anayeingia barabarani ili akapate ajali bali huwa ni miscalculation tu hutokea. Hivyo tusiweke speculation nyingi za kuwalaumu hata bila kuwasikiliza kujua kipi kilitokea.
 
Dah unakuta hapo abiria wa irnga mjin wameshuka zao salama..mbelen wenzao umauti unawakuta...yaan maisha bna yaani hata unachokitafuta muda mwingine hata hufaham...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…